Thursday 31 October 2013

‘Tunataka majina ya vigogo majangili

Dodoma. Wabunge jana walichachamaa na kushinikiza kutolewa kwa orodha ya vigogo wanaojihusisha na ujangili wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa 13 wa Bunge unaofanyika mjini Dodoma.
Wabunge hao walitaka kutajwa kwa majina ya mawaziri, viongozi wa Serikali na wabunge wanaojihusisha na biashara hiyo.
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, aliomba mwongozo, akiitaka Serikali kuwataja hadharani na kuwachukulia hatua viongozi wake na wanasiasa, wakiwamo mawaziri na wabunge, ambao wanatajwa kuhusika na vitendo vya ujangili nchini.
Lugola aliomba mwongozo wa Naibu Spika baada ya kutoridhishwa na jibu lililotolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli.
Katika jibu hilo, Nyalandu alilieleza Bunge kuwa Operesheni Tokomeza inayolenga kukomesha vitendo vya ujangili nchini bado inaendelea, lakini alishindwa kulieleza Bunge ni nani hasa wamebainika kuhusika na vitendo hivyo.
Lugola, hata hivyo, aliitaka Serikali kuwasilisha ripoti bungeni kuhusiana na utekelezaji wa operesheni hiyo.
“Tangu Aprili tumekuwa tukipewa majibu mepesi kuhusiana na operesheni hii, wakati suala hili si la masihara,” alionya Lugola.
Lugola alisema kuwa taarifa zimewataja watu wanaohusika na vitendo hivyo wakiwamo viongozi serikalini, mawaziri pamoja na wabunge, lakini tangu operesheni hiyo ilipoanza hakuna yeyote miongoni mwa hao wanaotajwa ambaye amekamatwa isipokuwa wananchi wa kawaida.
Alisema operesheni hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa unyama kwani wanaokamatwa hupigwa na kuteswa bila ya ushahidi unaoonyesha kuhusika kwao na vitendo vya ujangili.
“Inashangaza sana kuwa wale wanaotajwa hawachukuliwi hatua, lakini wananchi wanazidi kuteseka… Mathalani, zipo taarifa kuwa wakuu wa polisi katika mikoa inayopakana na Mbuga ya Serengeti ndio waratibu wa shughuli za ujangili, lakini hatujasikia hao wakichukuliwa hatua,” alisema.
Kabla ya Naibu Spika kutoa majibu ya mwongozo ulioombwa na Lugola, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisimama na kukiri kuwapo kwa vitendo vya utesaji wa watu wanaokamatwa katika operesheni hiyo.
Alitolea mfano tukio la kukamatwa kwa msaidizi wake jimboni ambaye alipigwa na kuteswa na askari hao kabla ya kuachiwa baada ya kushikiliwa kwa siku moja, huku akionyesha kuwa ushahidi wa tukio hilo anao kwenye simu yake.

“Lakini sisemi haya kwa kutaka kuitetea Serikali kuwa isilete ripoti hapa bungeni. Nadhani kuwa kuleta ripoti hivi sasa haitakuwa vizuri. Ni vizuri tusubiri mpaka kazi hii ikamilike na nina uhakika kuwa Wizara itaandaa ripoti na kuiwasilisha kwenye kamati husika,” alisema na kuongeza:
“Nadhani kuwa `entry point’ (mahali pa kuanzia) yetu iwe ni kwenye ripoti hii itakayowasilishwa kwenye Kamati,”
Suala la ujangili limeingizwa bungeni wakati kukiwa na usiri mkubwa wa nani anahusika na vitendo hivyo, huku majina ya vigogo wanaotajwa kuhusika nayo wakiwa hawafahamiki.
Polisi watajwa vinara
Awali akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndugulile, Nyalandu alisema Jeshi la Polisi ni vinara miongoni mwa makundi manne ya majeshi ambayo watumishi wake wamekamatwa wakijihusisha na ujangili.
Katika matukio saba ya ujangili yaliyowahusisha watumishi tisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, Nyalandu alisema kati ya hao sita ni polisi wakati kwa kupande wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza alikamatwa mtu mmoja mmoja.
“Katika matukio hayo, jumla ya meno ya tembo 686 na vipande 447 vikiwa na uzito wa kilogramu 4,253.9 vilikamatwa, jambo ambalo linaonyesha ukubwa wa tatizo hilo kwa vyombo vya ulinzi,” alisema Nyalandu.
Katika swali la msingi, Dk Ndugulile alitaka kufahamu idadi ya matukio ya upatikanaji wa pembe za ndovu yaliyohusisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika swali la nyongeza, Lembeli ambaye ndiye aliyeuliza swali hilo kwa niaba ya Dk Ndugulile, aliitaka Serikali kuacha kigugumizi na kueleza ukweli kuwa wapo baadhi ya viongozi, wakiwamo wabunge ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo.
“Katika biashara ile kuna hali ya kulindana sana, hebu Serikali itueleze taarifa za kuwa wahusika wengine ni wanasiasa na baadhi ya wabunge, ukweli uko wapi, na kuna taarifa kuwa viongozi wa Polisi wanaoishi kuzunguka hifadhi zetu ndio ambao wanatumiwa kusafirisha nyara hizo, Serikali inasemaje?” alihoji Lembeli.
Nyalandu alisema Tanzania iko katika hali mbaya katika kiwango cha mauaji ya tembo ambapo wastani unaonyesha kuwa kila siku tembo 30 huuawa na majangili.
“Hata hivyo, suala la ulinzi bado tuko nyuma sana kwani wastani wa ulinzi wa kimataifa ni askari mmoja kwa kilomita za mraba 25, lakini sisi askari wetu mmoja analinda kilomita za mraba 150 ndani ya hifadhi,” alisema Nyalandu.
Serikali yakiri tatizo
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha akizungumza bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, alikiri kuwapo fununu za wanasiasa ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo na kusema Serikali italifanyia kazi jambo hilo.
Nahodha aliwataka Watanzania kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaposhughulika na kusafisha tatizo hili na kuonya wanasiasa kuacha kutoa shinikizo kwa kutumia nguvu zao za kisiasa.

Kapt Komba ajitoa mhanga, asema Lowassa Rais 2015

Dar es Salaam. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni Mstaafu, John Komba amevunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye uchaguzi wa 2015.
Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kwa rais 2015.
Itakumbukwa Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM) naye alivunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Kikwete.
Shelukindo alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.
Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Komba ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Lowassa.
Komba aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.
“Nakuambia Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais... unafikiri kuna mwingine. Nina sababu zangu tatu,” alisema Komba na kuhoji:
“Wewe unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia kwa fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo Lowassa?”
alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM, katika kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa, Komba alisema: “Mimi sikwambii ni nani, lakini wapo Mawaziri waliomkana, lakini leo hii wapo kwenye Serikali hii hii ya Rais Kikwete.
“Mimi nasema Lowassa, na kama akipita sawa nitaburudiiika kwelikweli, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua, nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wanaCCM ule si wa Komba.” alisema.
Mbali na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na hata wananchi wanakikubali.
Akizungumzia suala la rushwa ndani ya CCM, Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga, alisema kama chama kuna watu wa aina nyingi, kuna wasafi, kuna wachafu lakini wote wako kwenye mstari mmoja
Alisema kuwa vita ya rushwa ndani ya CCM itamalizika endapo kila kiongozi atasimamia kwenye haki na maadili ya uongozi na pia kutambua wajibu wake ndani ya chama.Komba alijipigia upatu kuwa ameleta maendeleo katika jimbo lake kwani jimbo linatazamika ikilinganisha na miaka ya nyuma kuwa wananchi walikuwa wakiishi maisha ya tabu na kimaskini ilhali wana raslimali za kutosha.

Sare za polisi: Ney wa Mitego asimulia kilichotokea

Dar es Salaam. Siku chache baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kutumia sare za polisi bila kibali katika video ya wimbo ‘Salamu Zao’, na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Urafiki Manzese Jijini Dar es Salaam, rapa wa muziki wa kizazi kipya, Ney Wa Mitego amesimulia mkasa mzima na kusisitiza kuwa wabaya wake ndiyo waliycheza mchezo huo.
Akizungumza na Mwananchi, rapa huyo alisema sare hizo za polisi zilishonwa kwa ajili ya kazi hiyo na wala hazikuwa sare halisi za kipolisi.
“Mavazi haya ya kipolisi yalikuwa rasmi kwa ajili ya kutengeneza video ya Salamu Zao na hayakuwa halisi, ila nilishangaa pale nilipokamatwa na watu wasiojulikana jumamosi ya wiki iliyopita wakati tukitengeneza video, wakidai kwamba wao ni askari.Walinichukua hadi kituo cha urafiki, pale niliwekwa sero kwa kipindi cha dakika 20 hivi, baada ya kutoa maelezo ya kutosha niliachiwa”.
Baada ya kuachiwa, alirudi na kukamilisha kazi yake ambayo ameweka wazi kuwa itakuwa hewani wiki hii.
“Video ya Salamu Zao itaachiwa hewani Ijumaa ya wiki hii, hivyo watarajie kitu kipya na adimu kuonekana,” alisema Nay na kuongeza “Sijajua bado ni nani aliyenichomea lakini naahidi kuwa itaendelea kula kwao wale wote wanaonichukia na kamwe siwezi kuacha kuusema ukweli.”
Uongozi wa kituo cha Polisi Urafiki jijini Dar es Salaam ulithibitisha kumtia mbaroni msanii huyo kwa kukutwa akitumia sare zinazofanana na mavazi ya polisi kinyume cha sheria. Ofisi mmoja wa polisi ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini anasema waliamua kumuachia kwa vile waliridhika na maelezo yake.

Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

Dodoma. Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
“Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?” chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa,” alisema Dk Kashililah.
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
“Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo,” alisema Dk Kashililah.
Kuhusu Serukamba
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
“Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema Dk Kigwangalla alisema badala ya kumweka karibu katika ushiriki, Mgimwa alipokwenda katika kamati hiyo aliambulia kufukuzwa.
Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti Kuu ya Serikali.
Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki katika Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed (Wawi - CUF).
Kanuni za Bunge
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja hiyo.
Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.
Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati hiyo itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyo itaidhinisha hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.
Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote.

Babu Seya, watoto wake ‘watupa karata’ nyingine

Dar es Salaam. Mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na wanawe kupitia Wakili Mabere Marando wameiomba Mahakama ya Rufaa, ifanye marejeo kuhusu hukumu iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani na adhabu ya kifungo cha maisha jela wanayoitumikia.
Marando aliliwasilisha ombi hilo, kwa takribani saa 2 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo .
Jopo hilo linaongozwa na Jaji Nathalia Kimaro, akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Salum Massati.
Wakili huyo alisema wateja wake wanaoomba mahakama ifute ushahidi uliowatia hatiani washtakiwa na badala yake iwaachie huru.
Upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka, uliwakilishwa na mawakili Jacksoni Mlaki, Angaza Mwaipopo, Emakulata Banzi, Joseph Pande na Apimack Mbarouk.
Hata hivyo mawakili hao waandamizi wa Serikali, waliyapinga maombi hayo kuhusu marejeo kwa madai kuwa yamepelekwa mahakamani bila usahihi.
Marando alidai kuwa mahakama iliteleza katika kutoa uamuzi uliowatia hatiani na kuwafunga maisha Babu Seya na watoto wake na kwamba kuteleza huko kunaonekana wazi wazi.
Alifafanua kuwa wakati wakifanya majumuisho ya kesi hiyo, mahakama ilijiridhirisha kuwa kulikuwa na makosa katika kupokea ushahidi wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuatwa kwa taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa mtoto.
Alisema kwa msingi huo, ushahidi huo ulipaswa kufutwa.
“Katika hukumu yenu mlikubaliana na sisi kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kupokea ushahidi wa watoto , ila mlisema hiyo si hoja maadam kuna ushahidi unaounga mkono ushahidi huo ni bora,”alilalamika Marando.
Alieleza kuwa mtoto mdogo anapotoa ushahidi licha ya tahadhari, ana uwezo wa kutambua zuri na baya na kwamba lazima ushahidi wake uwekwe kwenye kumbukumbu ya maandishi na kwamba usipoonekana ushahidi wote ni batili na uondolewe.
Aliendelea kueleza kuwa kwenye hukumu wanayoilalamikia, anaiomba mahakama ijisikie kubadili uamuzi wa kuwafunga maisha wateja wake.
“Tuanaomba ushahidi wa wale watoto ufutwe, uondolewe mahakamani na washtakiwa waachiwe huru,”alisisitiza.
Upande wa mashtaka ulipaswa kuwaita mashahidi hao lakini nyie majaji katika hukumu yenu mlisema upande wa mashtaka uanahiari ya kumwita shahidi wanayemtaka wao.

