![]()
Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.
Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6. Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4 Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63 Methodius Kilaini shilingi 80.9 Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow Zitto: Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 Zitto: Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha |
Wednesday, 26 November 2014
Majina Ya Waliokula Fedha Za Akaunti Ya Escrow Katika Ripoti Ya PAC Iliyosomwa Sasa Bungeni
Friday, 14 November 2014
Bunge likatae miswada inayominya uhuru wa habari
Dar es Salaam Muungano wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) huenda ukapata nafasi kubwa katika Uchaguzi
Mkuu 2015, utafiti mpya wa Taasisi ya Twaweza umebanisha.
Utafiti huo umebainisha kuwa kuungana kwa vyama
hivyo kutaongeza ushindani na kukitisha Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambacho kina ngome imara. Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema,
NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Hata hivyo, takriban nusu ya Watanzania
waliohojiwa katika utafiti huo uliowataka kubainisha iwapo upinzani
ungesimamisha mgombea mmoja wangemchagua nani, walisema wangeichagua CCM
na karibu theluthi moja wangemchagua mgombea wa upinzani iwapo
watasimamisha mmoja.
Utafiti huo wa awamu ya 24 ulibainisha kuwa watu
wawili kati ya 10 walikuwa tayari kumpigia mgombea badala ya chama
wakati mmoja kati ya 10 akisema hajui angempigia nani iwapo upinzani
ungemsimamisha mgombea mmoja 2015.
“Kundi lililosema kuwa wangemchagua mgombea wa
upinzani lilipoulizwa kuwa nani anapaswa kuwa mgombea urais, watu wanne
kati ya 10 (asilimia 41) walimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa.
“Majina mengine ya viongozi wa upinzani yaliyopata
zaidi ya asilimia 10 ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kwa
asilimia 14 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akipata asilimia
kumi na moja.
Viongozi wengine wa upinzani waliotajwa kuwa
wangefaa kugombea urais ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto
Kabwe kwa asilimia sita huku Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakiambulia asilimia moja kila
mmoja.
Pamoja na mapendekezo hayo, bado karibu kila watu
wawili kati ya 10 (asilimia 21) walioulizwa swali hilo walisema hawajui
ni nani anafaa kugombea urais kupitia upinzani, jambo ambalo linaweza
kubadili matokeo hayo kwa urais katika dakika za mwisho.
Bunge likatae miswada inayominya uhuru wa habari
Serikali juzi iliwasilisha bungeni Muswada wa Sheria unaotishia
uhuru wa vyombo vya habari, lakini ikauchomoa baadaye jioni baada ya
kugundua kwamba umestukiwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Hatua hiyo ya Serikali ya kuwasilisha Muswada wa
Sheria ya Takwimu unaoonekana kulenga kukwamisha vyombo vya habari
katika kupata takwimu na kuzitumia katika habari na taarifa zinazotolewa
kwa wananchi, imeonekana kwa wengi katika tasnia ya habari kama
uthibitisho kwamba pengine Serikali haina dhamira ya kuona wananchi
wanapata haki ya kupata habari.
Moja ya kifungu cha muswada huo kilicholalamikiwa
na wabunge wengi ni Ibara ya 37 (4), ambacho kinaeleza kwamba wadau na
vyombo vya habari vitakavyotoa takwimu bila kibali cha Ofisi ya Takwimu
watakwenda jela miaka mitatu pamoja na faini ya Sh10 milioni au vyote
kwa pamoja.
Inasikitisha kuona kwamba adhabu hiyo kubwa kupita
kiasi imeungwa mkono na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na
Biashara, ambayo iliwasilisha maoni yake bungeni juzi.
Adhabu ya kosa hilo awali ilikuwa kifungo cha
mwaka mmoja, lakini katika hali ya kushangaza Kamati hiyo ilipendekeza
iongezwe hadi miaka mitatu eti kuzuia tabia ya baadhi ya watu kutoa
takwimu za uongo na kwa makusudi ili kupotosha jamii.
Hakuna anayepinga kuwapo umuhimu wa kuipa mamlaka
zaidi na kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutekeleza majukumu yake
ya kitakwimu kwa ufanisi, wala hakuna anayepinga uanzishwaji wa mfumo
thabiti wa utoaji wa takwimu unaokusudia kuboresha na kuimarisha takwimu
rasmi nchini.
Jambo hilo tumekuwa tukilisisitiza mara kwa mara na kwa kweli tunadhani Serikali imechelewa sana kuanza kuchukua hatua.
Hata hivyo, tunadhani Serikali inafanya makosa
kudhani kwamba uchapishaji wa takwimu zisizo sahihi unatokana na watu
kutaka kupotosha jamii na kuleta machafuko.
Ni kweli kwamba katika mazingira fulani takwimu
zisizo sahihi zinaweza kusababisha vurugu, lakini pia lazima tukubali
kwamba Serikali yenyewe ndiyo inapaswa kubeba lawama kwa uzagaaji wa
takwimu zinazokinzana na zisizo sahihi.
Tangu tupate uhuru Serikali haijawahi siyo tu kuwa
na utamaduni wa kuheshimu na kutunza takwimu, bali pia kuweka mazingira
ya kuboresha ukusanyaji wa takwimu kwa kuweka mfumo thabiti na
kuboresha Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Hivyo kama ni kupotosha takwimu, Serikali ndiyo
imekuwa mpotoshaji namba moja. Hii imetokana na kutokuwapo mfumo wa
kuainisha takwimu kutoka katika wizara, taasisi za Serikali, sekta ya
umma na sekta binafsi kama inavyofanyika katika nchi nyingi duniani. Kwa
mfano, hatudhani kama Serikali inazo takwimu sahihi kuhusu Deni la
Taifa hivi sasa.
Tunachotaka kusema hapa ni kwamba muswada huo wa
Sheria ya Takwimu uliochomolewa bungeni juzi ulilenga kuvibana vyombo
vya habari na kuminya uhuru na haki ya wananchi kupata habari.
Kwa miaka minane sasa, Serikali imekuwa ikisuasua kupeleka
bungeni Muswada wa Sheria ya Uhuru wa Habari na Vyombo vya Habari, hata
baada ya kuihakikishia jumuiya ya kimataifa mara kwa mara kwamba muswada
huo ungepelekwa bungeni.
