Tuesday, 10 September 2013

Simu za mikononi jamani!!!!!!!

 iPhone 5 - 16 GB

SIMU za mkononi ni muhimu katika maisha yetu, kwa sababu ni kiunganishi cha mawasiliano ya wanadamu walio maeneo tofauti.
Matumizi ya simu yana faida nyingi katika maisha ya sasa, hasa upande wa kiuchumi na kuwaweka watu karibu duniani kote.
Lakini mbali na faida, lengo la kuandika mtazamo huu ni kuhusu wale watumiaji wa simu hizi za mkononi ambao hawajua matumizi yake sahihi.
Wako watu ambao hujisikia kama burudani au sifa wanapokuwa wanazungumza na simu, tena kwa muda mrefu. Wakati mwingine hujionesha kwa watu walioko karibu nao kwa namna wanavyojua kutumia simu.
Kwa mtazamo wangu, usiyafanye matumizi ya simu kuwa starehe au maonesho kwa watu, kumbuka bila kujijua maneno yako wakati mwingine yanaweza kuwa si mazuri kwenye masikio ya watu, jaribu kutumia simu yako kwa faida yako.
Usiwe kikwazo kwa namna yoyote, hasa sehemu za huduma za kijamii, kwa sababu siku hizi hata heshima kwa watu wanaotakiwa kuhudumiwa imepungua, kwani kuna baadhi ya wahudumu na hata wakurugenzi wa ofisi mbalimbali hujisahau kuhudumia wateja wao linapokuja suala la kuzungumza na simu.
Kwa mfano, katika zahanati au hospitali wahuduma wengi hujikuta wakizungumza na simu badala ya kuhudumia wagonjwa.
Hilo hutokea baada ya kupigiwa simu au kupiga simu na kuanza maongezi, tena ya muda mrefu, huku wakisubiriwa, ukiyasikiliza maongezi yao yanakuwa si ya heshima, hayafai hata kusikilizwa kwani hayana maadili mazuri, nyingine ni ahadi za mapenzi na ulevi.
Wanazungumza maneno yasiyofaa kwa jamii inayowazunguka, ila kwa kuwa una shida au mgonjwa, huna la kufanya, ni lazima kuyasikiliza, ukitoka utawahiwa na wenzako, hii ni kwa watu wa jinsia zote, iwe wanawake au wanaume, hasa vijana.
Hizi simu ndizo zinazovunja hata ndoa kwa wanandoa, kupoteza maadili mema na hata kuondoa ufanisi wa kazi maofisini, hivyo kufanya uchumi wa baadhi ya miradi kushuka na kuharibu uchumi wa taifa.
Mwandishi wa kitabu cha ‘Madhara na Faida ya Simu ya Mkononi’, Sweetbirth Bruno, anasema: “Licha ya kero kwa wengine imefahamika kwamba baadhi ya watoto wa shule za msingi na sekondari hushindwa kufanya vizuri wawapo shuleni, hilo ni pamoja na kukesha usiku kucha waki ‘chati’ na simu, tena wakizungumzia maneno ambayo hayana msingi na kusababisha kuvuruga ufahamu wao na kupoteza uwezo wa kusoma, hatimaye kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata alama za daraja la nne au sifuri na kuongeza idadi ya wajinga nchini.”
Rai yangu kwa idara na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, ni kuliangalia hilo, kwa sababu matumizi haya ya simu kwa wanafunzi yamezidi hadi kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho, hasa kidato cha nne na sita.
Nawashauri wanafunzi kuachana na matumizi ya simu na waweke bidii katika masomo yao kwa sababu wanaweza kujisababishia kushuka kimasomo na kulisababishia taifa kukosa wasomi, chanzo kikiwa ni matumizi mabaya ya simu kama kuingia kwenye mitandao mbalimbali ya anasa badala ya kusoma masomo ya darasani.