Friday 25 October 2013

Rais wa Uswisi aifunda Tanzania jinsi ya kupata fedha za kifisadi


0
S

Katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa Mwananchi na The Citizen jana, Graf alisema kuwa Serikali ya Tanzania inapaswa kusaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa za masuala ya usimamizi wa fedha na kodi ili kuweza kujua ni kina nani wameweka fedha nchini kwake na kunufaika na kodi.
Graf, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini, alisema kuwa hivi karibuni Serikali ya Uswisi ilisaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa kuhusu masuala ya fedha, ambao unajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama `Convention on Mutual Administrative Assistance in Tax Matters’.
Alisema ikisaini mkataba huo ina maana itasaidiwa na Serikali ya Uswisi kupata fedha zilizofichwa na Watanzania.
“Serikali ya Tanzania inatakiwa kuweka mkakati wa kisheria utakaotengeneza mazingira ya kubadilishana taarifa za fedha na mataifa mengine. Kwa jambo hilo hata Serikali ya Uswisi inaweza kusaidia katika kupatikana kwa fedha zilizofichwa,” alisema Graf, ambaye anaongoza Serikali ya Uswisi kwani kwa kawaida Rais wa Bunge ndiye pia kiongozi wa taifa hilo.
Graf alisema kwa sasa itakuwa ngumu kwa Tanzania kupata fedha hizo kwani haijasaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa za fedha na mataifa mengine.
Alieleza pia katika miaka ya karibuni Serikali ya Uswisi imeandaa muswada wa sheria wa kubana fedha zilizopatikana kwa njia za kifisadi na kufichwa katika benki za Uswisi. Graf alisema sheria hiyo ikipita itaruhusu Serikali ya nchi hiyo kutaifisha fedha ambazo zimepatikana kwa njia haramu na kufichwa katika benki za huko.
Muswada huo unaoitwa kwa lugha ya Kiingereza `Freezing and Restitution of Assets of Politically Exposed Persons obtained by Unlawful Means Bill’ ulisomwa kwa mara ya kwanza kwenye Bunge la nchi hiyo mwezi Mei, mwaka huu.
Graf alisema faida nyingine ya Tanzania kusaini mkataba huo ni kuwa, itaweza kuwatoza kodi Watanzania hao walioweka fedha huko.
Alifafanua kuwa siyo fedha zote zinazowekwa kwenye benki za Uswisi kuwa ni haramu kwani kuna nyingine zimepatikana kihalali, lakini zinaweza kutozwa kodi.
“Tanzania inakosa kodi kutokana na fedha zilizohifadhiwa na Watanzania wenye akaunti kwenye benki za Uswisi,” aliongeza Graf, ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo Novemba 26, 2012 na kutakiwa kukaa madarakani kwa mwaka mmoja.
Graf alisema pia fedha za kodi zingeisaidia Tanzania kugharimia sekta mbalimbali za maendeleo.
Zito aitupia lawama Serikali
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, ambaye yuko nchini Uswisi akifuatilia masuala ya utoroshaji fedha na kufichwa kwenye benki za huko, alisema kuwa wakati shinikizo la dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Afrika, lakini Serikali ya Tanzania inasuasua juu ya kupambana na jambo hilo.
Zitto alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za kampuni kubwa za kimataifa yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa unaoitwa kwa lugha ya Kiingereza `automatic exchange of tax information’.
“Kutokana na shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa `tax havens’ (nchi zinazohifadhi fedha kwa siri) fedha zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Alisema kuwa Tanzania mpaka sasa haijaweka saini na Serikali haijatoa taarifa yoyote kwa umma juu ya sababu ya kutokufanya hivyo. “Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari,” aliongeza Zitto.Alisema asilimia 44 ya fedha za kigeni inazopata Serikali ya Tanzania zinatokana na mauzo ya madini nje. Kampuni za madini ndizo zinazoongoza kukwepa kodi.
Alisema Tanzania inapoteza jumla ya Dola 500 milioni (Sh783 milioni) na Dola 1.25 bilioni (Sh2 trilioni) kwa mwaka kutokana na kampuni kubwa za kimataifa kukwepa kodi.
“Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza Dola2 milioni (Sh3.1 bilioni) kila siku kwa uporaji huu,” alisema Zitto.
Zitto alisema Serikali lazima ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi.
Jaji Werema agoma kujibu
Alipoulizwa juu ya Tanzania kutokusaini mikataba ya kimataifa ya kubadilishana taarifa za utoroshaji fedha na mambo au kodi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema hawezi kujibu suala hilo.
“Muulize huyo aliyekwambia kuwa Tanzania haijasaini mikataba ya kubadilishana taarifa za utoroshaji fedha na masuala ya kodi. Naomba uniache nifanye kazi zangu,” alijibu Jaji Werema kwa mkato na kukata simu.
Mahojiano kamili na Rais wa Uswisi, soma Mwananchi Jumapili.

Wednesday 23 October 2013

Mshahara wa mwajiriwa wa wananchi unakuwaje siri


Share

Dar es Salaam. Ni ajabu kusikia kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kuhusu mishahara wanayolipwa Rais na Waziri Mkuu inazusha mjadala mkubwa.
Zitto akiwa wilayani Igunga hivi karibuni, alijitoa mhanga na kutangaza viwango alivyodai  kuwa ni mishahara ya rais na waziri mkuu kwa mwezi, huku akihoji iweje viwango viwe siri na visikatwe kodi.
Baadhi ya watu wamepinga hatua hiyo wakisema mshahara wa mtu ni siri yake. Waliopinga ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai na Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma, Celina Kombani akisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Sawa, inaweza kuwapo sheria inayozuia jambo hilo, lakini kwanini itungwe sheria ya namna hiyo?
Kwa upande wangu naunga mkono mishahara hiyo kuwa wazi. Nakubali kwamba mshahara wa mtu ni siri yake, lakini kwa viongozi wa umma kama rais na waziri mkuu, mishahara yao haipaswi kuwa siri, ndiyo maana nchi nyingi duniani zikiwemo Marekani, Ufaransa, Kenya na Afrika Kusini, mishahara ya viongozi kama huwekwa wazi.
Ifahamike kuwa rais ni kiongozi anayechaguliwa na wananchi, wao ndiyo wanaompa ajira ya kuwatumikia. Iweje mwajiri asijue anacholipwa mtumishi wake?
Kwenye nchi zilizoendelea kidemokrasia kama vile Marekani na nchi za Ulaya, masilahi na utendaji wa rais na waziri mkuu na viongozi wengine ni ya kikatiba.
Wananchi wanajua wazi kabisa, rais wanayemchagua watamlipa kiasi gani, Katiba inamwelekeza rais ateue mawaziri wangapi na watendaji wa Serikali kwa idadi maalumu.
Cha ajabu huku kwetu, rais anaamua kufanya atakavyo – anaweza hata kuteua mawaziri idadi anayoitaka na asiulizwe, mambo yanafanywa kwa siri ndiyo maana hata mikataba ya madini na uwekezaji mwingine ni siri.
Siri hizi za nini kama sisi wananchi ndiyo tumeichagua Serikali yetu wenyewe?
Hoja nyingine ni kuhusu mshahara wa rais kutokatwa kodi. Rais ni mtumishi wa umma namba moja na mlezi wa watumishi hata wa sekta binafsi.
Kwa muda mrefu wafanyakazi wamekuwa wakilalamikia kiwango cha asilimia 15 cha kodi wanayokatwa katika mishahara ndiyo ikashushwa hadi asilimia 14, hata hivyo bado ni mzigo.
Lakini rais atauonaje mzigo huo ikiwa yeye hakatwi kodi? Rais kwa mujibu wa Zitto analipwa wastani wa Sh32 milioni kwa mwezi bila kukatwa kodi, ana marupurupu ya safari za ndani na nje ya nchi na posho nyinginezo.
Kwa maana nyingine rais anaweza asiuguse kabisa mshahara wake kwa posho hizo, lakini bado akistaafu analipwa pensheni na atatunzwa na Serikali maisha yake yote.
Tuna viongozi wa Serikali wangapi wanaolipwa hivi, tuna marais wastaafu na mawaziri wakuu wangapi wanaofaidi kiinua mgongo cha Serikali huku idadi kubwa ya Watanzania ikiteseka katika lindi la umasikini na mlolongo wa kodi?

Vyama vya siasa vimebadilika kifikra’



Dar es Salaam. Baadhi ya wasomi jijini Dar es Salaam, wamevipongeza vyama vya siasa kwa kitendo cha kukubaliana kuhusu maboresho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuifanya Serikali kuandaa hati ya dharura.
Wasomi hao wamesema vyama hivyo vimeonyesha kubadilika kifikra.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema ili nchi iweze kupata Katiba Mpya yenye masilahi kwa nchi husika, lazima wananchi na vyama vya siasa wakubaliane na kuwa kitu kimoja, jambo ambalo limedhihirika juzi.
Mwanasheria maarufu, Profesa Chris Peter Maina alisema, “Vyama vimetoa hoja nzito kuhusu kasoro zilizomo katika sheria husika, pamoja na kuamua kuweka kando tofauti zao na kuungana, binafsi nimependa zaidi hoja zao za msingi zilizolenga masilahi ya taifa kuliko vyama vyao.”
Profesa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, alisema hata wabunge wa vyama hivyo wanapaswa kuwa kitu kimoja katika kupitisha mabadiliko hayo.
Mwanasheria mwingine, Berious Nyasebwa alivipongeza vyama hivyo na kusisitiza kuwa uamuzi uliochukuliwa umejaa busara na hekima.
“Hoja hii ya Serikali sidhani kama itapingwa na wabunge ikifika bungeni, wanasiasa wameamua kukubaliana na wametambua wazi kuwa tendo la kuandika Katiba Mpya ni la maridhiano si la mtu binafsi wala chama fulani” alisema Nyasebwa.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala alisema, “Binafsi nimepata matumaini mapya juu ya mchakato huu baada ya vyama kuamua kuweka kando tofauti zao. Kilichofanyika ni mageuzi ya kifikra.”
Hata hivyo Profesa huyo alisema kulikuwa na ulazima kwa tume hiyo iliyokuwa imalize kazi yake Novemba 1 kuomba kuongezewa muda, kwa maelezo kuwa bado ilihitaji kufanya uchambuzi wa maoni mbalimbali, ili kukamilisha rasimu ya pili ya Katiba.
“Sidhani kama muda ulioongezwa utaathiri mchakato mzima wa Katiba.”