Tunadhani Muswada wa Sheria wa Takwimu ni
mwendelezo wa mkakati wa Serikali wa kuvibana vyombo vya habari. Bunge
litafanya vyema kuukataa iwapo Serikali itaurudisha ukiwa na maudhui
yaleyale yaliyoufanya uchomolewe bungeni juzi.
Mbowe amtaka Kikwete avunje Baraza la Mawaziri
Kigoma. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtaka Rais
Jakaya Kikwete kulivunja Baraza la Mawaziri na kuunda jipya kutokana na
tuhuma za ufisadi.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya
habari baada ya mikutano yake katika mikoa ya Magharibi alisema ni
lazima hatua hiyo kuchukuliwa ili kukabiliana na mafisadi ambao
hakuwataja, vinginevyo alisema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
anayoiongoza, itaanza maandalizi ya kuwasilisha bungeni, hoja ya
kutokuwa na imani naye.
Alisema Serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua
za ufisadi ambazo zinawakabili watendaji wake: “Kambi ya Upinzani
Bungeni inamtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na mawaziri wake na kuunda Serikali mpya.”
Hivi karibuni, Mbowe alitoa tuhuma nzito kuhusu
ufisadi katika ujenzi na bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es
Salaam akisema kuna ufisadi umefanywa na vigogo wa Serikali wakiwamo
baadhi ya mawaziri.
Alisema mradi huo ulitakiwa kugharimu Sh1.2
trilioni lakini vigogo hao wakaongeza kiasi kama hicho na sasa
unagharimu Sh2.4 trilioni. Alitaka kuteuliwa kwa taasisi ya kimataifa ya
ukaguzi ili kufahamu thamani halisi ya ujenzi wa bomba hilo.
Alisema kutokana na ufisadi huo na mwingine katika
Akaunti ya Tegeta Escrow, ni dhahiri kuwa Baraza la Mawaziri
limeshindwa kazi ya kumsaidia Rais.
Mbowe amnanga Zitto
Katika mkutano wa juzi mjini Kigoma, Mbowe
alimzungumzia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe
akisema alimsaidia kuhakikisha anashinda ubunge wa Kigoma Kaskazini
mwaka 2005 lakini akakosa shukrani.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Kata ya Kalinzi
iliyopo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mbowe alisema hamchukii Zitto
kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali mbunge huyo alikiuka maadili ya
chama hicho akavuliwa uongozi.
“Nilimshauri Zitto Kabwe akagombee katika Jimbo la
Kigoma Kaskazini, lakini akaniambia kwamba hawezi kufanya hivyo kwa
sababu hana fedha, nikampa fedha za kutosha, nikampa gari Toyota Hilux
la kuzungukia katika jimbo na akawa mbunge.
Alisema gari hilo hajawahi kulirudisha hadi leo na
yeye hakumuuliza kwa sababu alimchukulia kama ndugu yake... “Zitto ni
kama mdogo wangu, amelala na kula nyumbani kwangu, nyumba yangu ilikuwa
kama yake, nashangaa anakosa shukrani.”
Alisema kabla ya kugombea alimlipia nauli kutoka
Ujerumani kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta nafasi hiyo ya ubunge,
hivyo anashangaa mtu wa aina hiyo amchukie kwa lipi.
Mbowe alisema Mkoa wa Kigoma umebahatika kuwa viongozi wa
upinzani wenye uwezo lakini wamekuwa wakiwasaliti wananchi wa mkoa huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum
Mwalimu alisema uchaguzi wa serikali ya vijiji, mitaa na vitongoji kiwe
kipimo cha kuing’oa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Aliwataka vijana kufanya uamuzi sahihi kwenye uchaguzi huo kwa kuvichagua vyama vinavyounda Ukawa kwa kuwa CCM imewatelekeza.
Zitto ajibu
Akizungumzia madai ya Mbowe, Zitto alisema ni
utoto kwenda kumtangaza kwamba alimsaidia... “Yeye Mbowe anajua
nilivyomsaidia pia lakini kwa kuwa nimelelewa kwa maadili mema na wazazi
wangu siwezi kumtangaza. Ila muulizeni alikuwa na hali gani baada ya
uchaguzi wa mwaka 2005 na nilimsaidia nini?
“Nimeshangazwa na tabia hiyo ya kusimanga tena
kunisimanga kwetu, nyumbani kwetu. Hata hivyo, nimepuuza maana kwa
vyovyote vile aliongea bila kufikiri.
“Anasema nilitaka kusaliti chama, aseme kwa ushahidi maana kutamka tu hakuna maana kitu hata kidogo.”
Alisema kiongozi mkubwa kama Mbowe anapaswa
kujadili masuala ya Taifa na namna ya kutatua changamoto si, kusema watu
na kuwasimanga.
“Nimeibadilisha Kigoma na kusimamia ujenzi wa
miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Yeye kafanya
nini Hai? Nimewezesha wakulima wangu kuwa na hifadhi ya jamii, bima ya
afya na kukuza uzalishaji, yeye kafanya nini Hai?
Nimeibua hoja bungeni za maana ikiwamo kubadili
sheria kwa manufaa ya nchi. Yeye kafanya nini bungeni tangu aingie,
ametoa hoja gani binafsi, ametunga sheria gani binafsi?
Friday, 31 October 2014
Mkapa atoa ya moyoni rais 2015
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, amezungumzia mbio za kuwania urais wa
2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akitaja sifa za mtu anayepaswa
kuteuliwa kuwa mgombea wake, ikiwamo ya kukubalika na kuuzika kwa jamii.
Amesema kukubalika na kuuzika kwa mtu katika siasa kunatokana na utendaji, haiba, wasifu na ushawishi wa mtu huyo ndani ya chama na serikalini na kwamba, umri siyo kigezo cha kuangaliwa ingawa siyo dhambi vijana wakajitokeza kujitosa katika kinyang’anyiro hicho.
Mkapa, ambaye anasifika kwa kuwa kiongozi jasiri na asiyemung’unya maneno, alisema hayo wakati akihojiwa na televisheni ya Citizen ya nchini Kenya, kwa njia ya simu.
Alikuwa akihojiwa juu ya kifo cha Rais wa Zambia, hayati Michael Satta, aliyefariki dunia, jijini London, nchini Uingereza Jumanne wiki hii.