Hivi ndivyo tutakavyoinua elimu ya msingi na sekondari nchini

Hivi karibuni Serikali ilizindua mpango ujulikanao kwa jina la  ‘’Matokeo Makubwa Sasa’’, uliohusu sekta mbalimbali zenye changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.
Sekta zilizoainishwa chini ya mpango huo ni elimu, miundombinu, madini na nishati, uchumi na fedha pamoja na sekta ya maji.
Katika sekta ya elimu, wataalamu kutoka ndani na nje ya vyombo vya Serikali vinavyoshughulikia elimu, walikutana na kuandaa mikakati tisa ya kunusuru sekta ya elimu nchini, hasa elimu ya msingi na ile ya sekondari.
Pamoja na mambo mengine, mikakati hiyo inalenga kwa kiwango kikubwa kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa  ngazi hizo muhimu katika mfumo wa elimu nchini.
Makala haya yanadurusu kwa kina maelezo ya mwongozo wa namna mikakati hiyo itakavyotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya mpango.
Ujenzi wa miundombinu muhimu shuleni
Shughuli za ujenzi zilizobainishwa kutekelezwa katika mpango huu ni pamoja na ujenzi, ukarabati na  ukamilishaji majengo kama  madarasa, maabara, vyoo, utoaji wa maji safi na kuweka umeme kupitia gridi ya Taifa au umeme wa mwanga wa jua.
Serikali imepanga kuwezesha utekelezaji wa haraka wa mradi wa awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II) katika ujenzi wa miundombinu ya msingi kwa shule 1,200 ifikapo mwaka 2014.
Serikali imepanga kukamilisha ujenzi wa shule hizi katika awamu tatu: awamu ya kwanza itakamilika Septemba 2013 ambapo shule za sekondari 264 zitajengwa.
Awamu ya pili itakamilika Machi 2014 ambapo shule za sekondari 528 zitahusika na  awamu ya tatu itakamilika Septemba 2014 ambapo shule za sekondari 408 zitajengwa au kukarabatiwa.
Mgawanyo wa shule kimkoa katika awamu kwanza unahusisha Arusha (14), Dodoma (12), Dar es Salaam (6), Geita (6), Iringa (8), Kagera (14), Katavi (4), Kigoma (8), Kilimanjaro (14), Lindi (12), Manyara (12), Mara (12) Mbeya (16), Morogoro (12),  Mtwara(12), Mwanza (11), Njombe (8), Pwani (14), Rukwa (6) Ruvuma (10), Shinyanga (8), Simiyu (7), Singida (8), Tabora (12)  na Tanga (18).
Ruzuku ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia:
Katika kutekeleza mpango, Serikali inatoa ruzuku ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia  kwa kuzipa shule uwezo wa kununua vitabu na vifaa vingine na kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule.
Kiwango cha ruzuku kilicholengwa kwa mwaka ni Sh 25,000 kwa kila mwanafunzi wa elimu ya sekondari na shilingi 10,000 kwa mwanafunzi wa elimu ya msingi.
Aidha, Serikali imepanga kuinua ufaulu katika shule kwa kuboresha upatikanaji  wa vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni, na kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinafika shuleni na kutumika.
Upangaji wa shule kuzingatia matokeo
Serikali imeanza kuzipanga shule kitaifa kwa kuzingatia matokeo, kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na ushiriki wa jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora. Uwajibikaji ni kati ya changamoto kubwa zinazoukabili mfumo wa elimu kwa sasa.
Shule zitapangwa kwa ubora wa matokeo katika mitihani na kisha kutangazwa kwa umma, ili iwe chachu ya kuandaa jamii kuwajibika na kuleta uelewa mpana.
Faida za upangaji wa shule ni pamoja na kuziamsha shule kufanya vizuri, itasaidia shule kujitathmini, itawahamasisha walimu na wanafunzi kufanya kazi kwa bidii na kuzitambua shule zilizofanya vizuri zaidi.
Shule zitakazofanya vibaya zitafuatiliwa na kupewa msaada kulingana na upungufu uliojitokeza. Shule zitakazoonyesha maendeleo chanya kwa asilimia 10 ukilinganisha na mwaka uliopita zitapewa tuzo.
Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi. Tuzo hii itaanzia katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na sekondari.
Aidha, tuzo za fedha taslimu na nyinginezo zitatolewa katika makundi mawili ya shule,  ambayo ni shule zilizoonyesha maendeleo ya juu na shule zilizofanya vizuri. Nafasi za ushindi zitagawanywa katika mikoa yote ili kupata msambao wa utoaji wa tuzo hizo.
Pia shule zitapanga utaratibu wa kugawana tuzo kwa uwazi na ushirikishwaji. Tuzo zitakazotolewa kuanzia mwaka huu zitajumuisha fedha, vyeti, vifaa mbalimbali, ngao na vikombe.
Motisha kwa walimu 

Katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji, Serikali imeandaa mkakati wa kuwatambua  walimu wanaofanya kazi  vizuri kwa kuwapa tuzo, kuhakikisha madeni yote ya walimu yanalipwa kwa wakati na kuandaa mpango wa motisha kwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo yenye mazingira magumu.
Motisha kwa walimu ni muhimu kwa kuwa kazi ya ualimu ni kazi yenye  jukumu la kumwandaa Mtanzania atakayesheheni maarifa, ujuzi na stadi za kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
 Aidha, walimu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo madai mbalimbali kutoshughulikiwa kwa , hali inayosababisha walimu wengi kukata tamaa.
Katika kutekeleza mkakati huu wa motisha kwa walimu, kuanzia Julai 2011 hadi sasa Serikali imelipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya walimu 31,779 yenye thamani ya  Sh 28.5 bilioni, ambapo Sh 28,544,743,604.06 zimelipwa kupitia mishahara ya watumishi husika.
Pia kutoka  Januari 2012 hadi Juni, 2013, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imelipa madai yasiyo ya mishahara ya walimu 2,825 yenye jumla ya Sh.2.6 bilioni kati ya shilingi 3.3 bilioni ya fedha kutoka Hazina. Lakini pia Serikali kwa sasa inaendelea na majadiliano na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuhusu kuboresha zaidi maslahi ya walimu.
Kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi
Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ujifunzaji na ufundishaji imeanzishwa ili kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani ambao husababisha wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika ujifunzaji kushindwa kusaidiwa.
 Pia kuna changamoto ya baadhi ya walimu kutokuwa na  nyenzo muhimu za kufundisha kwa ufanisi, kama vile kushindwa kuandaa maandalio ya somo na  kutokuwepo kwa utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi katika maeneo yenye changamoto za uelewa kwa baadhi ya shule.
Katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika ufundishaji na ujifunzaji, Serikali itaendesha mitihani ya majaribio kwa ajili ya kuwabaini wanafunzi wenye mahitaji ya ziada katika kujifunza, kutoa mafunzo kwa walimu kwa ajili ya utekelezaji na kutoa mafunzo rekebishi kwa wanafunzi kwa kuzingatia maeneo yenye changamoto za kuelewa.
Programu hii inawalenga walimu wa masomo ya Bayolojia, Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika ngazi ya sekondari na walimu  Hisabati, Kiswahili na Kiingereza kutoka  shule za msingi. Walengwa wengine ni wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha nne kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Friday, 6 September 2013

Majambazi yatingisha Dar, yapora maduka 11

Kundi la watu  wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki, wamefunga mtaa na kupora fedha na simu za kiganjani katika maduka 11 eneo la Mvumoni Madale, kata ya Wazo na Tegeta Kibaoni, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo, wakizungumza jana na NIPASHE, walisema tukio hilo lilitokea juzi Jumapili, majira ya saa 1:30 usiku.
Hata hivyo, kumekuwa na taarifa za kukanganya kati ya wananchi walioathirika kutokana na mkasa huo ambao wanadai wameporwa simu na fedha kwa viwango tofauti katika maduka 11 huku Jeshi la Polisi likisema kuwa maduka matatu pekee ndiyo yamevamiwa na kuporwa kiasi cha Sh. 300,000.

Katika eneo la Mivumoni Madale kwenye maduka yanayofahamika kama maduka 11, majambazi hao walivamia na kupora kwenye maduka sita.

Neema Charles, muuzaji wa Super Market, alisema akiwa anahudumia wateja alishangaa baada ya watu watatu kuingia na kumrudisha mteja aliyekuwa anatoka ndani na kutoa amri ya watu wote kulala chini na kutoa fedha na simu.

“Kati ya watu watatu walioingia ndani mmoja alivaa kininja akaficha sura, alikuwa na bunduki aliyotumia kupiga watu, walipora simu, pochi, fedha za mauzo na fedha zetu binafsi…nilikuwa na Sh. 250,000 kwenye pochi zimekwenda,” alisema.

Alisema walipekua kila mahali na kupora fedha, simu na pochi huku wakiwatolea lugha ya matusi na kuwataka kila mmoja kunyamaza kimya.

Alisema wakati wanaendelea na kupekua, aliwaangalia na ndipo alichomwa na kitu chenye ncha kali karibu na bega la mkono wa kulia na baada ya kupora walikwenda kwenye maduka mengine na tukio  hilo lililochukua dakika 20.

Poni Abdalah, mmiliki wa saluni ya kike, alisema alikuwa anahudumia wateja sita na watoto wanne, mara aliingia mtu mmoja na kuwataka kukaa kimya na kutotoka nje.

“Wakati anatoa amri hiyo mmoja wa wateja alikuwa na mwanaye aliyetoka nje akatoka kumfuata, alivutwa na kusukumwa ndani na tulikaa kimya baada ya kujua tumevamiwa,” alisema.

Alisema jirani yake kuna maduka ya M -pesa na Tigo-pesa nayo yaliporwa kiasi cha Sh. milioni 1.5, na kuwafungia ndani na kuondoka na funguo. Alifafanua kuwa baada ya majambazi kuondoka iliwabidi wavunje mlango ili kumtoa muuzaji aliyefungiwa ndani. 

“Baada ya kuona bibi aliyekuwa mteja kwenye duka langu kaporwa simu, nilizima taa ya dukani na kukaa kimya ikawa pona yangu, baada ya dakika 20 nikatoka nje nikakutana na dada mmoja ambaye alikuwa mteja kwenye duka la dawa amenyang’anywa funguo wa gari yake na watu hao,” alisema Amos Joseph.

Katika eneo la Tegeta, mtaa wa Tegeta Ndevu, Mariamu William, alisema majambazi hayo yalifika dukani humo kama wateja na kumtaka kaka yake, Emmanuel William, muuzaji kutoa fedha huku wakiwa wamemshikia bunduki.