Vatican yamsimamisha askofu Mjerumani kwa kupenda raha

Kumekuwa na kelele za waumini nchini Ujerumani wakishinikiza askofu huyo afukuzwe kwa kukiuka taratibu.
Vatican City. Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani (Vatican) yamemsimamisha kazi Askofu wa Jimbo la Limburg, Ujerumani Franz-Peter Tebartz-van Elst anayekabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha kwa shughuli za kifahari.
Vatican ilieleza jana kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuridhika kuwa Askofu van Elst amekiuka maadili yaliyowekwa na Papa Francis kwa viongozi walioko chini yake akiwataka waishi maisha ya uchaji, umaskini.
Hadi sasa, kumekuwa na kelele nyingi miongoni mwa waumini nchini Ujerumani wakitaka askofu huyo afukuzwe kazi.
Miongoni mwa matumizi yake makubwa ni ujenzi wa makazi yake binafsi yaliyogharimu Euro 2.9 milioni (Dola 3.9 milioni), ukumbi wa chakula wenye mita za mraba 63 ambao ni pamoja na mesi na bafu yenye thamani ya Euro 15,000.
Askofu van Elst (53) amekuwa akituhumiwa kuendesha miradi hiyo kwenye mji wa kihistoria wa Limburg, ikiwamo makumbusho, kumbi za mikutano, kanisa dogo na nyumba ya makazi yake binafsi.
Fedha hizo zinatokana na mapato ambayo ni misamaha ya kodi kwa vikundi vya kidini nchini Ujerumani kwa mujibu wa sheria.
“Baada ya uchunguzi wa awali, Vatican imeamua kuchukua hatua kumsimamisha na kumwondoa kwenye usimamizi wa jimbo,” ilieleza taarifa hiyo.
“Baba Mtakatifu (Francis) amekuwa akifuatilia kwa karibu mambo yote yanayoendelea katika Jimbo la Limbuerg,” iliongeza taarifa hiyo.
“Hali hiyo imefikia mahali ambako kiongozi huyu hawezi kuendelea kusimamia kazi zake za kitume kama askofu wa jimbo.”
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza ni kwa muda gani Askofu van Elst amesimamishwa kazi, ila iliongeza kuwa itategemea na kukamilika kwa uchunguzi, tathmini ya hali ya fedha ya jimbo na mambo mengine.
Wiki iliyopita, Askofu van Elst alisafiri hadi mjini Rome, Italia kwa ndege ya shirika la gharama nafuu, Ryanair kujieleza mbele ya Papa Francis – kutokana na madai kuwa alisafiri mwaka jana kwa ndege ya daraja la kwanza kwenda India na pia kutumia vibaya fedha.
Taarifa za matumizi hayo makubwa ya kiongozi huyo zimelitikisa Kanisa Katoliki la Ujerumani huku wengi wakitaka uwazi katika matumizi ya fedha -- mageuzi ambayo Papa Francis amekuwa akiyapigia kelele na kutaka kanisa maskini kwa watu maskini. Miradi hiyo kwa pamoja ambayo iliidhinishwa na mtangulizi wake awali ilikadiriwa kutumia Euro 5.5 milioni, lakini iliongezeka kwa kiasi cha kutisha na kufikia Euro 31 milioni ikiwamo bustani yenye thamani ya Euro 783,000.
Pia, Askofu Tebartz-van Elst anatuhumiwa kwa kutoa taarifa za uongo mahakamani kuhusu safari yake ya India kutembelea familia maskini.
Waendesha mashtaka wa Serikali wanaeleza kuwa askofu huyo alitoa taarifa za uongo chini ya kiapo kwenye mahakama ya mjini Hamburg dhidi ya gazeti la kila wiki, Der Spiegel akikana safari ya India anakodaiwa kutumia daraja la kwanza. Matumizi makubwa ya askofu huyo yameudhi walipa kodi wa Ujerumani wakidai kwamba wanakamuliwa huku fedha zikitumiwa vibaya na wengi wao kuandamana nje ya makazi ya askofu huyo.
Kansela Angela Merkel, binti wa kiongozi wa zamani wa Kipentekoste amesema kupitia msemaji wake, Steffen Seibert kwamba ana matumaini Kanisa Katoliki litamaliza tatizo hilo kwa jina la Yesu. Askofu Tebartz-van Elst hata hivyo ametetea miradi yote akieleza inalenga kudumisha mila na historia ya eneo hilo.
Tangu kuingia madarakani kwa Papa Francis, kumekuwa na kasi ya mabadiliko ndani ya kanisa.

Uswisi sasa kurejesha mabilioni ya mafisadi

Dar es Salaam. Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.
Akizungumza na gazeti hili, Zitto alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.
Alibainisha kuwa tangu kuibuka kwa sakata hilo mwaka 2012 na Bunge kuiagiza Serikali kufuatilia, Serikali haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi kuhusu Watanzania waliohifadhi fedha nchini humo.
“Jana nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi (Multilateral convention on administrative assistance in tax matters),” alisema Zitto na kuongeza;
“Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata kipato halali lazima alipe kodi.”
Zitto alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi au la.
“Kiufupi, Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi. Ila Uswisi wamebadili sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo anapaswa kuthibitisha kwamba ni safi, na ikithibitika kuwa hazina mwenyewe wala maelezo, zitarudishwa nchi husika,” alisema.
Zitto alisema mbali na kukutana na watendaji hao wa Serikali amezungumza na Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha kuwa Uswisi ina Watanzania wachache wenye fedha.
“Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza, Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana,” alisema Zitto. Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
“Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa. Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Hivi sasa hawapokei pesa kutoka nchi za Afrika au wanapokea kwa tahadhari sana, maana kuna reputational risk (kupoteza heshima),” alisema.
Wito wa timu ya uchunguzi
Zitto alipendekeza timu iliyoundwa kuchunguza fedha hizo itoe taarifa yake kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29, mwaka huu, akieleza kuwa, “Kuendelea kukaa na taarifa, kutaongeza tetesi za kweli au za uwongo.”
Alisema mpango huo wa kusaka fedha zilizofichwa nchini Uswisi, umelenga zile zilizofichwa na watu binafsi kutokana na rushwa au kuuza dawa za kulevya na kampuni kubwa za kimataifa.
Alibainisha kuwa wengi waliotambulika ni wanasiasa, vigogo wa jeshi na wakuu wa mashirika ya umma na watendaji wa Serikali.
“Katika mabenki ya Uswisi, kuna kiasi cha Dola za Marekani 197 milioni. Fedha nyingi zipo katika benki za Uingereza na visiwa vyake, Dubai na Mauritius,” alisema na kuongeza;
“Wapo watu waliopata fedha kihalali, lakini wanaficha fedha hizo na mali zao nje ili kukwepa kodi. Wengi wa hao ni wafanyabiashara wakubwa nchini. Tanzania inapoteza Dola za Marekani 1.25 bilioni kati ya mwaka 2001 na 2012 kwa njia hizi.”
Alibainisha kuwa Tanzania lazima itunge sheria ya kufilisi mali ambazo mtu anashindwa kuthibitisha amezipataje.
“Tayari ninafanyia kazi muswada binafsi wa sheria wa kubadilisha sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1991. Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
Madai hayo ya Zitto yamekuja ikiwa umepita mwaka mmoja tangu Bunge kuipa Serikali muda wa kuchunguza sakata la vigogo walioficha mabilioni katika benki za Uswisi.
Zitto ndiye aliibua sakata hilo mwishoni mwa mwaka 2012. Kufuatia hoja hiyo, Serikali iliunda timu kutokana na Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana.
Werema ahoji Mwananchi

ni Bunge?
Timu hiyo inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye jana baada ya kutafutwa na gazeti hili alisema, “Uchunguzi kuhusu walioficha fedha Uswisi bado haujakamilika.”
Viongozi wengine wanaounda tume hiyo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa ripoti hiyo kuwekwa wazi katika Mkutano ujao wa Bunge, Werema alisema, “Kwa nini, kwani wewe ndiyo Bunge. Uchunguzi bado unaendelea”
Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
Alipoulizwa kuhusu ripoti hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai alisema, “Wiki ijayo katika kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali itatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi huo na kama haujakamilika kikao hicho kitaamua jambo la kufanya na endapo uchunguzi utakuwa umekamilika zitapangwa taratibu za kuiwasilisha ripoti bungeni.”
Waziri wa Fedha anena
Naye Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema jana kuwa sheria za kimataifa zipo wazi kwamba fedha chafu zinazogundulika kufichwa nchi fulani, hurejeshwa katika Serikali ya nchi husika.
“Lengo la sheria hizi za kimataifa ni kuhakikisha kuwa fedha za wizi zinazoibwa nchi fulani, haziwezi kuhifadhiwa katika nchi nyingine,” alisema.
Alipoulizwa kama wizara yake ina taarifa zozote kuhusu Watanzania walioficha fedha Uswisi alisema, “Kuna Tume iliundwa na Bunge kufuatilia suala hilo nadhani ndiyo itakuwa na majibu sahihi.”
Uchunguzi wa walioficha mabilioni ya Uswisi uliibuka baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mapema Juni 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo inadaiwa kuwa na majina ya baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola 196 za Marekani milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.

Elimu ya Tanzania iko mahututi’

Dar es Salaam. Siku moja baada ya maudhui ya Ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kuwekwa wazi, wadau wa elimu wamekiri na kusema kuwa mfumo wa elimu ya Tanzania upo katika hali mbaya.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia alisema matokeo ya tume hiyo yanaonyesha udhaifu wa hali ya juu katika sekta ya elimu jambo ambalo alishawahi kulisema katika hoja maalumu bungeni.
Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, alisema alishawahi kuishauri Serikali kuufumua mfumo wa elimu nchini na kuanza upya ili kunusuru taifa la kesho ambalo ndilo linaloathirika na rasilimali watu zisizo na ubora.
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana yalionyesha kuwa asilimia 60.6 ya wanafunzi Tanzania walipata alama sifuri na wanafunzi 23,520 sawa na asilimia tano ndiyo waliofaulu jambo ambalo lilisababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza matokeo hayo.
Baadaye, mitihani hiyo ilisahihishwa upya na Pinda kukabidhiwa matokeo Juni, mwaka huu.
“Nilishasema katika hoja yangu bungeni Januari 31 na Februari 1, mwaka huu nikamwomba waziri anionyeshe mitaala ya elimu ya sasa, lakini hakuitoa,” alisema Mbatia.
Mbatia alisema ili taifa hili liondokane na janga la elimu lililopo halina budi kukubali kuwa ni kweli Tanzania ipo katika janga la elimu na kuunda dira ya elimu itakayotuongoza katika safari ya elimu nchini.
Mbatia aliongeza kuwa elimu ya Tanzania ipo mahututi na kuwa kila mwaka wanafunzi wanaomaliza katika shule mbalimbali hawana sifa za kutosha za kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa.
“Tumeshaanza kuona taifa linaangamia kwa sababu ya ubovu wa elimu, ni lazima tukiri hilo kwa sababu hata Rais alikiri na kuikubali hoja yangu Aprili 30 mwaka huu alipokuwa mkoani Mbeya” alisema Mbatia
Mbunge huyu ambaye awali aliteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa tume ya uchunguzi wa matokeo haya na kukataa kushiriki alisema, ili Serikali iondokane na janga hili haina budi kuunda Kamati ya Bunge ambayo itaisimamia Serikali na kutoa mawazo mapana kuhusu elimu.
Mbatia alishauri Bunge lisiegemee itikadi za vyama au porojo za kutaka sifa za kisiasa na badala yake suala la elimu lijadiliwe kwa maslahi ya taifa.
Mdau mwingine wa elimu, Dk Method Samwel, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUSE), alisema tatizo la elimu hapa nchini lielekezwe zaidi kwenye mfumo uliopo kuliko laumu taasisi au mtu mmoja mmoja

Dk Samwel alisema tangu zamani mfumo wa elimu umekuwa ni wa kudorora na haya ni matokeo ya mfumo huo ambao haukuwa na misingi imara kwa muda mrefu.
Alitolea mfano wanaokwenda kusomea ualimu wengi ni wale waliofeli kwa kupata daraja la nne, jambo ambalo linasababisha wataalamu wa kada hiyo kuwa ni wale waliofeli pekee.
“Yapo mambo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi katika sekta ya elimu Tanzania, suala la kudai kuwa Baraza la Mitihani na Taasisi kuwa ndizo taasisi zenye makosa, hazina ukweli,” alisema.
Hata hivyo, Dk Samwel alisema, tume hiyo bado ina maswali mengi ya kujibu kulingana na walichokisema katika sehemu ya ripoti yao.
“Nashindwa kuelewa kwa sababu kila nikisoma majibu ya tume hiyo napata maswali mengi zaidi. Kwa mfano, walimu waliofanya mtihani wakafeli walipewa muda wa kujiandaa? “ alihoji na kuongeza:
“Na kuhusu mitihani ya Tanzania kuonekana kuwa ni migumu zaidi, Je waliwapa mitihani ya Tanzania wanafunzi wa nchi nyingine au walitumia mbinu gani kupata matokeo hayo?”
Hata hivyo, Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo, alipinga ripoti ya tume hiyo na kusema kuwa wamepotosha taarifa kwani tatizo halikuwa katika mtihani bali ni wanafunzi wenyewe wamefeli.
Dk Mkumbo amesema tatizo si la walimu, wala baraza, wala mitihani yenyewe bali ukweli utabaki kuwa wanafunzi walifeli mtihani wa Kidato cha Nne kwa sababu ya mfumo mbovu wa elimu.
Mhadhiri huyo alihoji tena kuwa tume hiyo ilitumia njia gani kujua kuwa mtihani wa Sayansi ulihitaji saa sita kuufanya na ni kwa mbinu gani waliupima mtihani wa Tanzania na kujua kuwa ni mgumu kuliko mitihani mingine.
“Nilipata ripoti fulani iliyoonyesha kuwa mitihani ya Tanzania ni mizuri na haina matatizo, ripoti ilionyesha kuwa haina chembe ya mashaka na inatungwa kwa ustadi. Tusitafute sababu, tatizo si mitihani ni wanafunzi wenyewe wamefeli,” alisema.
Pia, Dk Mkumbo alisema kuwa ni dharau kubwa kusema kuwa baadhi ya wasahihishaji hawakuwa na sifa kwani hilo ni tusi kubwa kwa walimu kwani wao ndiyo wamekuwa wakisahihisha kila siku.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini,(Tamongsco), Albert Katagira alisema si kweli kuwa mtihani ulikuwa mgumu bali tatizo lipo katika uandaaji wa wanafunzi.
 “Mtihani ulikuwan sahihi kabisa, mbona wanafunzi wengine walifaulu. Ni wanafunzi wenyewe, ambao nao hatuwezi kuwalaumu moja kwa moja,” alisema Katagira.
Alisema taifa bado lina tatizo katika mfumo wa elimu na kuweka mkazo katika masomo ya sayansi na hisabati ambayo yanaonekana kuwa magumu kwa wanafunzi wengi.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mafinga, Mustapha Mambea alisema, mtihani wa Fizikia na Kemia haikuwa migumu, lakini kuna mada kadhaa ambazo hawakufundishwa.
Profesa Mchome aongea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema kuwa wameshindwa kuiweka hadharani ripoti hiyo kwa kuwa bado inafanyiwa kazi serikalini.
Profesa Mchome, ambaye ndio aliongoza tume hiyo, alisema kuwa ripoti hiyo inatakiwa kupelekwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa.
Alidokeza, hata hivyo, tayari walikuwa wameanza kufanyia kazi baadhi ya vitu vinavyotakiwa kufanyiwa kazi haraka kwenye ripoti hiyo.
Katibu Mkuu wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, ambaye ameomba likizo ya muda mrefu ikitafsiriwa pengine ndio mwanzo wa utekelezaji wa ripoti hiyo.