Katika mahojiano hayo, Mkapa pia aliulizwa na mwandishi kuhusu Tanzania kutazamiwa kufanya uchaguzi mkuu mwakani huku mambo mengi yakisikika, hasa kwa wanaojitokeza kupitia CCM kutaka kuwania urais katika uchaguzi huo hadi wengine kufikia kuadhibiwa na chama.
Kabla ya kujibu, Mkapa alianza kwa kucheka na kisha akasema anachelea kupata jibu sahihi kuhusiana na swali aliloulizwa na mwandishi.
“…Ila niseme CCM ni chama kikongwe na kina hazina kubwa ya kutosha. Na Katiba ya chama chetu inaelezea kuhusu dhumuni la chama chetu, kubwa ikiwa ni kuhakikisha tunakamata dola, kuanzia serikali za mitaa mpaka serikali kuu. Sasa swali ni kwamba, dola inakamatwaje?” alihoji Mkapa.
Aliongeza: “Chama kama chama lazima muwe na mtu anayeuzika na kukubalika katika jamii kwa utendaji wake, haiba yake, wasifu wake (ndani ya chama na serikali).
“Lakini vile vile, ushawishi wake...Haya mambo ya umri na kadhalika, sisi hatukutazama wakati huo. Ila siyo dhambi vijana wakijitokeza. Maana yake hata wakati wangu, Rais wa sasa Mheshimiwa Kikwete na kina Lowassa walijitokeza. Na leo unaona Kikwete ndiye Rais.”
Alisema wakati wa utawala wake, viongozi wenzake wengi walihisi na kuamini kuwa hakuwa akimuunga mkono Rais Kikwete.
“Lakini mwandishi, nataka nikuhakikishie, hata kama mimi Ben Mkapa siko na Kikwete, mwisho wa siku wanachama ndiyo watakaosema wewe humtaki ila sisi tuachie huyo huyo...,” alisema Mkapa.
Aliongeza: “Na hayo yalijitokeza mwaka 2005. Watu walimtaka Mheshimiwa Kikwete. Sasa mimi kuwa mwenyekiti wa chama hakunipi Mandate (mamlaka) ya kushindana na walio wengi. Na mliona (Kikwete) alishinda kwa asilimia kubwa kweli kweli”.
“Hivyo CCM ina taratibu zake na wanajua nani anafaa. Maana yake siasa hizi, tuhuma zingine za kipuuzi kweli kweli. Sasa mkiendekeza tuhuma, mwishowe mnakuta mnabaki bila chama. Na kwenye siasa mkianza kutuhumiana, hakuna wa kusimama...”
Alisema yeye binafsi, anaamini chama kitapata mtu safi, mwenye nguvu ya kukisaidia chama na serikali na kuendeleza yatakayoachwa na Rais Kikwete.
Mkapa alisema hakuna chama duniani kinachoona fulani atakivusha halafu kimwache na kusema kufanya hivyo, maana yake ni kukiua chama.
“Hivyo, hata sisi vyombo vyetu vya ndani vilikuwa vinatueleza kabisa kwamba, fulani yuko vizuri sana. Ila labda kuna aka katatizo. Sasa ako katatizo tunakafanyia kazi kwa maslahi ya chama na kwa maslahi ya huyo ajaye,” alisema Mkapa na kuongeza kuwa ana amini ndivyo ilivyo mpaka sasa.
Alisema tafiti zimefanyika na kwamba, anaamini wamesikika watu wakisema wanamtaka nani.
“Na wakati wangu mimi mgombea alikuwa ameshatungiwa nyimbo na watu mbalimbali wenye mapenzi naye. Hivyo, labda hata sasa yaweza kuwa hivyo...Waswahili walisema nyota njema huonekana asubuhi,” alisema Mkapa.
Aliongeza: “Nimalizie kama nilivyosema, ukongwe wa CCM na viongozi wake, naamini watapata mtu bora na mwenye nia njema na Taifa hili...”
Akijibu kuhusu wana CCM waliotajwa kwamba, anaamini yupo mmoja au wawili, ambao ameona wanaweza ama kufuata nyayo zake au za Mwinyi au za Mwalimu Nyerere au za Rais Kikwete, kwanza alianza kwa kucheka.
Baada ya kicheko, Mkapa alisema Tanzania kuna Kamati ya Maadili na kwamba, yeye na wenzake hivi sasa kikatiba ni wazee washauri, hivyo akasema vikao vya chama ndivyo vitakavyowaongoza na baada ya hapo, nao wanaenda na mtu huyo huyo.
Makada wa CCM waliowahi kutuhumiwa kuanza kampeni za kuwania urais mwaka 2015 kabla ya kuzuiwa na chama kupitia Kamati yake Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu kujihusisha na suala hilo kwa miezi 12, huku mienendo yao ya kisiasa ikifuatiliwa, ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Wengine ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira.
Yumo pia aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, pia hivi karibuni alikaririwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akitangaza nia yake ya kuwania urais 2015. Mwingine aliyekwisha kutangaza nia ya kuwania urais mwakani ni Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalla.
KUHUSU USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI (UKAWA)
Akijibu swali kuhusu ushirikiano uliosainiwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD wa kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi, kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa hadi urais kama ilivyokuwa kwa Kenya, Mkapa alisema bado hajajua
sera za vyama hivyo na namna makubaliano yao yalivyo.
Alisema pia bado hajaelewa kama inawezekana kuufananisha ushirikiano wa vyama hivyo na muungano wa Coard na Jubilee uliokuwapo nchini Kenya.
“Otherwise I'd like to wish them all the best (vinginevyo ningependa kuwatakia kila kheri),” alisema Mkapa na kumfanya mwandishi aangue kicheko.
KIFO CHA RAIS SATTA
Akimzungumzia hayati Rais Satta, Mkapa alisema hakuitwa “King Cobra” kimakosa, bali alistahili kutokana na uwezo aliokuwa nao ama wa kimaamuzi au wa kimsimamo.
“Nina hakika sana kwamba Wazambia na sisi kama Mataifa ya Afrika tutamkumbuka daima ndugu Satta. Satta daima alikuwa kwa ajili ya watu wake na Bara letu kwa jumla. Alisema na kusimamia kile alichokiamini kuwa ni cha kweli na chenye mafanikio, Satta ataendelea kuwa kiongozi mzuri daima,” alisema Mkapa.