“Kabla ya kuamuru wenye maduka kuwapa fedha walipiga risasi mbili hewani, alivyokuwa anachelewa kuwapa walichotaka walimpiga na kitako cha bunduki,” alisema.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kusema kuwa maduka yaliyoporwa ni matatu katika eneo la Madale mawili na moja ni eneo la Tegeta Kibaoni ambayo yaliporwa kiasi cha Sh. 300,000.

Wambura alisema hana taarifa za kuporwa maduka 11 na kuongeza kuwa polisi wanaendelea kuwasaka majambazi hayo.

MWANAMKE ABAMBWA NA SARE ZA JESHI
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limemkamata  mwanamke aliyefahamika kwa jina la Saida Mohamed (30),  mkazi wa Mwasonga Kigamboni akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kamanda wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema jana kuwa mwanamke huyo alikamatwa juzi saa 4:00 asubuhi eneo la Mwasonga Kigamboni, wilayani Temeke.

Kova alisema, mwanamke huyo alikuwa na sare za jeshi hilo ambazo ni suruali saba za kombati, mashati saba ya kombati, kofia 10 za kombati, mashati mawili mepesi, fulana mbili, kofia aina ya bereti moja, viatu jozi tatu, ponjoo moja, koti moja, begi moja la kuwekea nguo za kipolisi pamoja na mikanda miwili ya kijeshi.

Aidha, Kamanda Kova alisema  mwanamke huyo anaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano.

Katika tukio lingine, watu wawili  wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kukutwa  na mihuri  27 na  nyaraka mbalimbali za serikali pamoja na za taasisi binafsi wakizitumia kufanyia utapeli kwa wananchi.

Kova aliwataja watu hao kuwa ni Sadraki Mwangwi (27), mkazi wa Mbagala Sabasaba na Samuel Mwangwi (38), mkazi wa Kimara Baruti.

Alisema, waliwakamata watu hao wakiwa na nyaraka hizo wakizitumia kuwatapeli wananchi wa sehemu mbalimbali jijini wakiwa wanakata risiti za serikali kama vile bima za magari, risiti za benki, manispaa na halimashauri. Aliongeza kuwa watu hao walikuwa kama mawakala wa kutoa risiti ambazo wananchi walizihitaji kwa bei yoyote ile.

Kova alisema katika msako huo walifanikiwa kuwakamata watu 120 kwa makosa mbalimbali na kusema msako huo ni endelevu.

Tunataka Katiba ya mwafaka, siyo jeuri na kiburi

Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa siku mbili mfululizo umekuwa shubiri bungeni.
Juzi wabunge wote wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walitoka bungeni kuonyesha kutokufurahishwa kwao na uamuzi wa kukataliwa kwa pendekezo la kuuondoa kwanza bungeni ili kutoa fursa kwa wadau wa Zanzibar kutoa maoni yao.

Jana ilikuwa ni tafrani tena baada ya pendekezo la kutaka kuondolewa bungeni kwa muswada huo kukataliwa baada ya kupigwa kura hali iliyoishia kiti cha spika kuamuru Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, Freeman Mbowe, kutoka nje kwa madai kuwa alikataa kutii kiti.

Hali iliyoonekana bungeni haikuwa nzuri kwa vigezo vyovyote vile.

Muswada huu umekuwa na mwelekeo unaovunja maelewano, mshikamano na kuna kila dalili kwamba wabunge wa kambi ya upinzani wanaamini kwamba serikali inatumia nguvu zake hasa kwa kujiegemeza kwenye wingi wa wabunge wake kuupitisha muswada huo.

Tangu jana asubuhi kulikuwa na dalili kwamba baadhi ya wabunge hawakuwa radhi muswada huo ujadiliwe katika mkutano wa sasa na badala yake walikuwa wanaomba uondolewe bungeni ili kufanya mashauriano.

Swali aliloulizwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwake, kama hakuona ni busara kwa serikali kuondoa muswada huo bungeni, ilikuwa ni kielelezo kingine cha kuonyesha kwamba bado kulikuwa na mwako mkubwa wa kisiasa kwamba mambo hayakuwa yamekaa sawa juu ya muswada huo.

Kimsingi muswada huu ni sehemu ya mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo inatarajiwa kwamba ifikapo mwaka 2015 itakuwa tayari ili itumike kwenye uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.

Hadi sasa Tume ya Katiba imekwisha kupokea maoni ya wananchi juu ya katiba wanayoitaka, imetayarisha rasimu ya katiba, imeunda mabaraza ya katiba, na yatari mjadala wa mabaraza umemalizika juu ya rasimu husika na mapendekezo yamewasilishwa kwa Tume.

Hata hivyo, pamoja na hatua zozote zilizopigwa hadi sasa juu ya mchakato wa katiba mpya, safari bado ni ndefu na ngumu. Ugumu wa safari hii unajikita kwenye jambo muhimu kubwa, maelewano ya kisiasa.