Friday 18 October 2013

Ubabe wa Dk Magufuli unaumiza uchumi wa nchi


Tumeshuhudia mvutano kati ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) ambao wanapinga sheria ya tozo ya asilimia tano kwa wasafirishaji wanaozidisha mizigo na kusababisha uharibifu wa barabara.
Mbali na Tatoa, Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) pia wanapinga sheria hiyo ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 2001.
Waziri Magufuli alisema anasimamia sheria hiyo ili kuhakikisha barabara haziharibiwi na watu wachache wenye nia ya kujinufaisha binafsi bila kujali masilahi ya Taifa.
Hata hivyo wamiliki hao kupitia Tatoa walisema Waziri huyo amerudisha tozo ya asilimia tano kwa maslahi yake na amekuwa mtu ambaye haambiliki, hashirikiani na wadau pamoja na kujichukulia sheria mkononi.
Wakizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wamiliki hao walieleza kuwa sheria hiyo iliyotangazwa na Magufuli ilianza kutumika Oktoba Mosi na kupatiwa barua Oktoba 2, mwaka huu ya kueleza kwamba tozo hiyo imeondolewa jambo ambalo lilisababisha msongamano. Hata hivyo Waziri Mkuu, Mizengo Pinga aliumaliza mgogoro huo na kuruhusu wamiliki wa magari hayo kuendelea na safari zao kwa mwezi mmoja wakati jitihada nyingine zikiendelea.
Pinda alisema kutokana na sakata hilo, amelazimika kuunda kamati ambayo itakutana na wadau, Tatoa na Taboa ili kupata ufumbuzi wa mgogoro uliojitokeza. Athari zilizojitokeza ni pamoja na kusimama kwa upakuaji na upakiaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, kukwama kwa usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi na kukwamisha biashara na huduma za jamii kwa wananchi.
Kutokana na mvutano huo ni wazi kwamba usingekuwa na tija kwa Serikali wala Tatoa na Taboa, bali ungeleta maumivu makubwa kwa wananchi.
Pamoja na ushupavu wake Dk Magufuli katika kusimamia sheria, mimi naona wakati mwingine atumie pia busara, kwani wakati mwingine sheria pekee hazitatui matatizo.
Ni kweli kwamba Dk Magufuli anasimamia sheria halali, lakini ajue kwamba sheria hizo hutungwa na Bunge linalowawakilisha wananchi. Dk Magufuli akitoa tamko lake anasema wasafirishaji wengi nchini ni wanasiasa, kama wanaona kuondolewa kwa ofa ya uzito uliozidi wa asalimia tano wapeleke hoja bungeni ipitishwe rasmi.
Dk Magufuli akaendelea kusema kuwa, wanaogomea ni matajiri hivyo waende mahakamani.
Ubabe huu hauna tija yoyote, badala yake anashiriki kwa namna moja au nyingine kuhujumu uchumi wa nchi.
Nchi yetu inapaswa kuondoa vikwazo hivyo ili kuimarisha biashara za ndani na nje ya mipaka yake. Nchi yetu hii ina bandari ambayo inategemewa na nchi kama vile Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Anachotakiwa kufanya Dk Magufuli ni kuimarisha utengenezaji wa barabara kwa kuongeza kiwango cha ubora ili magari yachukue uzito mkubwa zaidi

Kwa upande mwingine, Serikali ichukue changamoto hii kama nafasi ya kufufua Mashirika ya Reli ya TRC na Tazara badala ya kuachia tu malori yasafirishe mizigo. Wakati sasa umefika mizigo isafirishwe kwa reli ili kuepuka msongamano wa magari, uharibifu wa barabara na kuharakisha mizigo inafika kwa wateja kwa wakati.
Kazi ya Waziri Mkuu Pinda isiwe kusubiri migogoro tu, bali aisimamie Serikali ifufue njia mbadala za usafiri. Ni aibu kwa nchi yetu yenye zaidi ya miaka 50 ya uhuru, inashindwa kuendesha mashirika ya usafirishaji kwa mfano shirika la reli na ndege ambayo yaliyoachwa na wakoloni.

Mfumo wa kupanga alama kidato cha 4 na 6 kubadilishwa

Ikiwa yamebaki majuma machache wanafunzi wa kidato cha nne waanze mtihani wa wa taifa, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iko kwenye mchakato wa kubadilisha mfumo wa upangaji za mitihani ya sekondari na matumizi wa alama za maendeleo ya mwanafunzi (Continuous Assessment (CA).
Mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwenye Mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka huu, unakuja ikiwa ni miezi michache tangu Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kufeli kwa maelfu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012.
Akizungumzia mchakato huo, Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa alisema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu na kuwa haina uhusiano na taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu ambayo mpaka sasa haijawekwa hadharani.
“Mambo yanakwenda yanabadilika hata binadamu yeyote anabadilika kila siku, mfumo unaotumika sasa hivi ni wa siku nyingi,” alisema.
Alisema kuwa, ili kuweza kuboresha vyema mfumo huo wameshirikisha wadau mbalimbali zikiwamo shule za sekondari.
“Kama unataka kuboresha lazima upate maoni, lengo letu ni kushirikisha shule zote za sekondari za Tanzania, ila siwezi kukuhakikishia kama zote zitashiriki kwa kuwa tunawatumia zaidi maofisa elimu mkoa na wilaya. Tumeweka pia dodoso kwenye mdandao ili watu zaidi washiriki.
Kuhusu tume ya Pinda hapa haihusiki kabisa, ile ilikuwa na mambo yake, hata bila ile tume sisi hii tungefanya tu,” alisema Profesa Bhalalusesa.
Alisema kuwa, mpaka sasa wameshapokea zaidi ya asilimia 60 ya maoni hayo kutokana na lengo walilo jiwekea.
Dodoso hilo ambalo pia Mwananchi imefanikiwa kuliona, linasema kuwa serikali inakusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita pamoja na matumizi ya ‘Alama Endelevu ya Mwanafunzi [Continuous Assessment (CA)].
“Serikali imeamua kukusanya maoni haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na kidato cha sita havifanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari.
Pia mfumo wa elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),” sehemu ya dodoso inasema.
Dodoso hilo linafafanua kuwa, muundo wa kwanza ni ule wa shule ambao alama mgando (Fixed Grade Ranges) ambao alama zinazotumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20.
Muundo wa pili ulioidhinishwa kutumiwa na Necta kuanzia mwaka 2012 ni Upangaji wa Alama Mgando usiobadilika (Fixed Grade Range).
Kwa kidato cha nne alama zilizotumika ni A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49 na F = 0 – 34.
Kwa upande wa kidato cha sita alama zilizotumika ni A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39.
Kwa mujibu wa dodoso hilo, alama zinazopendekezwa ni A = 81 – 100, B = 61 – 80, C = 41 – 60, D = 21 – 40 naF = 0 - 20.

Wasomi watoa tahadhari majadiliano ya JK, wapinzani

Dar es Salaam. Wasomi wameonyesha wasiwasi wao juu ya mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na vyama vya siasa vya upinzani vyenye wabunge, kuhusu tofauti zilizojitokeza katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Wasomi hao licha ya kuunga mkono mazungumzo, wamesema wanasiasa wana kawaida ya kuwa na agenda za siri jambo ambalo baadaye huzusha tena mzozo, huku wakirejea kwamba si mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kufanya mkutano wa aina hiyo.
Kauli hizo zimetokana na Rais Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya siasa; CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, TLP na UDP kukubaliana kuweka pembeni tofauti za kiitikadi na kutanguliza masilahi ya taifa katika mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Azavery Lwaitama alisema uamuzi wa Rais Kikwete ni mzuri lakini unaweza ukawa umechezwa kwa karata ya kisiasa.
Alifafanua, “Inaweza kuwa karata ya kisiasa kwa sababu bado Bunge lina wabunge wengi wa CCM, pia marekebisho yatasimamiwa na Waziri wa Katiba na Sheria, (Mathias Chikawe) sijui kutakuwa na jipya gani.”
Lwaitama alisema ili mambo yaende sawa, Rais Kikwete anatakiwa kuhakikisha kuwa marekebisho hayo yatakayofanywa nje ya Bunge, hayabadilishwi tena bungeni. “Ahakikishe kuwa wabunge wanapitisha tu yale ambayo yamerekebishwa nje ya Bunge.”
Naye Profesa Gaudence Mpangala wa UDSM alisema: “Tutajua kama hili jambo limetulia ama la, kama Bunge likipitisha mapendekezo mapya, kama ikiwa hivyo mambo yatakwenda vizuri.”
Hata hivyo, Profesa Mpangala alionyesha wasiwasi wake kama wabunge wataamua kuyapinga mabadiliko hayo, huku akishauri itumike njia ambayo itawafanya wabunge kukubaliana na kile kilichojadiliwa nje ya Bunge.
Alisema Katiba nzuri ni lazima itokane na mwafaka wa pamoja na kwamba nia ya Rais Kikwete inapaswa kuendelezwa hadi bungeni.
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Bashiru Ally alisema: “Siku zote mtu asiyejua anapokwenda hawezi kupotea njia, mchakato wa Katiba Mpya una mgongano wa mtazamo kuna maswali mengi kuhusu mchakato huu kuwa wa kisiasa na kisheria.
Alisema kuwa mchakato huo sasa haujulikani unaendeshwa kwa masilahi ya nani, kwa sababu kila malalamiko mengi yanayotolewa yamebebwa na vyama vya siasa.
“Tupo njiapanda, binafsi sina imani kubwa na mchakato huu, vyama vimeweka masilahi yao zaidi mbele,” alisema Bashiru.
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli na Mkuu wa wilaya, Lepilal Ole Moloimet alisema mtindo wa Rais Kikwete wa kuzungumza na wapinzani ni mzuri kwa sababu unasaidia kuweka mazingira ya utulivu na maelewano nchini.
Alisema utaratibu huo ni mzuri katika kuondoa manung’uniko, hasa kwa wale ambao hawaridhiki na hali halisi ya mambo yanavyokwenda nchini.
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema atakuwa kwenye mazingira mazuri ya kuchambua mpango wa Rais Kikwete kukutana na vyama vya upinzani, pindi mchakato ukikamilika.
“Bado ni mapema sana. Mazungumzo bado hayajamalizika. Tusubiri yamalizike ndipo nitakapokuwa na nafasi nzuri ya kuyazungumzia,” alisema Nape.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Ntatiro alisema kwamba wanatarajia kutoa taarifa kuhusu mazungumzo hayo na Rais Kikwete.
Alisema mpaka sasa chama hicho bado hakina uhakika kama kweli kilichoandikwa kwenye vyombo vya habari jana ndicho kilichoafikiwa kwenye mazungumzo hayo.
Kwa upande wake Chadema kupitia kwa Ofisa wake wa Habari, Tumaini Makene nao walisema watatoa taarifa yao baadaye.
Makubaliano ya mkutano
Taarifa ya Ikulu juzi, ilisema Rais Kikwete na viongozi hao walikubaliana vyama vyote vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha sheria hiyo, viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili itafutwe namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.
Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Wenyeviti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Chadema, Freeman Mbowe, NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.
Katika hoja zao, wapinzani wanataka kuangaliwa upya kwa idadi ya wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba, utaratibu wa
kupitisha Katiba Mpya kwenye Bunge Maalumu wakisisitiza kwamba kuwapo haki sawa kwa kila upande wa Muungano
Hoja nyingine ni ukomo wa Tume ya Mabaraza ya Katiba ambapo viongozi hao walipendekeza kwa rais kuwa tume iendelee kuwapo hadi Katiba Mpya itakapopatikana badala ya kuvunjwa mapema kabla ya Katiba Mpya.
Hoja nyingine kuingizwa kwa mambo ambayo hayakujadiliwa wala kupitishwa na Bunge kwenye muswada huo, wakitoa mfano wa
kifungu kipya kinachompa Katibu wa Bunge na yule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mamlaka ya kusimamia mchakato wa kumchagua mwenyekiti wa muda wa Bunge.
Walisema pendekezo hilo ni jipya na kwamba halikuwepo kwenye muswada uliotolewa maoni na wadau.