Aliongeza: “Hivyo, maumivu yanayotukabili kwa kumpoteza Mzee Nyerere, Mzee Nkrumah, Mzee Mandela, Mzee Kenyatta ni sawa na yale yanayotukabili leo tunapomjadili Mheshimiwa Satta (Inatosha kusema kwamba tumempoteza shujaa mwingine katika Bara letu) Naitakia roho yake mapumziko ...”
Akijibu swali namna anavyoziona siasa za Afrika akiwa Rais mstaafu, Mkapa alisema ni kawaida na hana jambo kubwa la kusema japo kuna mengi yanatokea, ambayo mengine ni ya hovyo.
“Mathalan, Waafrika wazee wetu, walipigania sana ukombozi wetu. Ila nadhani wengi bado kuna watu wana matatizo na wanahitaji kukombolewa kifikra,” alisema Mkapa.
Aliongeza: “Maana yake kuna wenzetu wanatumika pasipo kujua na kusababishia nchi zao kuingia katika matatizo, kama vita na wengi wao wameanza kujuta”.
“Hivyo, ni lazma ifikie mahali watu waweze kujitambua na kujua ni yepi malengo mema kwa Bara letu ni yepi tunashinikizwa...” aliongeza kusema Mkapa.

Lowassa amuombea radhi Sitta kwa Kanisa
Wakati Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (MBK) ikitarajia
kuingia katika hatua ya kura ya maoni mwakani, Waziri Mkuu Mstaafu,
Edward Lowassa, ameibuka na kuliomba radhi Kanisa Katoliki kufuatia
mgongano iliyojitokeza kati ya kanisa hilo na baadhi ya viongozi
serikali na wa Bunge hilo.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, aliomba msamaha huo wakati akitoa salamu zake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge, mkoani Morogoro.
Alisema Kanisa Katoliki lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na mshikamano nchini, hivyo mambo yaliyojitokeza yanapaswa kusamehewa.
“Najua hivi karibuni tumewaudhi, lakini mimi naomba mtusamehe bure tu, kama vile mzazi anavyomsamehe mtoto wake anapokosea,” alisema Lowassa na kuongeza kuwa Kanisa Katoliki ni muhimu katika maendeleo ya nchi.
Ingawa Lowassa hakueleza kwa undani tofauti zilizojitokeza kati ya Kanisa hilo na baadhi ya viongozi wa serikali, lakini wakati BMK likiendelea, taasisi za dini zilisambaza waraka uliosainiwa na viongozi wake ukilikosoa Bunge hilo kwa mambo mbalimbali ikiwamo kuendelea kujadili rasimu bila maridhiano kutokana na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia.
Kadhalika, viongozi wa madhahebu hayo ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT) na Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walilikosoa BMK kwa kupuuza maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Waraka huo ulisababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kujiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi na wa hovyo hovyo.
Sitta ambaye alitoa kauli hiyo Oktoba Mosi mwaka huu, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa waraka wa maaskofu una lugha ya Ukawa, ingawa maaskofu kwa upande wao waliueleza kuwa ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.
Sitta alitoa kauli ya kuuponda waraka huo bungeni alipokuwa akielezea mwenendo wa upigaji kura za kupitisha ibara na sura za rasimu ya katiba iliyopendekezwa kabla ya upigaji wa kura na wakati wa kutangaza matokeo, akisema watu wa Mungu kama maaskofu hawawezi kutoa waraka kama huo na kudai kuwa amekuwa akituhumiwa kwenye mitandao kwamba anadharau maaskofu.
“Nimalizie na viongozi wangu wa kiroho…mababa zangu maaskofu, natuhumiwa sana kwenye mablog kwamba nadharau maaskofu. Wakiwa na matendo kama hayo hao baadhi ya maaskofu itabidi tuendelee kuwadharau,” alisema na kuongeza:
“Ninao waraka huu ambao umelazimishwa kutumwa katika makanisa. Sioni utukufu wa Ukristo katika waraka huo. Huu waraka unamwamuru Rais airudishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba.”
Kuna Ukristo hapa?” alihoji na kuendelea: “Waraka huu unamlazimisha Rais asitishe mchakato wa Bunge Maalum…tangu lini watu wa kiroho wanatoa maagizo ya kisiasa? Hii sio haki hata kidogo…kuna Ukristo hapa? Waraka una lugha za wale Ukawa tuliowazoea.”
“Hivi kweli maaskofu wa Kikristo wanaweza kusema kwamba Wizara ya Katiba na Sheria irudishe tovuti ya Tume ya Jaji Warioba na kuirejeshea nyaraka zake zote ili wananchi wasome na kujifunza?” alihoji Sitta.
“Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauriwa na chama tawala, hivyo basi Bunge la Katiba lijadili na kuboresha tu rasimu ya katiba na si kubadilisha,” alisema Sitta.
“Waraka huu kwa shinikizo la maaskofu umesambazwa kwenye makanisa na kusomwa. Mimi nasema kama Mkristo, tukianza kuruhusu nchi yetu kutoa nyaraka hizi za kisiasa zisomwe makanisani kwa kudai huo ni msimamo wa maaskofu, basi nchi hii tutaipeleka kubaya.
“Na mini kama mtu mzima lazima nionye kuhusu tabia hii, ukizingatia nchi hii haina dini, hawa baadhi ya maaskofu ambao walikusanywa Dar es Salaam na makundi yale yale yanayohusishwa na Ukawa, kama wao ni wanachama wa siri wa vyama vya siasa vinavyochukia CCM wajitokeze waziwazi,” alisema Sitta.
Sitta aliendelea kunukuu waraka huo kwamba kuna askofu mmoja ameapa kwamba atawaelimisha waumini wake ili siku za usoni wawashughulikie viongozi kama mimi (Sitta). Nasema aendelee, lakini Mungu anaona yote yaliyo moyoni mwetu.”
Baada ya Sitta kutoa kauli hiyo, Askofu wa Jimbo la Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwande, alisema matamshi ya Sitta yanaonyesha anavyohangaika kualalisha kilicho haramu.