Kwamba ni kwa kiwango gani wadau wote kwa ujumla wao, iwe ndani ya bunge, nje ya bunge, ndani ya  baraza la wawakilishi, kwenye vyama vya hisari na kila mwenye kuitakia nchi hii mema na anayeweza kuwa na maoni juu ya  mchakato huu, wamehusika katika kuandaa sheria ambayo mwisho wa siku itawapatia katiba nzuri ambayo ni sheria mama.

Kwa upeo wetu, kazi ya kutunga katiba kwa mataifa mengi imekuwa ya mgogoro mkubwa sana. Yapo mataifa mengi ya Afrika ambayo yaliishia kusambaratishana kwa sababu tu ya kushindwa kuendesha vema mchakato wa katiba.

Kwa Tanzania kumekuwa na mwanzo mzuri. Awali kulikuwa na kishindo kilichosababisha rasimu ya awali ya sheria ya kuundwa kwa Tume ya Katiba kuamsha taharuki kubwa. Hali ilitulizwa kwa mazungumzo na kuingiza ndani ya muswada yale yote yaliodhaniwa kuwa na umuhimu wa kuzingatia maslahi mapana ya kitaifa.

Lakini pia kuna wakati Rais Jakaya Kikwete kwa hekima zake, aliamua kusikiliza kilio cha baadhi ya vyama vya siasa hata pale sheria ilipopitishwa kwa msukumo tu wa wingi wa wabunge wa chama tawala, bila kuzingatia maslahi mapana ya kitaifa.

Rais aliita makundi ya vyama vya siasa Ikulu na kupokea mawazo na mapendekezo yao ambayo yalizaa marekebisho ya sheria ya kuundwa kwa Tume ya Marekebisho ya Katiba.

Umauzi wa Rais Kikwete ulifikiwa bila kujali kwamba waliokuwa wamepitisha muswada husika walikuwa ni wabunge wa chama chake tena wakiwa wengi ndani ya bunge.

Hakung’ng’ana tu na hoja ya wingi wa wabunge wake. Hakubweteka tu kwa kuwa ana wabunge zaidi ya theluthi mbili wanaotokana na chama chake, ila  alisukumbwa na  hoja ya kutaka kuona makubaliano ya pamoja yanafikiwa katika machakato wa katiba mpya.

Kila sauti na hoja yenye nguvu inasikika, inazingatiwa kwa kuwa katiba ni maafikiano ya kitaifa kuliko dhana tu ya wengi wape.

Ni kwa msingi huu sisi tunasema kuwa mijadala ya kisiasa katika kutengeneza sheria katika mchakato mzima kuelekea kupatikana kwa katiba mpya, ni lazima dhana ya makubaliano ya kitaifa itawale akili za wale wote wanaodhani kwamba leo wako salama sana kwa sababu tu wanatokana na upande wa chama kinachounda serikali.

Ni vema ikaeleweka kwamba katiba ni zaidi ya vyama vya siasa. Ni zaidi ya uanachama wa chama cha siasa; ni misingi wa haki, uhuru na wajibu katika taifa.

Wapo wabunge wengi ndani ya bunge la sasa ambao awali hawakuwa wanachama wa vyama ambavyo vimewapa uwakilishi. Lakini, katiba ni ile ile, wakiwa chama tawala, wakiwa upinzani na vinginevyo.

Tunaasa kwamba hasira, jeuri, kiburi na unazi havitatupa katiba mpya inayokidhi vizazi vya sasa ni vijavyo. Tuwe makini.
CHANZO: NIPASHE

Tusipokuwa makini tofauti hizi zitaiua EAC


Sasa ni bayana kwamba tofauti zilizopo miongoni mwa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zimeanza kukuzwa, huku wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wakionya kwamba tofauti hizo zisipotatuliwa haraka jumuiya hiyo itasambaratika na kubaki historia.