Kesi ya Pinda kuunguruma leo

Dar es Salaam. Kesi ya Kikatiba inayomkabili Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), inaanza kuunguruma leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo ilifunguliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS, wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kwa kauli aliyoitoa Bungeni kuhusu polisi kuwapiga raia wanaokaidi amri.
Walalamikaji hao wanadai kuwa kauli hiyo ni amri kwa vyombo vya dola kutekeleza sheria ya kuwapiga wananchi, wakati wa vurugu.
Hata hivyo Pinda na AG katika majibu yao, wamewasilisha pingamizi la awaliambalo pamoja na mambo mengine wanadai kuwa walalamikaji na watu waliorodheshwa katika kesi hiyo, hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
Pingamizi hilo limepangwa kusikilizwa leo na jopo la majaji linaloongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu.

Wednesday 16 October 2013

Zitto asimamisha ruzuku za mwezi kwa vyama vya siasa

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Pac),Zitto Kabwe amevilipua vyama vya siasa kwa uvunjaji wa sheria na kusimamisha ruzuku ya kila mwezi hadi vitakapowasilisha taarifa za ukaguzi wa fedha za umma tangu mwaka 2009 kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Pia kamati hiyo itawaweka kitimoto makatibu wakuu wa vyama vya siasa vinavyopata ruzuku ili wajieleze ni kwa nini hawajawasilisha taarifa hiyo hadi sasa.
Alisema hayo jana wakati kamati hiyo ilipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa katika Ofisi ndogo za Bunge.
Zitto alisema tangu mwaka 2009 vyama tisa vya siasa vinavyopewa ruzuku na Serikali vilipata jumla ya Sh67.7 bilioni lakini havijawahi kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa ruzuku kwa msajili kama vinavyopaswa kufanya hivyo kisheria.
“Ninaagiza msajili kuanzia sasa ruzuku isitolewe kwa chama chochote cha siasa hadi hapo kitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu tangu mwaka 2009 hadi sasa na makatibu wataitwa ili wajieleze kwa nini hawajafanya hivyo,” alisema.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alipoulizwa jana alisema: “Ninahitaji muda kuangalia kama kweli taarifa hiyo haijawasilishwa na sheria inasemaje kuhusu suala hilo,” alisema.
Alisema baada ya siku mbili za kazi atakuwa na majibu ya kuridhisha kuhusiana na suala hilo.
Viongozi wengine wa vyama vya siasa vinavyopata ruzuku, hawakupatikana kuelezea hali hiyo. Zitto aliongeza,“ Hivi ni vyama vya siasa ambavyo wakati ukifika vinaweza kuja kuongoza Serikali, lakini inashangaza ni kwa nini vinatumia fedha za walipakodi bila kukaguliwa, huu ni uvunjaji wa sheria.”
Kwa mujibu wa Zitto, vyama hivyo na fedha za ruzuku walizopata kwenye mabano tangu mwaka 2009 ni CCM (Sh50.9 bilioni), Chadema (Sh9.2 bilioni) na CUF (Sh 6 bilioni).
Vingine ni NCCR-Mageuzi(Sh677 milioni),UDP (Sh333 milioni), TLP (Sh217 milioni), APPT-Maendeleo (Sh217 milioni), DP (Sh3.3 milioni) na Chausta (Sh2.2 milioni).
Zitto alisema ingawa jukumu la ukaguzi wa fedha za umma ni la ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali lakini hakufanya hivyo kwa sababu ya ufinyu wa bajeti.
Alisema vyama vya siasa viliagizwa kufanya ukaguzi kwa kutumia kampuni binafsi kama vilivyokuwa vikifanya zamani hadi hapo ofisi ya CAG itakapopata fedha.
Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa msajili kuviagiza vyama vya siasa kutenga sehemu ya fedha za ruzuku kwa ajili ya ukaguzi.
Alisema viongozi hao waone kwamba suala la ukaguzi wa fedha za ruzuku ni muhimu ili kuleta uwazi katika matumizi ya fedha za umma.
“Sasa kamati imeshindwa kuendelea na kazi kwa sababu hakuna hesabu zilizokaguliwa, nendeni tutawaita siku nyingine,” alisema.
Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi alisema vyama hivyo vimekuwa vikidai kwamba havina ruzuku ya kufanya ukaguzi kwa kutumia kampuni binafsi.
“Kwa hiyo siwezi kuchukua fedha nikavipa vyama vya siasa kwaajili ya ukaguzi wakati hazijatengwa katika bajeti,” alisema.
Hata hivyo,Zitto alimwelekeza Mutungi kwamba fedha za ukaguzi ziko kwenye ruzuku wanazopewa na kwamba hiyo siyo sababu ya kuhalalishwa kutokaguliwa kwa hesabu zao.

Tuesday 15 October 2013

Kisumo: CCM inaweza kung’oka madarakani

Dar es Salaam. Mwanasiasa na kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Kisumo ameonya kuwa chama hicho kinaweza kuondolewa madarakani kutokana na kunyamazia vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma vinavyotokea nchini.
Mzee Kisumo alitoa onyo hilo wiki iliyopita katika mazungumzo maalumu aliyofanya na Mwananchi nyumbani kwake Dar es Salaam kuhusu kumbukumbu ya miaka 14 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere inayoadhimishwa leo.
Alisema tatizo kubwa la chama hicho ni kwamba kimemeendelea kuwa chama dola kikikaa mbali na wananchi, huku kikishindwa kuidhibiti rushwa na kuwajibisha wahusika wa vitendo hivyo.
“Chama kimebaki kuwa cha walalamikaji, kila mtu amekuwa mlalamikaji. Hata Waziri Mkuu amegeuka mlalamikaji. Sijaona watu wanaowajibishwa kwa ufisadi,” alisema Kisumo na kuongeza:
“CCM haiwezi kujivunia ufisadi unaoonekana nchini. Siwezi kusema imeukumbatia, lakini nasema imekuwa CCM bubu, hata kuukemea ufisadi haiwezi. Utamaduni huu enzi za Mwalimu Nyerere haukuwapo.”
Alisema kutokana na udhaifu huo wa CCM, kuna uwezekano mkubwa wa chama cha upinzani, na hasa Chadema kutumia mwanya huo kuwashawishi wananchi na kushinda uchaguzi.
Kisumo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa CCM, alisema ingawa Chadema haijaonyesha wazi mambo kinayoyapigania, kinaweza kutumia agenda ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma kuwavutia wananchi na kuchaguliwa.
Alitoa mfano wa tuhuma za baadhi ya viongozi wa Serikali kuficha mabilioni ya shilingi kwenye benki za Uswisi, kuwa zinaweza kuwa kete muhimu ya kuwaingiza Chadema madarakani, iwapo Serikali ya sasa haitawashughulikia wahusika.
“Wakijitokeza na kuwataja majina wahusika, wakasema fulani na fulani ndiyo wenye mabilioni haya Uswisi, na Serikali ikasita kuwachukilia hatua, wakasema tukiingia madarakani tutawakamata, wananchi wanaweza kuwaamini na kuwachagua,” alisema na kuongeza: “Wakishinda uchaguzi hata kwa viti vichache tu, watakosa nguvu bungeni, lakini kwa wananchi watakuwa na nguvu sana.
Hii inaweza kuwasaidia kwa miaka mitano ya kwanza. Wanaweza kupata ushindi mkubwa zaidi kwa mara ya pili na wakiingia madarakani watawafunga viongozi wa zamani kweli.”
Mzee Kisumo anasistiza, “Hili linawezekana. Anayesema uwezekano wa CCM kushindwa haupo, anajikana mwenyewe. CCM inabidi ijihami na majibu ya jinsi inavyotumia rasilimali za nchi.”
Alionya kuwa si vizuri kuishia kujinadi kwa mambo mengi mazuri iliyofanya huko nyuma, akitolea mfano kuwa hiyo ni sawa na nguo nyeupe ambao ikiingia doa moja tu inakuwa haitamaniki tena.

“Sisemi kwamba hawajafanya kitu, yapo mengi mazuri waliyoyafanya, lakini ufisadi ni sawa na doa kwenye shati jeupe ambalo huwa linaonekana kuliko weupe na ung’avu wa shati hilo,”alisema Kisumo.
Alisema katika siku za karibuni ufisadi umekuwa jambo la kawaida, hadi umegeuzwa kuwa wa kitaasisi, ambapo aligusia hata Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ulioanzishwa na Bunge kuwa ni sehemu ya ufisadi.
Alihoji iweje fedha za umma zitumike kumsadia mtu mmoja kujiimarisha kisiasa, akisema hiyo ni ‘Built in Corruption’.
Mzee Kisumo pia alizungumzia mvutano ambao umekuwa ukijitokeza kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwamba msingi wa mvutano huo ni kuwapo tabaka la wahalifu wasioweza kuguswa na sheria.
“Unapokuwa na mvutano huo una maana mbili, kwanza ni hali kwamba huyo mmoja anajua sabababu za watuhumiwa kutochukuliwa hatua, lakini pili ni kwamba huenda tuna watu wawili katika nafasi hizi, lakini wana nia mbili tofauti,”alisema Kisumo na kuongeza:
“Ni hatari sana unapokuwa na mfumo kwenye nchi ambao unawalinda baadhi ya wahalifu, unakuwa na wahalifu wanaoguswa na wengine hawaguswi, watu wanasubiri pengine itokee siku waone mtu wasiyemtarajia anafikishwa mahakamani na hapo watajua kwamba kweli nchi imeamua kupambana na rushwa na ufisadi.”
…Aonya Zanzibar
Mzee Kisumo pia alizungumzia mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya na kwamba mvutano kuhusu muundo wa Muungano ni matokeo ya upande wa Zanzibar kuachiwa kufanya vitendo vingi vinavyoashiria kutafuta uhuru kamili kama nchi nje ya Muungano huo.
Vitendo hivyo kwa mujibu wa kada huyo ni mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalitamka kuwa Zanzibar ni nchi, kurejesha bendera yake, wimbo wake wa taifa na mambo mengine.
“Katika hatua sasa Zanzibar wanajiona kwamba wamekaribia kutimiza azma yao, kuelekea katika ‘uhuru’ kamili, nasema whoever (yeyote) aliyefumbia macho vitendo hivi akiwa Rais, alifanya makosa makubwa,”alisema Mzee Kisumo na kuongeza:
“Ukitafakari hali hiyo, kama tukiwa na mfumo wa Serikali Tatu, ni kitu gani kitawazuia Tanganyika nao wasidai kuwa na Katiba sawa na ile ya upande wa pili? Ikifika hapo mimi sioni Muungano kuwapo.”
Hata hivyo, alionya kuwa masuala yote yanayohusu Muungano ikiwa ni pamoja na lile la mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar, yanapaswa kufanyiwa uamuzi wa busara kwani historia inaonyesha kuwa kuvunja Muungano wowote ule lazima damu imwagike.