Alisema kitendo cha Sitta kuendesha BMK kwa kukejeli wajumbe wenzake walioondoka bungeni (Ukawa) na wajumbe walioandaa rasimu ya pili kwenye Tume ya Katiba Mpya chini ya Jaji Joseph Warioba, ni jambo la aibu ambalo halivumiliki, na ndiyo maana walitoa waraka wa kutokubaliana nacho.
“Kwa kweli Sitta ametutukana, ametafuta ubaya kwa viongozi wa dini, kwa kuwa tumesema ukweli ? Sisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu kwa Wakristo …tulizungumza kutokana na hitaji la wakati, na ulikuwa waraka wa unabii,” alisema.
Viongozi wengine wa kanisa Katoliki waliojibu kauli za Sitta ni Makamu Mwenyekiti wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini, ambaye alinukuliwa akisema kuwa Sitta amelewa madaraka.

JK: Watendaji wakuu wananikwamisha
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amewatuhumu baadhi ya
watendaji wa serikali yake kuwa ni kikwazo katika kufanikisha masuala
mbalimbali ya maendeleo kutokana na urasimu usiokuwa wa lazima katika
kutoa huduma kwa wananchi.
Akifungua kongamano la miaka 10 ya Tume ya
Utumishi wa Umma Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alikemea na kulaumu
tabia ya baadhi ya watendaji hao wa Serikali ambao wamekuwa wakikwamisha
kwa makusudi kasi ya viongozi wa kisiasa ya kuleta maendeleo.
“Katika utendaji wa baadhi ya watendaji wakuu wa
Serikali limekuwa ni tatizo na wamekuwa wakikwamisha sana kasi ya
utekelezaji wa haraka wa malengo ya kisiasa,” alisema.
“Mara nyingine, viongozi wa kisiasa wamekuwa mbele
kimtazamo kuliko watumishi wa umma, hili limekuwa tatizo sana katika
utekelezaji wa malengo kwa haraka,” alisema Kikwete.
Alisema kumekuwa na malalamiko kwa makatibu wakuu
wa wizara kutoka kwa wawekezaji ambao huwachelewesha kwa makusudi kwa
visingizio vya kufuata utaratibu.
Alisema katika kufuatilia, amekuwa akilazimika
kuingilia utendaji wa baadhi ya wizara ili kuhakikisha mambo yanakwenda
na mara nyingine urasimu huo umekuwa ukifanywa kwa makusudi ili
kuwachosha wawekezaji na ‘kuwatoa upepo’ kwa manufaa binafsi.
“Haya ni malalamiko makubwa sana na yanatoa picha
mbaya kwa nchi yetu…watendaji wa namna hii ni lazima wabadilike,
ninahitaji kuona mabadiliko makubwa kwa kupitia Tume ya Utumishi ambayo
inatakiwa kukaa na hawa watumishi na kuwapa mafunzo ya kiutendaji
yanayoendana na mahitaji ya sasa,” alisema.
Abeza zawadi ya uprofesa
Akizungumzia utaratibu wa upandishwaji vyeo, Rais
Kikwete alisema ni muhimu weledi ukazingatiwa na utaratibu uliowekwa
ukaheshimiwa, kwamba lazima wafanyakazi wapandishwe vyeo na madaraja
ndani ya kipindi kilichowekwa, ambacho ni miaka mitatu.
Alisema kumekuwa na malalamiko kwa wafanyakazi
wengi wa Serikali kutopandishwa vyeo kwa muda mrefu na hata
wanapopandishwa vyeo mabadiliko ya mishahara kuendana na vyeo na
madaraja mapya hayafanyiki kwa wakati.
Alieleza kwamba utaratibu unaotumika katika vyuo
vikuu wa namna ya kuwapata wahadhiri wasaidizi, wahadhiri, maprofesa ni
wa wazi na ni mfano wa kuigwa kutokana na namna unavyofanyika, kwa kutoa
mafunzo kisha kuyathibitisha na kumpandisha mhusika daraja.
“Vyuo vikuu wana ngazi wanazotakiwa kuzipitia na
mafunzo maalumu hadi mtu anakuwa profesa. Siyo honorary professor
(uprofesa wa heshima) niliopewa mimi nilipokwenda China…walinishtukiza.
Nilifika pale wakanipiga na uprofesa, nikasema haya sasa makubwa!
(kicheko),” alisema.
Alisema matatizo ya upandishwaji vyeo yasipotatuliwa kwa wakati
ni tatizo kubwa kwa Serikali hasa unapokutana na vyama vya wafanyakazi
vyenye nguvu kama Chama cha Walimu na wanapofikia hatua ya kusema
wanagoma, unalazimika kuwaangukia.
Alisema suala la mtumishi kupandishwa cheo ni haki
yake ya msingi kazini hivyo hatarajii kusikia matatizo ya malalamiko ya
watumishi kutopanda vyeo kwa wakati.
Ukawa na dhana ya nguvu ya mnyonge au ‘zamu yetu kula’
Dar es Salaam. Kwa jumla, kuungana ni jambo jema kwani muungano
huongeza nguvu. Muungano ni silaha ya mnyonge dhidi ya mwenye nguvu.
Ni kwa sababu hii, tumekuwa tukipigania umoja wa
Afrika ili kujenga nguvu ya pamoja dhidi ya mabeberu wa mataifa ya
Magharibi tukiamini kwamba bila nguvu moja mataifa ya Afrika hayataweza
kuukabili ubeberu wa mataifa haya.
Tunao msemo maarufu usemao nguvu ya mnyonge ni
umoja na hivi ndivyo waasisi wa mataifa ya Afrika walivyofanya katika
kumfukuza mkoloni.
Bila kujali tofauti zao za kikabila na vinginevyo,
wananchi wa Afrika waliunganisha nguvu na hatimaye pamoja na silaha zao
duni, wakafanikiwa kumfukuza mkoloni katika ardhi ya Afrika.
Katika uwanja wa siasa, vyama vya siasa huungana
kwa sababu mbalimbali lakini sababu tatu ni za msingi zaidi. Mosi,
huungana pale ambako hakuna chama kinaibuka na ushindi wa moja kwa moja
katika uchaguzi ulio na ushindani mkali.