Sote tunatambua kwamba tofauti hizo zilianza baada ya Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kumshauri Rais Paul Kagame kuzungumza na FDLR ambao ni waasi wa nchi hiyo wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Rais Kikwete pia alimshauri Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuzungumza na waasi wa nchi hiyo ADF, akisema hatua hiyo italeta amani ya kudumu katika ukanda mzima wa Maziwa Makuu.
Kwa bahati mbaya Rais Kagame alikasirishwa na ushauri huo. Alisema ushauri wa Rais Kikwete yalikuwa matusi kwa Rwanda na kusema nchi hiyo haiwezi kamwe kuzungumza na watu waliofanya mauaji ya kimbari.
Kiongozi huyo alitoa kauli zisizokubalika kidiplomasia dhidi ya Rais Kikwete ambaye aliamua kuzipuuza, ingawa baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda vimeendeleza vita ya maneno.
Tunashawishika kusema kwamba Rais Museveni kwa kukaa kimya aliukubali ushauri wa Rais Kikwete au alifanya hivyo tu ili kuepusha kukua kwa mgogoro huo. Wapo wanaosema Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa nia njema, lakini wakosoaji wake wanasema pamoja na nia yake hiyo kuwa ya dhati kabisa, angeutoa faragha kwa Rais Kagame au katika vikao mwafaka vya EAC badala ya kufanya hivyo katika kikao cha Umoja wa Afrika (AU), kilichofanyika Addis Ababa, wakisema huko hapakuwa pahala pake.
Hilo hakika ndilo chimbuko la mgogoro tunaoushuhudia hivi sasa ambao tunadhani umekuzwa kupita kiasi tukitilia maanani matukio ambayo yamekuwa yakitokea katika siku za hivi karibuni. Hata hivyo, zipo tetesi pia kwamba Rwanda haikufurahishwa na kitendo cha Tanzania kukubali kupeleka wanajeshi wake nchini DRC kuungana na kikosi cha Umoja wa Mataifa (UN), kulinda amani nchini humo kwa lengo la kuwanyang’anya silaha waasi wa M23 wenye asili ya Rwanda.
Tumelazimika kuandika hayo yote ili kuweka kumbukumbu sahihi za mtiririko wa mgogoro huo ambao baadhi ya watu walidhani ungeziingiza nchi hizo mbili jirani katika vita.
Hivi sasa umefanyika mkakati wa kuitenga Tanzania kiuchumi ambapo juzi marais wa Kenya, Uganda na Rwanda waliungana kuzindua upanuzi wa Bandari ya Mombasa inayokusudiwa kutumiwa na nchi hizo kupakua na kusafirisha mizigo. Mkakati huo ulizinduliwa na marais wa nchi hizo mjini Entebbe hivi karibuni ambapo Tanzania haikualikwa kama ambavyo haikualikwa juzi wakati wa uzinduzi huo.
Tofauti zinazoendelea kujitokeza hakika sio ishara njema kwa mustakabali wa EAC. Siku chache zilizopita uliibuka mzozo miongoni mwa wabunge wa EAC jijini Arusha ambapo wabunge wa Uganda, Kenya na Rwanda walisababisha kikao cha Bunge kuvunjika ili kumshinikiza Spika aruhusu kujadiliwa kwa hoja ya vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama badala ya Tanzania pekee.
Wabunge wa Tanzania nao walifanya hivyo siku iliyofuata wakipinga hatua ya wabunge hao kutaka kumshinikiza Spika kukubali hoja hiyo kinyume na Kanuni za Bunge.
Kwa mwenendo huo sisi tunadhani kuna ajenda ya siri iliyofichwa chini ya zulia. EAC inachungulia kifo. Zinahitajika busara kuinusuru. Vinginevyo, historia ya EAC ya mwaka 1977 itajirudia.