“Muungano wa States (nchi) za Marekani uligharimu umwagaji damu, United Kingdom (Uingereza) pia damu ilimwagika, kwa hiyo lazima tujifunze kwamba ikiwa tutafikia hatua ya kuvunja Muungano wetu, hatuwezi kupita salama katika hili,” alisema.
Alisema kinachotokea sasa kuhusu Zanzibar kuwa na mwelekeo wa kujitenga, ilianza katika chaguzi zilizopita, pale ambapo Mzanzibari aliyekaa nje ya visiwa hivyo kwa zaidi ya miaka mitano anakosa haki ya kupiga kura kwa kukosa sifa ya ukaazi.
“Hili nalo ni tatizo kubwa, Mzanzibari ambaye ameamua kuishi Moshi, Morogoro au kwingineko nchini uhalali wake wa kuwa Mzanzibari unawekwa shakani, kwani hawezi kupiga kura kama hajaishi Zanzibar mfululizo kwa kipindi hicho,” alisema Mzee Kisumo na kuongeza:
“Ukiangalia kwa Mtanzania wa Bara, hakutani na kadhia hii, yeye ataishi popote hata kama nje ya nchi kwa muda wowote, lakini akirudi nyumbani haambiwi eti si mkaazi, kama ni Tabora atakwenda kwao au Mbeya”.
Mzee Kisumo alisema kutokana na hali hiyo kuna kundi kubwa la Wazanzibari ambalo linajikuta katika hatari ya kukosa haki zao na kwamba ikiwa kutakuwa na mfumo wa Serikali Tatu na upande wa Tanzania Bara kuanzisha utaratibu kama wa Zanzibar, watajikuta kwenye utata wa uraia wao.
“Tukiwa na Tanzania moja iliyoungana, ambayo watu wake hawana mwelekeo wa kuangalia masilahi yao zaidi, haya mambo hayawezi kutokea. Kimsingi mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania anapaswa kujivunia uraia wake kama Mtanzania na hapaswi kuishi kwa vikwazo vya aina hii,”alisema Kisumo na kuongeza:
“Kwa hiyo mimi nasema haya mambo lazima… Lazima tuyatizame kwa upana wake….Maana hawa watu wapo wanaathirika, sihitaji kutaja majina ya watu hapa, lakini wapo, wanafahamika na wengine ni wafanyabiashara wakubwa sana nchini, wametoka Zanzibar na wameishi Tanzania Bara kwa miaka mingi.”
Kisumo alionekana kukerwa zaidi na pendekezo la kuwapo kwa Serikali ya mkataba na kusisitiza kuwa wanaotoa mawazo ya aina hiyo wanakusudia kuvunja Muungano kwa masilahi yao binafsi.
... Asema Nyerere alijaa katika mioyo ya Watanzania
Wakati taifa leo linatimiza miaka 14 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Kisumo anasema kuwa kiongozi hiyo alikuwa na sifa nyingi ambazo zilimfanya kujaa mioyoni mwa wa Watanzania.
Akizungumzia sifa za Nyerere kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika iliyokuja kuwa Tanzania baadaye , Kisumo anaeleza kiongozi huyo alikuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake na Bara la Afrika kwa jumla.
Kisumo, ambaye alifanya kazi na kiongozi huyo kabla na baada ya uhuru, alisema sifa nyingine ya Mwalimu Nyerere ilikuwa uwezo wake wa kushawishi na kuongoza.

“Nyerere pia aliamini katika umoja wa taifa na uongozi wa pamoja na ndio maana alifanikiwa katika nyanja nyingi,” anasimulia Kisumo, ambaye alianza siasa kupitia kwenye vyama vya wafanyakazi akiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Rashid Kawawa na Marehemu Michael Kamaliza katika miaka ya 1950.
Kisumo anasema bila ya kificho kuwa marais waliomfuatia Nyerere wameshindwa kufikia sifa ya Mwalimu hasa linapokuja suala zima la sifa za uongozi.
Alitoa mfano kitendo cha Nyerere kwa kutumia lugha ya Kiswahili na kuunganisha watu wa Tanganyika kupigania uhuru bila ya kumwaga damu kutoka kwa Waingereza.
“Alipigania uhuru bila ya kuwa na jeshi au silaha unaweza mwenyewe ukamfikiria mwenyewe Mwalimu alikuwa ni kiongozi wa aina gani?
“Nyerere aliunganisha machifu waliokuwa na nguvu sana katika kipindi kile ingawa alipingwa na baadhi yao kama Chifu Thomas Marealle wa Moshi.
“Huyu Chifu Marealle alikwenda mbali zaidi na hata kwenda kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani na kueleza kuwa Tanganyika haikuwa tayari kujitawala, lakini alishindwa kwa hoja za Mwalimu,” aliongeza Kisumo, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali wakati wa uongozi wa Nyerere zikiwamo za Uwaziri na Ukuu wa Mkoa.
Kisumo anaeleza kuwa Mwalimu aliwazidi kete Waingereza kwani alipenya katika asasi mbalimbali za Watanganyika.
“Mwalimu alitumia michezo kudai uhuru, alikuwa karibu sana na klabu ya Yanga pia hata vikundi vya muziki wa dansi na taarabu,” aliongeza Kisumo.
Kisumo anasimulia kuwa baada ya Tanganyika kupata uhuru bado Nyerere alisaidia mataifa mengine katika harakati zao za kupigania uhuru wao na alitaka Umoja wa Afrika na ndio maana akaasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Ukombozi wa Afrika
Alisema Nyerere alikubali Kamati ya Ukombozi ya iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) iweke makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
“Kilikuwa kitendo cha hatari kwani mataifa mengi wakati ule hayakukubali kupokea wapigania uhuru kwa kuhofia usalama wa nchi zao.

“Vyama mbalimbali kutoka nchi za Afrika Kusini, Angola, Msumbiji na Namibia vilileta watu wao kwa mafunzo ya kijeshi, jambo ambalo lilitutisha wakati ule,” anaongeza Kisumo.
Kisumo alisimulia kuwa Nyerere alisimamia umoja na ukombozi wa Bara la Afrika na kumfanya ajizolee sifa sawa na marais wengine kama Gamal Abdel Nasser wa Misri, Ben Bella wa Algeria na Kwame Nkrumah wa Ghana.
Kisumo alisema kuwa Mwalimu hakuishia kuunga mkono wapigania uhuru wa Afrika pia aliunga mkono harakati za Wapalestina kujikomboa kutoka kwa Israel, ambayo katika miaka ya mwanzo wa Uhuru ilikuwa kati ya wafadhili wakubwa wa Tanzania.
“Nakumbuka Kiongozi wa Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Yasser Arafat alialikwa katika moja ya mikutano ya chama cha TANU iliyofanyika jijini Dar es Salaam,” anaongeza Kisumo.
Sera za uchumi
Kisumo anasema kuwa Nyerere alikuwa anaamini kuwa Tanzania itaendelea kiuchumi kama itawekeza vya kutosha katika kilimo.
“Ndio maana katika miaka ya mwanzo baada ya uhuru tulikuwa na sera ya `Siasa ni Kilimo’ na baadaye `Kilimo cha Kufa na Kupona’,” alisema Kisumo.
Kisumo alisema kuwa baada ya kampeni ya kilimo, Nyerere aliona umuhimu wa kujenga viwanda ili kutumia malighafi iliyotoka katika kilimo.
“Ndio maana ukaona tukajenga viwanda vya nguo katika Miji ya Dar es Salaam, Arusha, Musoma na Mwanza pia kiwanda cha nyuzi pale Tabora,” alisema.
Pia Kisumo alisema kuwa Mwalimu aliweka mkazo katika elimu ya kujitegemea ili kumwandaa kijana wa Kitanzania.
“Hivi majuzi nilisikitika sana baada ya kusikia ikiwa shule moja huko Kigoma imepokea msaada wa vyoo vya shimo kutoka kwa Wachina! Hivi kweli imefika mahali wanafunzi wetu wanashindwa kuchimba vyoo?” alihoji Kisumo kwa masikitiko.
Kisumo alisema kuwa mambo yalibadilika katika miaka ya 1990 wakati Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margareth Thatcher alipoanzisha sera za ubinafsishaji na utandawazi.
“Hapo ndio yakabadilika ambapo mataifa makubwa yakazidi kuzikandamizia nchi changa kupitia misaada ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF),” alisema Kisumo.
Kisumo alisema Mwalimu alipambana na mataifa hayo makubwa na kutaka kuacha kukandamiza nchi changa. Alipambana na mataifa kupitia Tume ya Kusini 1986, taasisi ambayo ilitokana na uliokuwa Umoja wa Nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM).

Zitto sasa aanika mshahara wa Rais

Igunga. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe amesema sababu ya kutaja mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
Zitto alitoa kauli hiyo jana mjini Igunga, wakati akitangaza mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Zitto, kwa mwaka kiongozi huyo wa nchi analipwa Sh384 milioni ambazo ni wastani wa Sh32 milioni kwa mwezi bila kukatwa kodi.
Hatua ya Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), kutaja mshahara wa rais inakuja wiki moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri mkuu kuwa ni Sh26 milioni kwa mwezi pasipo kukatwa kodi
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanancholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho. Alisemaha ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa Sh200,000 kwa mwezi ukikatwa kodi huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi.
Alisema katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara na malipo mengine huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupu rupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk Slaa akiwa Rais na akataka kupunguza mshahara wake kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka Serikalini,” alisema Zitto.
Zitto alisema kuwa kitendo cha Serikali kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania, hakikuzingatiwa kulingana na uwazi uliowekwa kwa kuandika uwazi wa viwango vya mishahara.
Alisema kuwa waziri aliyehusika kufunguia magazeti hayo hakufikiria kwa makini kutokana na kuwa na uelewa mdogo na kuongeza kuwa hakuna kosa lolote linalopelekea kufungiwa magazeti hayo kutokana na ukweli ulioandikwa

Kikwete: Tumeshinda maadui zetu

Dar/Iringa. Rais Jakaya Kikwete amesema maadui wote ambao walitaka kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi wamedhibitiwa .
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui wote wanaohusika na kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria. “Kulikuwapo na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda adui,” alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema katika siku za hivi karibuni, maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na mkakati wa kuvuruga amani ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola vimewadhibiti na nchi iko salama.
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani kwa sababu inajua wazi kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano utavurugika na shughuli za maendeleo zitasimama.
Katiba Mpya
Rais Kikwete alisema mwaka 2014 ni mwaka wa kipekee kwa nchi kwa kuwa utakuwa na mambo makubwa matatu yatakayofanywa.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba Katiba Mpya ni lazima ikamilike mwakani kama mambo yatakwenda kama ilivyopangwa.
Vilevile, alisema mwakani Tanzania itasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoondoa udhalimu na kuwarudishia Wazanzibari heshima ya mwanadamu na utu wake.
“Pia tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wetu. Nawaomba Watanzania wajiandae kuyafanikisha vizuri mambo hayo ili historia mpya ifunguliwe nchini.
“Wazanzibari waanze miaka mingine baada ya miaka hamsini ya uhuru wao, muungano uanze miaka mingine baada ya miaka hamsini na Katiba Mpya itupeleke miaka mingine tukiwa wamoja,” alisema Kikwete.
Rais Kikwete alionya kuwa asingependa mchakato wa kupata Katiba Mpya uligawe taifa na kuleta mfarakano utakaovunja umoja wa kitaifa badala ya kuuimarisha.
“Tunataka tuwe na Katiba itakayojenga, siyo kubomoa, kutugawa kwa misingi ya kiitikadi,” alionya Rais Kikwete.

Alisema kuwa kaulimbiu ya maadhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa kwa mwaka huu ni kusisitiza mshikamano wa kitaifa unaopinga mbinu zozote za kuligawa taifa. “Kaulimbiu ya mwaka huu; Tanzania ni wamoja, tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi au rasilimali,” alisema Rais Kikwete.
Alisisitiza kuwa amekusudia mabadiliko ya Katiba ambayo mchakato wake unaendelea yawe ya kulipeleka mbele taifa kimaendeleo kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema atapendelea kuona Katiba Mpya inazinduliwa Aprili 13, mwakani, siku ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Baba wa Taifa.
Alisema kitendo hicho kitaienzi zaidi siku hiyo na kuandamana na mpango wa kubadilisha maadhimisho ya kitaifa ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere kutoka Oktoba 14 siku aliyofariki na kuwa Aprili 13, siku aliyozaliwa.
..ataka kuvuruga Mwenge
Maadhimisho ya Mwenge nusura yaingie dosari baada ya mwanamume kujichomeka katika kundi la wanahabari akiwa na lengo la kumdhuru kiongozi wa Mbio za Mwenge.
Kitendo hicho kilifanyika wakati Rais Kikwete akiwa tayari ameshuka chini katika jukwaa dogo akisubiri kukabidhiwa mwenge huo, mtu huyo alichomoka kutoka katika kundi la waandishi wa habari na kujaribu kumvamia kiongozi wa Mbio za Mwenge, Juma Ali Sima aliyekuwa ameshikilia Mwenge huo.
Hata hivyo, jitihada za mtu huyo za kutaka kumvamia kiongozi wa Mwenge zilikwama baada ya kudhibitiwa vikali na askari waliokuwa wakilinda amani uwanjani hapo.
Katika kipindi hicho, Rais Kikwete pamoja na wasaidizi wake wengine walikuwa mita kama tisa kutoka katika eneo la tukio akisubiri kukabidhiwa Mwenge huo.
Rais Kikwete alisema kilele cha maadhimisho ya Mbio za Mwenge kimefanywa kuwa pia siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tangu afariki miaka 14 iliyopita.
Alisema Watanzania wote bila kujali vyama vyao wana wajibu wa kuyakumbuka mema yote ya Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni pamoja na mafundisho yake.
Rais pia alisema ili kumkumbuka zaidi Mwalimu Nyerere alipendekeza siku yake ya kuzaliwa ndiyo iitwe Nyerere Day na ianze kusherehekewa kwa mbwembwe, iwe na mijadala ya kazi zake na itumiwe kufanya shughuli mbalimbali za kujenga taifa kwa lengo la kumuenzi.
Kuhusu dawa za kulevya
Katika maadhimisho hayo, Rais Kikwete alizungumzia mkakati wa Serikali yake wa kupambana na dawa za kulevya kwamba kitaanzishwa chombo maalumu kwa ajili ya kazi hiyo.
Alisema kazi ya kupambana na dawa za kulevya ni ngumu na hatari kutokana na wanaofanya kazi hiyo kuwa na fedha nyingi, lakini Serikali itawalinda wote

Friday 11 October 2013

Museveni, Dk Besigye wakutana ana kwa ana

Kampala. Wapinzani wawili wa kisiasa, Rais Yoweri Museveni na mpinzani wake mkuu, Dk Kizza Besigye wamekutana ana kwa ana kwenye sherehe za Uhuru huko Rukungiri, siku moja baada ya Rais Museveni kumrushia vijembe Besigye.
Wawili hao wanakutana baada ya Museveni kumtaka Besigye na Meya wa Jiji la Kampala, Erias Lukwago kuacha kuchochea machafuko kwenye mji huo kwa nia ya kutaka kuiingiza nchi hiyo kwenye vurugu kama ilivyo Misri kwa sasa.
Pia aliwataka kuacha kuingia katika mapambano ambayo hayana faida kwao kwa kuwa mara zote wamekuwa wakishindwa hivyo ni vyema wakirejea kwenye chama tawala, ambako watapokelewa kwa heshima.
Maoni hayo yaliibua mvutano wa maeneo kutoka kwa Dk Besigye ambaye amewahi kuwa daktari wa Museveni ambapo alikaririwa na gazeti la Daily Monitor akihoji “Niombe samahani kwa lipi? Yeye amejifanya kuwa jaji na hilo ndilo tunapambania,” alisema.
Katika maadhimisho ya leo, dhima kuu ni ‘Kuimarisha fursa za uwekezaji’ ambapo Rais Museveni ndiye mgeni rasmi na Dk Besigye akihudhuria kwa mwaliko rasmi wa Ikulu.