Katika mazingira haya, inakuwa hakuna chama
kinachoweza kuunda serikali imara peke yake bila kushirikisha kingine
kwa sababu hakitaweza kupitisha sera au sheria yoyote bungeni.
Hivi ndivyo vyama vya Conservatives na Liberal
Democrats vilivyoungana huko Uingereza baada ya vyama vikuu nchini humo
vya Labour na Conservatives kushindwa kupata ushindi ambao ungekiwezesha
chama kimojawapo kuunda serikali na kupitisha sera bungeni bila
msukosuko mkubwa.
Hivi ni vyama ambavyo vina itikadi na msimamo
tofauti kabisa kifalsafa na ilibidi viongozi wake wakae saa nyingi
kukubaliana programu ya kutekeleza kabla hawajakubaliana kugawana nafasi
za uongozi.
Kiongozi wa Liberal Democrats, Nick Cleggy
alimshinikiza David Cameroon akubaliane na masharti ya kulegeza misimamo
mikali ya chama chake kuhusu sera ya uhamiaji na hifadhi ya jamii kabla
hajakubali kuingia naye ubia kuunda serikali.
Cameron amekiri mara kadhaa kwamba alilazimika
kulegeza msimamo kuhusu sera mama za Conservatives ili kufanikisha
kuwashawishi Liberal Democrats kuunda nao serikali vinginevyo Nick
Cleggy angeunda serikali na Gordon Brown wa chama cha Labour.
Ni katika mazingira ya chama kimoja kushindwa
kupata ushindi wa wazi ambayo yalivilazimisha vyama hasimu vya CUF na
CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar.
Pamoja na kwamba SUK iliundwa kama njia sahihi ya
kuepusha shari na vita visiwani, msingi wa serikali hiyo ni ukweli
kwamba hakuna chama chochote kati ya hivi viwili chenye uwezo wa kuunda
serikali imara kwa sababu ushindi wa chama chochote huwa ni mwembamba.
Hata hivyo, hatujui ni kwa kiwango gani vyama vya CUF na CCM huko
Zanzibar vilikubaliana kutekeleza programu ya pamoja inayotokana na sera
za vyama hivyo viwili.
Sababu ya pili ya vyama kuungana ni kuunganisha nguvu katika jitihada za kumwondoa adui anayefanana.
Kwa mfano, huko Zanzibar kabla ya mapinduzi ya
mwaka 1964, vyama kadhaa viliungana katika jitihada za kuuondoa utawala
wa Sultani uliokuwa unaendeshwa kibaguzi. Kwa hiyo, adui hapa alikuwa
Sultani na ubaguzi wake wa rangi.
Sababu ya tatu ni pale vyama vinapounganisha nguvu
ili kushinda uchaguzi kwa kutambua kwamba vikiingia kwenye uchaguzi
kimoja, kimoja havitaweza kushinda kutokana na nguvu kubwa aliyonayo
mshindani wao.
Hata hivyo, kushinda uchaguzi hakuwezi kutokana na
kuunganisha nguvu ya kiuongozi pekee. Ni lazima kuunganisha pia nguvu
ya kiitikadi, kifalsafa na kisera ili kuweza kujipambanua kwa wananchi.
Muungano wa kisera ni muhimu ili kuweza kutabirika
tabia za wagombea watakapokuwa madarakani. Aidha, ni programu ya kisera
inayoweza kuongoza kuchagua mgombea anayefaa zaidi kushika usukani wa
utekelezaji wake baadaye.
Muungano wa vyama vinavyounda Ukawa umepokewa kwa
shangwe kubwa. Furaha hii inatokana na msingi nilioueleza hapo awali
kwamba wanyonge wakiungana hupata nguvu ya ajabu hata ya kuweza
kuangusha milima.
Kwa hiyo, watu ambao wamekuwa wakisubiri utawala
wa CCM kuanguka wanaamini kwamba kwa muungano huu angalau vyama vya
upinzani vitafuta unyonge.
Nami naungana na Watanzania wengine kuwapongeza
viongozi wa vyama ya Chadema, CUF, NCCR na NLD kwa ujasiri na uthubutu
waliouchukua katika kujaribu kushirikiana katika chaguzi mbalimbali
zijazo.
Lakini tunapowapongeza Ukawa, ni vizuri kutambua
kwamba kuunganisha nguvu kama walivyofanya ni hatua moja tu inayopaswa
kuanzisha hatua nyingi huko mbele. Hatua muhimu inayofuata sasa ni
kujipambanua kwa wananchi kiitikadi, kifalsafa na kisera.
Kwa bahati viongozi wa sasa wa vyama vilivyoungana siyo watu wanaoamini katika mambo ya itikadi na falsafa.
Hawa ni viongozi ambao huitwa ‘wayakinifu’
(pragamatists). Myakinifu ni kiongozi anayeamini katika kinachowezekana
leo na haongozwi na falsafa bayana ya kisiasa.
Kwa hiyo kiongozi yakinifu atambeba yeyote
anayeona anafaa na huwezi kumuweka katika mrengo wowote kiitikadi.
Kimsingi, hii ndiyo aina ya viongozi tulionao sasa tangu Mwalimu Julius
Nyerere alipoondoka.
Ndiyo maana tumekuwa Taifa ambalo si la kijamaa, wala kiliberali wala kibepari. Tupotupo tu maadamu siku zinakwenda.
Pamoja na uyakinifu wao, bado naamini kwamba Ukawa
watahitaji programu ya pamoja ya kisera. Hii ni hatua muhimu ili kutoa
nafasi kwa wananchi kupima aina ya serikali watakayounda kama watashinda
katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Bila msimamo yakinifu wa kisera, ni rahisi
kutofautiana kwa sababu ya kukosa msingi wa kugawana madaraka. Bila sera
yakinifu, utakapofika wakati wa kugawana nafasi za kugombea na hatimaye
katika kuunda Serikali watalazimika kuzingatia sifa za kuchagulika na
umaarufu badala ya sifa za kiuwezo.
Nakumbuka mwaka 2005 palipokuwa na jitihada za
kuunda ushirikiano kama huu wa sasa, nilipewa jukumu la kufanya utafiti
kujua nani alikuwa anakubalika zaidi katika Jimbo la Ubungo kati ya
mgombea wa Chadema (John Mnyika) na mgombea wa CUF (marehemu mama
Minja).