Ghasia kubwa zalipuka kupinga muswada

Dodoma. Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.
Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku akiwa hana viatu.
Pamoja na tafrani hiyo, Ndugai alisema wakati akihitimisha kikao cha Bunge kipindi cha asubuhi kuwa amewasamehe wabunge wote waliohusika na kosa hilo la utovu wa nidhamu na kuwaruhusu kurejea kipindi cha jioni kuendelea na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.
Msimamo huo ulitolewa na Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mbunge wa CUF, Habib Mnyaa.
Mbowe alisema wameamua kususia majadiliano hayo kuonyesha msimamo wao wa kupinga kupitisha mambo yasiyo na masilahi kwa nchi.
“Hatuko tayari kushiriki katika uchakachuaji wa Katiba... Matumizi ya nguvu ya polisi kamwe hayatatupatia Katiba nzuri,” alisema. Alisema kambi rasmi ya upinzani inalaani vikali kitendo cha Ndugai kuruhusu Bunge kunajisiwa kwa kuruhusu polisi kuingia ndani kinyume na kanuni.
Mnyaa alisema kitendo cha wadau wa Zanzibar kutoshirikishwa katika kutoa maoni yao katika muswada huo wa marekebisho ni dharau kubwa.
Mbatia alisema Tanzania haiwezi kuingia Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kutumia Katiba ya sasa kwa sababu tayari kuna mgongano wa kikatiba kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutoa ushahidi kama Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kulingana na mapendekezo ya taasisi zao.Kuanza kwa tafrani
Sakata hilo lilianza saa 6:45 mchana muda mfupi baada ya kukamilika kwa kura kuamua kama Bunge liahirishwe au la kutokana na hoja iliyotolewa na Mbunge wa Mkoani (CUF), Ali Hamisi Seif (CUF). Waliotaka liahirishwe walipata kura 59 na waliokataa 159.
Baada ya Ndugai kutangaza matokeo hayo na kutaka shughuli za Bunge ziendelee, Mbowe aliposimama na kusema ana hoja Naibu Spika alimwamuru akae chini.
Baada ya Mbowe kusisitiza ana hoja na kumwomba Spika amsikilize ndipo Ndugai alipomwamuru atoke nje na alipokaidi alisema:” Naomba askari wote waliopo katika mazingira haya (ya Bunge) waingie ndani ya ukumbi wa Bunge”.
Baada ya kitambo kifupi, Mbowe akiwa bado amesimama alitoa maagizo atolewe nje: “Kiongozi wa upinzani atolewe nje.”
Polisi waliingia ndani ya Ukumbi wa Bunge lakini Wabunge wa Kambi ya Upinzani kwa umoja wao, walimzinga Mbowe asifikiwe na askari hao.
Baada ya kuona polisi wanaelekea kushindwa, Ndugai alitoa maagizo mengine: “Askari hamjaletwa humu ndani kufanya majadiliano mnatakiwa kuhakikisha kiongozi wa upinzani anatolewa nje”.
Alisema yeye ndiye anayeendesha kikao hicho hivyo lazima Mbowe atolewe nje.
Hapo ndipo wabunge hao wa upinzani walipoanza kuimba: “Hatutaki kuburuzwa hatutaki kuburuzwa… hatutaki kuonewa,” huku wakiendelea kumzinga Mbowe.
“Askari wote mliopo humu ndani naomba mnisikilize… Sasa naagiza kwa mara ya mwisho... nasema kiongozi wa upinzani atolewe nje.”
Ngumi zarushwa
Baada ya kauli hiyo ya Ndugai, ndipo polisi walipotumia nguvu hasa kwa Mbilinyi na Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), Silvester Kasulumbai.
Katika patashika hiyo, inadaiwa kwamba Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alipigwa ngumi ambayo ilimfanya apepesuke hadi sakafuni.
Kilichomponza Mbilinyi ni hatua yake ya kusogelea Siwa. Polisi waliokuwa karibu, walimbeba juujuu hadi nje ya ukumbi.
Wakati akitolewa nje ya ukumbi, alijaribu kujizuia kwa kushika kipaza sauti kinachotumiwa na upande wa upinzani hadi kikang’oka.
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Mozza Abeid, alivuliwa hijabu katika vurumai hizo wakati polisi walipokuwa wakitumia nguvu ili kumfikia Mbowe.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mbowe aliamua kutoka nje huku akisindikizwa na polisi pamoja na wabunge wa vyama hivyo na alipofika nje ya ukumbi alipokewa na polisi wa kawaida waliomweka chini ya ulinzi kabla ya kumwachia baada ya ombi la Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini.
Kutokana na hali ya mambo kuwa tete, askari wa Bunge waliwaondoa wageni waliokuwa wamekaa katika kumbi za wageni wakiwamo wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari huku baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa na simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (Ipad) wakichukua picha za tukio zima.
Inadaiwa kwamba baada ya kutoka nje ya ukumbi, Mbilinyi alimtwanga ngumi mmoja wa askari waliomtoa kwa nguvu kabla ya kuamuliwa na wabunge na polisi.
Wakati wote huo, wafanyakazi wa Bunge na wageni walionekana wakiwa wamejikusanya katika makundi wakitafakari na kushangaa yaliyokuwa yakitokea.
 Balaa lilivyoanza
Akitumia Kanuni ya 69(1), Mbunge wa Mkoani (CUF), Ali Hamisi Seif, alitaka kuahirishwa kwa mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 kutokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Bunge ilipaswa kukusanya maoni ya wadau mbalimbali nchini ikiwamo upande wa Zanzibar jambo ambalo halikufanyika wakati wa maandalizi ya muswada huo.
“Ilipaswa sheria hii inapotaka kufanyiwa marekebisho iende tena kulekule Zanzibar lakini jambo la kusikitisha kamati inayohusika na masuala ya Katiba haikwenda. Mimi ni mjumbe wa kamati na tuliitwa Dar lakini ratiba waliyotupa haikuonyesha kama tungekwenda Zanzibar,” alisema. Mkosamali naye aliomba mwongozo kwa Spika, akisema kwa kuzingatia matakwa ya kiapo cha Spika au Naibu alipaswa kuendesha Bunge kwa haki bila upendeleo.
“Kanuni inasema Spika ama Naibu Spika ama Mwenyekiti ataendesha shughuli za Bunge kwa haki, uadilifu, bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba ya nchi,” alisema na kuongeza: “Kwa kuwa sisi tumekuweka hapo ili uendeshe Bunge kwa uadilifu, usiburuzwe na chama chako na uzingatie miongozo yote kwa wakati. Kwa nini usitumie mamlaka yako kuondoa muswada huu”?
Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenister Mhagama aliomba mwongozo kwamba kwa kuwa bado kuna malalamiko basi waipe Serikali nafasi ya kuthibitisha kwamba majadiliano ya kamati yalikamilika.
Lissu katika kuomba mwongozo wake, alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, Pindi Chana alilidanganya Bunge alipowasilisha maoni ya kamati kwamba wadau wa muswada huo walishirikishwa jambo ambalo alisema si kweli.
Lissu alisema hakuna Mzanzibari aliyefika mbele ya kamati hiyo kutoa maoni kuhusu muswada wowote.
Hata hivyo, Chana alijibu akisema wadau wa Zanzibar walitoa maoni yao na kukabidhi nyaraka mbalimbali kwa Spika kuthibitisha kauli yake hiyo. Alivitaja vyama vya Jahazi Asilia na ADC kuwa vilihojiwa.
Kwa upande wake, Lukuvi alimshambulia Lissu kwa kauli yake ya juzi kwamba uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete ulikuwa na walakini. “Lissu alisema jana (juzi) kwamba wapo wadau ambao walisema ijapokuwa waliandikiwa barua ya kuwasilisha majina matatu kila moja ili Rais ateue mmoja lakini hakuna mjumbe aliyeteuliwa”.
Alitaja majina ya walioteuliwa kuwa ni Maria Kashonda (Tec), Jesca Mkuchu (CCT), Humphrey Polepole (Civil Society) na Profesa Palamagamba Kabudi (Kundi la Wasomi).
Lukuvi aliwataja wengine waliopendekezwa na taasisi zao na Rais kuwateua kuwa ni Mwamtumu Malale (Bakwata) na Dk Sengondo Mvungi (NCCR) na Profesa Mwesiga Baregu wa Chadema.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Fredrick Werema alisema katika mchakato wa muswada huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliwasilisha maoni yake mbele ya kamati.
Alisema Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi aliwasilisha kwa kamati mapendekezo ya SMZ, Mei mwaka huu na mapendekezo hayo ikiwamo uteuzi wa wajumbe 166 yalizingatiwa.
 Waacha muswada, wapiga vijembe
Baada ya kurejea katika kikao cha Bunge cha jioni jana, wabunge wa CCM waliopewa fursa ya kuchangia mjadala wa muswada huo walitumia muda mwingi kuwajadili wabunge wa kambi ya upinzani.