Tanzania, Burundi zashikilia msimamo EAC



 Kenya, Uganda na Rwanda wachafua hali ya hewa

HALI ya mambo imezidi kuwa tete katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya Tanzania na Burundi kutaka maelezo ya kina kutoka kwa nchi nyingine tatu wanachama za Kenya, Uganda na Rwanda zilizoanzisha ushirikiano mpya kinyemela kati yao, kwa kuzitenga nchi hizo mbili.Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria kuwa Tanzania na Burundi zimetengwa na nchi hizo tatu ambazo zimeanzisha ushirikiano mpya kati yao kinyemela, kinyume cha mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo mwaka  1999.Jumuiya ya sasa ilizaliwa tena upya Novemba 30, mwaka 1999 ikishirikisha nchi za Tanzania, Uganda na Kenya, wakati Rwanda na Burundi zilikaribishwa baadaye mwaka 2008.Jumuiya hiyo mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).Habari za hivi karibuni zilizopatikana kutoka ndani ya EAC zinabainisha kwamba Tanzania na Burundi zimekerwa na hatua ya nchi wanachama wenzao za Kenya, Uganda na Rwanda kuanza mchakato wa kuanzisha shirikisho la kisiasa bila ya kuzishirikisha nchi hizo.Tanzania na Burundi zinaelezwa kuwa kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Agosti 31, mwaka huu, mjini Arusha zilimtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Shem Bageine, kutoka Uganda kutoa maelezo ya kina kuhusu hatua za nchi hizo tatu kufanya mambo ambayo yanakwenda kinyume cha mkataba wa Jumuiya hiyo.Taarifa zinaeleza kuwa hata hivyo Bageine hakuwa na majibu muafaka kuhusu hatua hiyo na ndipo nchi hizo mbili zilipoazimia kuhitaji majibu ya kina zaidi kuhusu suala hilo katika kikao kijacho kitakachofanyika Novemba, mwaka huu.Pamoja na suala la kuanzisha mchakato wa shirikisho la kisiasa, nchi hizo tatu pia zinaelezwa kukubaliana kuanzisha ushirikiano katika eneo la kukusanya kodi  (single costumes territory).Masuala mengine ambayo yanaelezwa kutozifurahisha nchi za Tanzania na Burundi ni hatua yao ya kukubaliana kuwa na visa moja kwa watalii watakaotembelea nchi hizo, kuimarisha miundombinu hasa ujenzi wa reli kutoka Bandari ya Mombasa-Kenya hadi Kigali Rwanda kupitia Kampala-Uganda.Moja wa maofisa wa EAC ambaye ni Mtanzania (jina linahifadhiwa) alilimbia gazeti hili la Raia Mwema kuwa hali ndani ya sekretarieti ya jumuiya hiyo ni mbaya na hata watumishi kutoka nchi za Tanzania na Burundi wameanza kutengwa na wenzao.“Kumekuwa na kutokuaminiana miongoni mwa maofisa wa juu katika jumuiya yetu, watumishi wa Tanzania ni kama tunatengwa na wenzetu,” alidai mtumishi huyo bila ya kufafanua zaidi.Katika mkutano wake na waandishi wa habari mwezi uliopita Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya EAC, Dk. Richard Sezibera, alikanusha madai kuwa hali si shwari ndani ya Jumuiya anayoiongoza.Dk. Sezibera alikaririwa akisema: “Hali ni shwari katika jumuiya na kila kitu kinakwenda vizuri kulingana na mkataba wa jumuiya tofauti zinazojitokeza ni za kawaida katika jumuiya yoyote ile ya watu kutofautiana mawazo.”!Taarifa zinaeleza kuwa katika utetezi wake, Bagaine ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki nchini Uganda, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kuwa mikutano iliyowakutanisha viongozi wakuu wa nchi hizo tatu iliratibiwa na wizara za mambo nje katika nchi husika.Waziri huyo alieleza kuwa kwa kawaida mikutano inayohusiana na masuala ya Afrika Mashariki huratibiwa na wizara husika katika kila nchi, lakini kwa suala hilo ilikuwa kinyume hivyo asingekuwa na majibu muafaka.“Kutokana na mgongano uliojitokeza ujumbe wa Tanzania ulitaka upewe maelezo yanayotosheleza katika kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri kinachotarajiwa kufanyika mapema Novemba, mwaka huu, kabla ya kikao cha wakuu wa nchi ambao watakutana Novemba 30,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.Akizungumzia mzozo huo aliyekuwa Waziri wa kivuli wa Afrika Mashariki kutoka Kambi Upinzani Bungeni- CHADEMA, Mustafa Akonaay, alisema ilikuwa mapema kwa nchi wanachama waanzilishi wa jumuiya kuziruhusu Rwanda na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo.“Hizi nchi mbili zilikuwa na matatizo ya ndani ya kiutawala baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu, hivyo ilikuwa ni mapema sana kuziruhusu kujiunga na jumuiya wakati bado zina matatizo ya ndani,” alieleza Akonaay.Naye mwanzuoni maarufu katika diplomasia, Profesa Abdallah Safari, anasema katika msuguano huo kuna taarifa za muda mrefu kuwa baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wanataka kuharakisha shirikisho la kisiasa kwa maslahi yao wenyewe.“Tetesi kuhusu suala hilo ni za muda mrefu na kulikuwa na mipango ya kupanua kitu kinachoitwa dola ya Wahima (Hima Empire) katika eneo la Maziwa Makuu hadi Tanzania, kuna uwezekano mipango hiyo bado iko vichwani mwa viongozi hao,” anasema Profesa Safari.Anaongeza kusema; “Wakati mwingine sisi Watanzania ni chanzo cha kuanza kutengwa na wenzetu kutokana na kushamiri kwa tabia ya urasimu, uzembe na wizi katika sekta mbalimbali za umma na hata kushindwa kwenda sambamba na wenzetu ambao wanadhamira ya kufanya mambo kwa weledi zaidi.”!Akitoa mfano Profesa huyo anasema katika sekta ya biashara Tanzania imeshindwa kuondoa urasimu katika Bandari ya Dar es Salaam kiasi cha wafanyabiashara kutoka nchi jirani wanaoitumia kusafirisha bidhaa zao kupata hasara.
“Mlolongo  huo wa mambo yasiyo na msingi unasababisha usumbufu kwa wafanyabiashara wengi wanaopitisha bidhaa zao katika ardhi ya Tanzania na bidhaa hizo hupanda bei marudufu katika masoko zinakopelekwa na hivyo kuongeza gharama kwa watumiaji,”!Katika hatua nyingine, alidai hatua ya Tanzania kuanza kutengwa inatokana na uongozi dhaifu wa serikali.“Hili la Rais kusafiri sana nalo ni tatizo na wenzetu wameona sisi kama Taifa hatuko makini  na wametumia mwanya huo kutaka kujitenga, kama kuna uongozi imara wasingethubutu kuanza kufanya mambo kama hayo kwa mlango wa nyuma,” anasema Profesa Safari.Hata hivyo, kwa mujibu wa Profesa Safari, ni vigumu kwa shirikisho hilo la kisiasa kufanikiwa haraka kutokana na changamoto kadhaa ikiwamo nchi husika kuwa na matatizo ya ndani, hasa ya kidemokrasia ambayo yalitakiwa kupatiwa ufumbuzi kwanza.
  • Kenya, Uganda na Rwanda wachafua hali ya hewa
HALI ya mambo imezidi kuwa tete katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya Tanzania na Burundi kutaka maelezo ya kina kutoka kwa nchi nyingine tatu wanachama za Kenya, Uganda na Rwanda zilizoanzisha ushirikiano mpya kinyemela kati yao, kwa kuzitenga nchi hizo mbili.
Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria kuwa Tanzania na Burundi zimetengwa na nchi hizo tatu ambazo zimeanzisha ushirikiano mpya kati yao kinyemela, kinyume cha mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo mwaka  1999.
Jumuiya ya sasa ilizaliwa tena upya Novemba 30, mwaka 1999 ikishirikisha nchi za Tanzania, Uganda na Kenya, wakati Rwanda na Burundi zilikaribishwa baadaye mwaka 2008.
Jumuiya hiyo mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).
Habari za hivi karibuni zilizopatikana kutoka ndani ya EAC zinabainisha kwamba Tanzania na Burundi zimekerwa na hatua ya nchi wanachama wenzao za Kenya, Uganda na Rwanda kuanza mchakato wa kuanzisha shirikisho la kisiasa bila ya kuzishirikisha nchi hizo.
Tanzania na Burundi zinaelezwa kuwa kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Agosti 31, mwaka huu, mjini Arusha zilimtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Shem Bageine, kutoka Uganda kutoa maelezo ya kina kuhusu hatua za nchi hizo tatu kufanya mambo ambayo yanakwenda kinyume cha mkataba wa Jumuiya hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa hata hivyo Bageine hakuwa na majibu muafaka kuhusu hatua hiyo na ndipo nchi hizo mbili zilipoazimia kuhitaji majibu ya kina zaidi kuhusu suala hilo katika kikao kijacho kitakachofanyika Novemba, mwaka huu.
Pamoja na suala la kuanzisha mchakato wa shirikisho la kisiasa, nchi hizo tatu pia zinaelezwa kukubaliana kuanzisha ushirikiano katika eneo la kukusanya kodi  (single costumes territory).
Masuala mengine ambayo yanaelezwa kutozifurahisha nchi za Tanzania na Burundi ni hatua yao ya kukubaliana kuwa na visa moja kwa watalii watakaotembelea nchi hizo, kuimarisha miundombinu hasa ujenzi wa reli kutoka Bandari ya Mombasa-Kenya hadi Kigali Rwanda kupitia Kampala-Uganda.
Moja wa maofisa wa EAC ambaye ni Mtanzania (jina linahifadhiwa) alilimbia gazeti hili la Raia Mwema kuwa hali ndani ya sekretarieti ya jumuiya hiyo ni mbaya na hata watumishi kutoka nchi za Tanzania na Burundi wameanza kutengwa na wenzao.
“Kumekuwa na kutokuaminiana miongoni mwa maofisa wa juu katika jumuiya yetu, watumishi wa Tanzania ni kama tunatengwa na wenzetu,” alidai mtumishi huyo bila ya kufafanua zaidi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mwezi uliopita Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya EAC, Dk. Richard Sezibera, alikanusha madai kuwa hali si shwari ndani ya Jumuiya anayoiongoza.
 Dk. Sezibera alikaririwa akisema: “Hali ni shwari katika jumuiya na kila kitu kinakwenda vizuri kulingana na mkataba wa jumuiya tofauti zinazojitokeza ni za kawaida katika jumuiya yoyote ile ya watu kutofautiana mawazo.”!
Taarifa zinaeleza kuwa katika utetezi wake, Bagaine ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki nchini Uganda, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kuwa mikutano iliyowakutanisha viongozi wakuu wa nchi hizo tatu iliratibiwa na wizara za mambo nje katika nchi husika.
Waziri huyo alieleza kuwa kwa kawaida mikutano inayohusiana na masuala ya Afrika Mashariki huratibiwa na wizara husika katika kila nchi, lakini kwa suala hilo ilikuwa kinyume hivyo asingekuwa na majibu muafaka.
“Kutokana na mgongano uliojitokeza ujumbe wa Tanzania ulitaka upewe maelezo yanayotosheleza katika kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri kinachotarajiwa kufanyika mapema Novemba, mwaka huu, kabla ya kikao cha wakuu wa nchi ambao watakutana Novemba 30,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.
Akizungumzia mzozo huo aliyekuwa Waziri wa kivuli wa Afrika Mashariki kutoka Kambi Upinzani Bungeni- CHADEMA, Mustafa Akonaay, alisema ilikuwa mapema kwa nchi wanachama waanzilishi wa jumuiya kuziruhusu Rwanda na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo.
“Hizi nchi mbili zilikuwa na matatizo ya ndani ya kiutawala baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu, hivyo ilikuwa ni mapema sana kuziruhusu kujiunga na jumuiya wakati bado zina matatizo ya ndani,” alieleza Akonaay.
Naye mwanzuoni maarufu katika diplomasia, Profesa Abdallah Safari, anasema katika msuguano huo kuna taarifa za muda mrefu kuwa baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wanataka kuharakisha shirikisho la kisiasa kwa maslahi yao wenyewe.
“Tetesi kuhusu suala hilo ni za muda mrefu na kulikuwa na mipango ya kupanua kitu kinachoitwa dola ya Wahima (Hima Empire) katika eneo la Maziwa Makuu hadi Tanzania, kuna uwezekano mipango hiyo bado iko vichwani mwa viongozi hao,” anasema Profesa Safari.
Anaongeza kusema; “Wakati mwingine sisi Watanzania ni chanzo cha kuanza kutengwa na wenzetu kutokana na kushamiri kwa tabia ya urasimu, uzembe na wizi katika sekta mbalimbali za umma na hata kushindwa kwenda sambamba na wenzetu ambao wanadhamira ya kufanya mambo kwa weledi zaidi.”!
Akitoa mfano Profesa huyo anasema katika sekta ya biashara Tanzania imeshindwa kuondoa urasimu katika Bandari ya Dar es Salaam kiasi cha wafanyabiashara kutoka nchi jirani wanaoitumia kusafirisha bidhaa zao kupata hasara.
“Mlolongo  huo wa mambo yasiyo na msingi unasababisha usumbufu kwa wafanyabiashara wengi wanaopitisha bidhaa zao katika ardhi ya Tanzania na bidhaa hizo hupanda bei marudufu katika masoko zinakopelekwa na hivyo kuongeza gharama kwa watumiaji,”!
Katika hatua nyingine, alidai hatua ya Tanzania kuanza kutengwa inatokana na uongozi dhaifu wa serikali.
“Hili la Rais kusafiri sana nalo ni tatizo na wenzetu wameona sisi kama Taifa hatuko makini  na wametumia mwanya huo kutaka kujitenga, kama kuna uongozi imara wasingethubutu kuanza kufanya mambo kama hayo kwa mlango wa nyuma,” anasema Profesa Safari.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Profesa Safari, ni vigumu kwa shirikisho hilo la kisiasa kufanikiwa haraka kutokana na changamoto kadhaa ikiwamo nchi husika kuwa na matatizo ya ndani, hasa ya kidemokrasia ambayo yalitakiwa kupatiwa ufumbuzi kwanza.