Niliandaa hojaji na nikaligawa katika kata zote za
Jimbo la Ubungo kwa kutumia sampuli iliyopatikana kwa njia ya bahati
nasibu. Matokeo yalionyesha kwamba Mnyika alikuwa anakubalika kwa mbali
dhidi ya wagombea wengine wa upinzani.
Hata hivyo, katika kikao cha kujadili matokeo
hayo, wawakilishi wa CUF waliyakataa na kunituhumu kwamba nilikuwa
napendelea chama changu na huo ndiyo ukawa mwanzo wa ushirikiano
kusuasua na hatimaye kusambaratika kabisa kabla ya kampeni kuanza.
Yote hii ni kwa sababu tuliwekeza zaidi kwenye kugawana wagombea lakini hatukuwekeza kabisa katika ushirikiano wa kisera.
Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba, muungano
wowote endelevu wa vyama vya siasa Tanzania, lazima uwe wa kuunganisha
nguvu za wanyonge dhidi ya mabavu ya chama dola cha CCM.
Muungano wa namna hii lazima uwaunganishe kisera Watanzania na ndiyo unaopaswa kuwa msingi wa kugawana vyeo.
Lipumba: Kwanza CCM ing’oke, ruzuku baadaye
Dar es Salaam. Wakati Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi akisema suala la ruzuku na viti maalumu ni changamoto kwa Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba amesema hicho si kipaumbele.
“Tunachokitaka ni kuunganisha nguvu zetu ili
kuhakikisha tunaing’oa CCM madarakani kwanza, masuala mengine kuhusu
ruzuku tutaweka utaratibu maalumu baadaye,” alisema.
Profesa Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa
Ukawa, alisema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akiwaeleza waandishi
wa habari maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lililokutana
Jumatatu na Jumanne iliyopita.
“Wenzetu Kenya waliweza kuungana na kuhakikisha
wanaking’oa chama tawala madarakani, lakini sasa kwa hapa mkiungana na
kuwa chama kimoja ni lazima msajili chama chenu, sasa tunachokitaka ni
kushirikiana tu kwanza,’’ alisema.
Alisema suala la ruzuku na uteuzi wa viti maalumu
siyo lengo kuu la Ukawa inayoundwa na vyama vinne; CUF, Chadema,
NCCR-Mageuzi na NLD kwa kuwa linajadilika. Alisema jambo la msingi hivi
sasa ni ushirikiano wa amani.
Alisema kinachotakiwa kwa viongozi wa Ukawa ni
kuaminiana kwanza ili kulinda muungano huo ambao alisema umeshaanza
kukitikisa chama tawala, CCM.
Maazimio ya Baraza Kuu
Alisema Baraza hilo lilisisitiza umuhimu wa
kuaminiana miongoni mwa vyama washirika katika ngazi zote ili kudumisha
umoja huo na kufikia lengo la kuitoa CCM madarakani.
“Baraza limetaka uwepo utaratibu mzuri na wa wazi
utakaoonyesha mambo ya msingi ambayo vyama vinavyounda Ukawa
vimekubaliana. Utaratibu huu uwafikie viongozi wa ngazi zote za chama
ili kuhakikisha jukwaa la Ukawa linatumika kwa lengo na dhamira iliyopo
ndani ya hati ya makubaliano ambayo ni kuing’oa CCM madarakani,”
alisema.
Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa Profesa
Lipumba alisema Baraza limetaka sheria irekebishwe ili uchaguzi wa
diwani ufanyike pamoja na wa viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji kwa
wakati mmoja, kwa vile diwani ndiye kiongozi mkuu wa kuchaguliwa wa
kata.
Baraza hilo pia limetaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), iratibu na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
utengenezwe utaratibu ambao utaifanya Tume hiyo kuwa huru kuwezesha
chaguzi zote zijazo kufanyika kwa uhuru na haki.
“Taarifa za Tume zilieleza kuwa itaandikisha
wapigakura mpaka kwenye ngazi ya vijiji na vitongoji, kwa hiyo uchaguzi
wa Serikali za Mitaa usubiri mpaka daftari la kudumu la wapigakura
likamilike na ndilo litumiwe kwenye uchaguzi huo,” alisema.
Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, Profesa Lipumba alisema
Baraza Kuu la CUF, limesikitishwa kwa kiasi kikubwa na kitendo cha
kupitishwa na kutangazwa kwa katiba hiyo na Bunge la Katiba
lililoongozwa na Samuel Sitta akisema halikuzingatia sheria na taratibu
za mabunge ya Jumuiya ya Madola.
“Ni ukweli usiofichika kwamba mchakato mzima wa
kupitisha katiba haukuwa na mwafaka wa kisiasa, kanuni za uendeshaji wa
bunge hilo zilikiukwa na Katiba yote inayopendekezwa haikupigiwa kura ya
mwisho,” alisema
Profesa Lipumba alisema, katika vikao vya
ushauriano na viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD), Rais Jakaya Kikwete alikubaliana na viongozi
hao kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya, hususan kura ya maoni
uahirishwe mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
“Mwanasheria wa Serikali alitangaza kura ya maoni
Machi 30, Rais akiwa China alisema Aprili, yaani tayari tarehe
imeshatangazwa kabla hata ya daftari la wapigakura kukamilishwa,”
alisema.
Alisema baraza hilo pia limesikitishwa na
utaratibu unaofanywa na NEC juu ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la
Wapigakura akisema hadi sasa hatua za uandikishaji hazipo wazi na wadau
wengi hawana taarifa za kutosha juu ya nini kinaendelea.
Alisema takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2012,
zinaonyesha kuwa kuna vijana zaidi ya milioni 4.6 ambao watafikisha umri
wa kuwa wapigakura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 lakini bado
hawajapewa fursa ya kuandikishwa huku wananchi wengi wakiwa
wameshapoteza vitambulisho vya kupigia kura.
Alisema Juni, 19 mwaka huu, Nec, ilitangaza kufuta
matumizi ya vitambulisho vya kupigia kura vya sasa na badala yake
itatumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR), ikiwa ni
maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba Mwenyekiti wa
Nec, Jaji Damian Lubuva alinukuliwa akisema katika Kura ya Maoni ya
Katiba na Uchaguzi Mkuu, mpigakura atatumia kitambulisho kipya baada ya
kuandikishwa upya katika mfumo huo na si vinginevyo.
