Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa utafunaji wa Big G
zisizo na sukari unasaidia kuongeza usikivu na kumbukumbu,
kunakosababishwa na urahisishaji wa mtiririko wa damu kuelekea kwenye
ubongo.
Pengine mzazi wako, mwalimu amewahi kukukataza kutumia, kununua
kitu hiki, lakini imebainika Big G inaongeza kumbukumbu usikivu makini
na uchangamfu, kuimarisha afya ya kinywa.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa
utafunaji wa Big G zisizo na sukari unasaidia kuongeza usikivu na
kumbukumbu, kunakosababishwa na urahisishaji wa mtiririko wa damu
kuelekea kwenye ubongo.
Utafiti huo uliofanywa katika Chuo Kikuu cha
Cardiff nchini Uingereza na kuchapishwa mwezi uliopita, ulihusisha
kikundi cha watu ambao walitafuna Big G na wengine wasiotafuna kwa
kuwapa zoezi la kuweka kumbukumbu katika sauti kwa muda wa nusu saa.
Zoezi hilo lilikuwa ni la kusikiliza sauti ya orodha ya namba na kuzitaja kwa mfululizo.
Big G inatoa majibu sahihi
Waliotafuna Big G walitoa majibu sahihi tena kwa haraka zaidi tofauti na wenzao ambao hawakutafuna Big G.
Tafiti zilizotangulia zilionyesha kwamba utafunaji
wa Big-G una faida nyingi mwilini na Dk Chris Miles aliongoza utafiti
huo uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Cardiff.
“ Kutafuna Big-G kunawafanya watu wawe katika tahadhari zaidi.
“Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kitendo hicho
kinasaidia kwa kiasi kikubwa usafirishaji wa damu safi kwenda kwenye
ubongo,” anasema daktari huyo.
Lakini kama utawaambia watu watafune bila kuwapo
kwa Big G, hutapata matokeo yanayofanana. Hivyo inaonekana kuwa,
unahitaji kuwa na Big G ili kurahisisha utafunaji wako.
Madereva wa magari makubwa ya mizigo watakuwa
wamepata habari njema, kwani ikiwa kutafuna Big-G kunaongeza tahadhari
ni wazi kuwa inaweza kuwasaidia kuwa makini zaidi wawapo barabarani
hususani wakati wa usiku.
Hili halijajulikana bado, licha ya ukweli kuwa athari za utafunaji huo hutegemea na aina ya Big-G yenyewe.
Dk Miles anasema watu wengi hutafuna Big-G kwa lengo la kupata
harufu nzuri kinywani na sio kwa madhumuni ya kuongeza usikivu ama
tahadhari.
Utafiti uliofanywa na mchambuzi wa masuala ya
masoko anayefahamika kama Mintel, unaonyesha kwamba asilimia 92 ya
watumiaji wa Big-G wanafanya hivyo wakiwa na lengo la kutengeneza harufu
nzuri vinywani.
Wengu wanaofanya hivyo wanajiongezea hali ya
tahadhari bila ya wao kufahamu. Zipo faida nyingi za kiafya
zinazotokana na utafunaji wa Big-G.
Mapitio mengine yaliyofanywa na watalaam kutoka
katika Chuo Kikuu hicho cha Cardiff mwaka 2011, yalitoa ushahidi kuwa
utafunaji wa Big-G unasaidia sana katika kupunguza msongo wa mawazo.
Utafiti wa Cardiff haukuangalia athari
zinazosababishwa na utafunaji wa Big-G kiafya, lakini utafiti wa Mintel
uliofanyika Disemba mwaka jana ulionyesha kuwa ni watu sita kati ya kumi
wanaotafuna Big-G huamini kuwa zinaweza kuwasaidia kuboresha meno yao.
Ukweli ni kwamba watu hao wako sahihi, hiyo ni kwa
mujibu wa Dk Nigel Carter, Mkuu Taasisi ya Dental Health Foundation ya
nchini Uingereza.
Pamoja na mapitio yaliyobainishwa na Jarida la
British Jounal la Uingereza mwaka 2011, kuna athari iliyojificha katika
bidhaa zenye sukari inayokinzana na zile zisizo na sukari.
Kwa kawaida Big –G zenye sukari zinaongeza ‘asidi’ mdomoni inayoweza kuharibu meno kwa kuathiri mizizi yake.
“Hii ni hatari, nafikiri ulaji wa aina hizo za Big-G ni hatari sana kwa afya ya meno yao,” anasema Carter.
Kuna kiwango kidogo sana cha Big-G zisizo na
sukari zenye ladha inayoweza kuzalisha ‘asidi’ mdomoni. Kama athari zipo
ni kwa kiwango kidogo sana.
Kama ‘asidi’ hiyo itazalishwa kwa kiasi kidogo
sana nadhani itakuwa ni rahisi kupotea tofauti na zile za kawaida
zilizoongezewa sukari.
Athari kubwa ya kutafuna Big-G, ni kusaidia kuongeza mate mdomoni anasema Dk Carter.
Mate yanasaidia utaratibu wa kinga asilia unaojumuisha chumvi
iliyomo ndani yake kwa kuongeza ama kupunguza madini kwenye meno ambayo
yanasababishwa na vyakula vyenye asidi inayotokana na sukari.
Kadri jinsi chumvi inavyokuwa nyingi kwenye mate, ndivyo utaratibu huo unavyokuwa rahisi zaidi.
Big G inalinda meno
Dk Carter anabainisha kwamba kwenye Big-G zenye
sukari, sukari inachanganywa haraka na mate hayo na kuondoa na uharibifu
wa meno.
Pamoja na yote hayo BDHF inasisitiza matumizi ya Big-G zisizo na sukari kwamba zina faida zaidi.
Utumiaji wa vyakula visivyo na sukari ni muhimu
sana katika kulinda fizi. Je, matumizi hayo yanahesabiwa kama kitendo
chanya kwa afya ya fizi na kinywa kwa ujumla?
“Ni kweli kabisa”. Hivyo ni vizuri kutosafisha
meno baada ya kula na badala watu wanapaswa kutafuna Big G kwa muda wa
dakika 10 hadi 20. Hii itasaidia kuongeza mate mdomoni na pia kuboresha
meno yako kwa kuyaondoa katika hatari ya kuoza, anahitimisha Daktari
huyo.