Soma zaidi kuhusu:

Tufuatilie mtandaoni:

Maoni ya Wasomaji

Historia hujirudia. Chonde yasitupate yale ya 1977 jumuia ya awali ya Afrika Mashariki iliposambaratika. Sababu zilikuwa tofauti za kiuchumi na kisiasa. Baada ya miaka miwili Tz na Uganda zikaingia vitani! Kumbe chokochoko za kisiasa kati ya hizi nchi mbili zilikuwa zikikua tangu Idd Amin alipompindua Obote mwaka 1971.Tofauti za kiuchumi kati ya Kenya na Tz kutokana na siasa za ujamaa(tz) na siasa ya upebari(Kenya)zilisababisha kutoelewana, Kenya ikidhani inacheleweshwa na Tz. Leo mambo yanaelekea kujirudia. Kuna chokochoko za kisiasa kati ya Rwanda na Tz. Hatutarajii kunyukana lakini upepo haujakaa sawa. Bandari ya Dar ni tishio kwa uchumi wa kenya. Kama bidhaa za Uganda na Rwanda zinaweza kupitia Mombasa Kenya itapumua zaidi. Kwa hali hiyo sishangai Kenya kuungana na Uganda na Rwanda katika harakati za kuikwepa bandari ya Dar! Katibu wa sasa wa jumuia hii Sezibera nadhani ni Myarwanda kama sio mtu wa Uganda. kwa vyovyote vile hawezi kukwepa mbinu hizi ili kuikomoa Tz. Mbona haya hayakuwepo wakati Mwapachu ni katibu wa jumuia hii? Rwanda kaingia juzi juzi katika jumuia hii. Sasa anaanza kuwa mwenyewe! Dunia hii!! Tuwashauri viongozi wetu waache ubinafsi na wajikite katika kushauriana na kushirikiana ili wawe na nguvu zaidi.

Toa maoni yako

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-burundi-zashikilia-msimamo-eac#sthash.XWXpKgzg.dpuf
  • .Kenya, Uganda na Rwanda wachafua hali ya hewa
HALI ya mambo imezidi kuwa tete katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya Tanzania na Burundi kutaka maelezo ya kina kutoka kwa nchi nyingine tatu wanachama za Kenya, Uganda na Rwanda zilizoanzisha ushirikiano mpya kinyemela kati yao, kwa kuzitenga nchi hizo mbili.
Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria kuwa Tanzania na Burundi zimetengwa na nchi hizo tatu ambazo zimeanzisha ushirikiano mpya kati yao kinyemela, kinyume cha mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo mwaka  1999.
Jumuiya ya sasa ilizaliwa tena upya Novemba 30, mwaka 1999 ikishirikisha nchi za Tanzania, Uganda na Kenya, wakati Rwanda na Burundi zilikaribishwa baadaye mwaka 2008.
Jumuiya hiyo mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).
Habari za hivi karibuni zilizopatikana kutoka ndani ya EAC zinabainisha kwamba Tanzania na Burundi zimekerwa na hatua ya nchi wanachama wenzao za Kenya, Uganda na Rwanda kuanza mchakato wa kuanzisha shirikisho la kisiasa bila ya kuzishirikisha nchi hizo.
Tanzania na Burundi zinaelezwa kuwa kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Agosti 31, mwaka huu, mjini Arusha zilimtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Shem Bageine, kutoka Uganda kutoa maelezo ya kina kuhusu hatua za nchi hizo tatu kufanya mambo ambayo yanakwenda kinyume cha mkataba wa Jumuiya hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa hata hivyo Bageine hakuwa na majibu muafaka kuhusu hatua hiyo na ndipo nchi hizo mbili zilipoazimia kuhitaji majibu ya kina zaidi kuhusu suala hilo katika kikao kijacho kitakachofanyika Novemba, mwaka huu.
Pamoja na suala la kuanzisha mchakato wa shirikisho la kisiasa, nchi hizo tatu pia zinaelezwa kukubaliana kuanzisha ushirikiano katika eneo la kukusanya kodi  (single costumes territory).
Masuala mengine ambayo yanaelezwa kutozifurahisha nchi za Tanzania na Burundi ni hatua yao ya kukubaliana kuwa na visa moja kwa watalii watakaotembelea nchi hizo, kuimarisha miundombinu hasa ujenzi wa reli kutoka Bandari ya Mombasa-Kenya hadi Kigali Rwanda kupitia Kampala-Uganda.
Moja wa maofisa wa EAC ambaye ni Mtanzania (jina linahifadhiwa) alilimbia gazeti hili la Raia Mwema kuwa hali ndani ya sekretarieti ya jumuiya hiyo ni mbaya na hata watumishi kutoka nchi za Tanzania na Burundi wameanza kutengwa na wenzao.
“Kumekuwa na kutokuaminiana miongoni mwa maofisa wa juu katika jumuiya yetu, watumishi wa Tanzania ni kama tunatengwa na wenzetu,” alidai mtumishi huyo bila ya kufafanua zaidi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mwezi uliopita Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya EAC, Dk. Richard Sezibera, alikanusha madai kuwa hali si shwari ndani ya Jumuiya anayoiongoza.
 Dk. Sezibera alikaririwa akisema: “Hali ni shwari katika jumuiya na kila kitu kinakwenda vizuri kulingana na mkataba wa jumuiya tofauti zinazojitokeza ni za kawaida katika jumuiya yoyote ile ya watu kutofautiana mawazo.”!
Taarifa zinaeleza kuwa katika utetezi wake, Bagaine ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki nchini Uganda, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kuwa mikutano iliyowakutanisha viongozi wakuu wa nchi hizo tatu iliratibiwa na wizara za mambo nje katika nchi husika.
Waziri huyo alieleza kuwa kwa kawaida mikutano inayohusiana na masuala ya Afrika Mashariki huratibiwa na wizara husika katika kila nchi, lakini kwa suala hilo ilikuwa kinyume hivyo asingekuwa na majibu muafaka.
“Kutokana na mgongano uliojitokeza ujumbe wa Tanzania ulitaka upewe maelezo yanayotosheleza katika kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri kinachotarajiwa kufanyika mapema Novemba, mwaka huu, kabla ya kikao cha wakuu wa nchi ambao watakutana Novemba 30,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.
Akizungumzia mzozo huo aliyekuwa Waziri wa kivuli wa Afrika Mashariki kutoka Kambi Upinzani Bungeni- CHADEMA, Mustafa Akonaay, alisema ilikuwa mapema kwa nchi wanachama waanzilishi wa jumuiya kuziruhusu Rwanda na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo.
“Hizi nchi mbili zilikuwa na matatizo ya ndani ya kiutawala baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu, hivyo ilikuwa ni mapema sana kuziruhusu kujiunga na jumuiya wakati bado zina matatizo ya ndani,” alieleza Akonaay.
Naye mwanzuoni maarufu katika diplomasia, Profesa Abdallah Safari, anasema katika msuguano huo kuna taarifa za muda mrefu kuwa baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wanataka kuharakisha shirikisho la kisiasa kwa maslahi yao wenyewe.
“Tetesi kuhusu suala hilo ni za muda mrefu na kulikuwa na mipango ya kupanua kitu kinachoitwa dola ya Wahima (Hima Empire) katika eneo la Maziwa Makuu hadi Tanzania, kuna uwezekano mipango hiyo bado iko vichwani mwa viongozi hao,” anasema Profesa Safari.
Anaongeza kusema; “Wakati mwingine sisi Watanzania ni chanzo cha kuanza kutengwa na wenzetu kutokana na kushamiri kwa tabia ya urasimu, uzembe na wizi katika sekta mbalimbali za umma na hata kushindwa kwenda sambamba na wenzetu ambao wanadhamira ya kufanya mambo kwa weledi zaidi.”!
Akitoa mfano Profesa huyo anasema katika sekta ya biashara Tanzania imeshindwa kuondoa urasimu katika Bandari ya Dar es Salaam kiasi cha wafanyabiashara kutoka nchi jirani wanaoitumia kusafirisha bidhaa zao kupata hasara.
“Mlolongo  huo wa mambo yasiyo na msingi unasababisha usumbufu kwa wafanyabiashara wengi wanaopitisha bidhaa zao katika ardhi ya Tanzania na bidhaa hizo hupanda bei marudufu katika masoko zinakopelekwa na hivyo kuongeza gharama kwa watumiaji,”!
Katika hatua nyingine, alidai hatua ya Tanzania kuanza kutengwa inatokana na uongozi dhaifu wa serikali.
“Hili la Rais kusafiri sana nalo ni tatizo na wenzetu wameona sisi kama Taifa hatuko makini  na wametumia mwanya huo kutaka kujitenga, kama kuna uongozi imara wasingethubutu kuanza kufanya mambo kama hayo kwa mlango wa nyuma,” anasema Profesa Safari.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Profesa Safari, ni vigumu kwa shirikisho hilo la kisiasa kufanikiwa haraka kutokana na changamoto kadhaa ikiwamo nchi husika kuwa na matatizo ya ndani, hasa ya kidemokrasia ambayo yalitakiwa kupatiwa ufumbuzi kwanza.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/tanzania-burundi-zashikilia-msimamo-eac#sthash.XWXpKgzg.dpuf