Pia alisema Baraza Kuu linalaani vitendo vya
uvunjifu wa haki za binadamu na sheria vinavyoendelea kufanywa na
Serikali kwa kulitumia Jeshi la Polisi.
Alitoa mfano wa masheikh waliokamatwa Zanzibar na
kuhamishiwa Dar es Salaam na kufunguliwa kesi akisema walijitokeza mbele
ya Mahakama na kusema waziwazi kwamba wamefanyiwa mateso na vitendo vya
kinyama lakini hakuna hatua zilizochukuliwa ikiwamo kupelekwa
hospitali.
Kadhalika, alisema baraza hilo limepokea kwa
mshangao taarifa za utoaji wa uraia unaofanywa na Serikali kipindi hiki
cha kuelekea kwenye uchaguzi. Alisema uamuzi wa kuwapa uraia wakimbizi
katika majimbo yanayoongozwa na wabunge wa vyama vya upinzani ni mbinu
ya kudhoofisha upinzani kwa kuwa wakimbizi wanaopewa uraia
wanahamasishwa kuwa wachague chama tawala.
Kuhusu ardhi alisema: “Pamoja na Tanzania kuwa na
ardhi ya kutosha kwa raia wake, ugawaji wa mapande makubwa ya ardhi kwa
wawekezaji yataleta mtafaruku wa uvunjifu wa amani na kuwafanya raia
wazawa kuwa maskini wa kudumu,’’ alisema Profesa Lipumba.
Kuhusu maradhi hatari ya ebola, Profesa Lipumba
alisema Baraza Kuu limeitaka Serikali kuwa makini ili usiingie nchini
akisema limesikitishwa na taarifa ya kwamba mpaka sasa nchi haina vifaa
vya kuthibitisha kuwapo kwa vimelea vya ebola.
Monday, 27 October 2014
KNCU wamlaumu mrajisi wa vyama
Moshi. Chama Kikuu cha Wakulima wa Kahawa Mkoa wa Kilimanjaro
(KNCU), kimemjia juu mrajisi wa vyama hivyo nchini kwa kile ilichodai
kukwamisha ustawi na maendeleo yake.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na
mwenyekiti wa KNCU, Maynard Swai wakati akisoma hotuba yake katika
mkutano mkuu maalumu ulioitishwa kwa shinikizo la mrajisi huyo, Dk Audax
Rutabanzibwa.
Licha ya kupokea lawama hizo, Dk Rutabanzibwa
aliyekuwa mwenyekiti katika mkutano huo hakuweza kujibu malalamiko
yaliyoelekezwa kwake na mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo aliwaachia wajumbe wa mkutano huo
kufanya uamuzi kwa njia ya kura kama bodi ya uongozi iendelee au ing’oke
ambapo kura 83 zilikataa na 68 zikitaka ing’oke.
Swai alisema ofisi ya mrajisi huyo imekuwa kikwazo cha maendeleo kwa KNCU .
“Mfano, shamba la Garagagua lilitakiwa kuuzwa Mei
2014, wajumbe mlisharidhia lakini kutokana na ukiritimba wa ofisi ya
mrajisi imekwama,” alisema Swai. Swai aliitaja mipango mingine kuwa ni
ujenzi wa hosteli ya kisasa na hoteli kwenye eneo la makao makuu ya
KNCU.
“Sina nia ya kuifundisha au kuikumbusha ofisi ya
Mrajisi wajibu wake kiutendaji lakini ina wajibu wa kushauri na
kusimamia ushirika ili uendelee kushamiri nchini kwa manufaa ya
wanachama,”alisema.
Lakini Swai alisema hata tume mbalimbali za
uchunguzi zilizotumwa KNCU katika kipindi kifupi cha miaka miwili na
Mrajisi, hazijawahi kutoa mrejesho wa matokeo ya uchunguzi huo.
“Kifungu 57(1) cha sheria namba 6 ya Ushirika ya
mwaka 2013 imeweka bayana kuwa ikiwa kuna uchunguzi au ukaguzi umefanywa
dhidi ya chama cha Ushirika, Mrajisi atapaswa kutoa matokeo ya
uchunguzi huo,”alisema Swai.
KNCU kimeshangazwa pia na hatua ya Mrajisi
kutoamini ukaguzi uliofanywa na COASCO ambacho ni chombo cha Serikali
kuhusu kiasi cha hasara ambayo KNCU ilipata wakati wa mdororo wa uchumi
duniani mwaka 2008.
Katika hesabu hizo, KNCU ilionyesha kupata hasara
ya zaidi ya Sh765 milioni wakati uhakiki uliofanywa na hazina ulionyesha
KNCU kilipata hasara ya Sh250 milioni.
“Mrajisi aliagiza kufuatiliwa kwa tofauti hii huku
akionesha kutokuwa na imani na hesabu zilizokaguliwa na COASCO jambo
ambalo linashangaza kama Serikali haiwezi kuamini kazi iliyofanywa na
chombo chake,” alisisitiza Swai.
Swai alisema tofauti hiyo ilifanyiwa kazi na KNCU na taarifa
kurejeshwa kwa Mrajisi lakini hawajaona mawasiliano yoyote yanayoonyesha
ufuatiliaji wa suala hilo hiyo inadhihirisha namna Mrajisi
alivyoshindwa kuitetea KNCU.
Mwenyekiti huyo alipigilia msumari zaidi pale
alipodai hata mkutano huo mkuu maalumu ulioitishwa na Mrajisi ni batili
na unakiuka kifungu namba 55(9) cha sheria ya Ushirika.
“Sheria iko wazi kuwa hesabu zikishawasilishwa na
kujadiliwa na kisha kupitishwa na mkutano mkuu, uamuzi wao (wajumbe)
kuhusiana na hesabu hizo unakuwa wa mwisho,”alisema Swai.
Swai alisema ilikuwa ni batili kisheria, kwa
Mrajisi kushinikiza kuitishwa kwa mkutano huo ili kujibu hoja za ukaguzi
ambazo alidai hazikupatiwa majibu ya kutosha na KNCU wakati wenye mali
walisharidhika na majibu hayo.
Subscribe to:
Comments (Atom)