Monday, 29 July 2013

Utafiti:Sera ya uwekezaji madini hainufaishi jamii

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha na Mchumi, Balozi Morwa alitoa mapendekezo hayo juzi, wakati akiwasilisha utafiti kuhusu wajibu wa kampuni kwa jamii(CSR),uliofanyika katika machimbo ya Tanzanite Mirerani, wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Arusha. Serikali imeshauriwa kubadili sera ya uwekezaji nchini kwa kulazimisha kisheria kampuni za wawekezaji hasa wa Sekta ya Madini, kutekeleza miradi ya jamii inayozunguka maeneo yao ya uchimbaji badala ya suala hilo kuwa ni la hiari.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha na Mchumi, Balozi Morwa alitoa mapendekezo hayo juzi, wakati akiwasilisha utafiti kuhusu wajibu wa kampuni kwa jamii(CSR),uliofanyika katika machimbo ya Tanzanite Mirerani, wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Morwa akiwasilisha utafiti huo ,ambao uliratibiwa na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Finnish NGO Platform, alisema wamebaini kuwa jamii zinazozunguka migodi ya Tanzanite hazinufaiki ipasavyo.
Morwa alisema utafiti huo, ulihoji watu 350 na nyaraka kukusanywa,wamebaini,wajibu wa kampuni ya wawekezaji kwa jamii ukiwa wa kisheria kama Ghana, utawanufaisha na ikishindika ifutwe na kampuni hizo zilipe kodi kubwa kama nchi nyingine.

Tume ya Uchaguzi itasababisha vurugu

Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne za Jimbo la Arusha Mjini ulifanyika juzi, ambapo Chadema kiliibuka mshindi katika kata zote nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya madiwani wake kutimuliwa uanachama na chama hicho kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama chao kuhusu kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha.
Kinyume na matarajio ya wengi, uchaguzi huo ulikuwa na idadi ndogo sana ya wapigakura kulinganisha na chaguzi zilizopita, kwani kati ya wapigakura zaidi ya 60,000 waliojiandikisha ni 11,042 tu waliojitokeza kupiga kura.
Kwa mfano, Kata ya Elerai inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wapigakura 23,885 lakini waliojitokeza kupiga kura juzi ni 3,824 tu.
Takwimu hizo zinaibua maswali magumu, hasa kuhusu hali inayoendelea kujitokeza ya kudidimia kwa demokrasia nchini.
Takwimu hizo zinatoa tahadhari ya kishindo kwamba huko tuendako sio salama na kwamba nchi yetu inakabiliwa na maangamizi makubwa iwapo Serikali haitaweka mazingira ya kuwawezesha wananchi kushiriki katika chaguzi mbalimbali pasipo kuhofia maisha yao.
Kutojitokeza kwa idadi kubwa ya wananchi kupiga kura katika uchaguzi wa Arusha juzi kumehusishwa na hofu iliyotokana na bomu lililorushwa katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za Chadema mwezi uliopita ambapo watu wanne walikufa na wengine 60 kujeruhiwa, hivyo kusababisha kuahirishwa kwa uchaguzi katika kata hizo hadi juzi.
Lakini pia utendaji mbovu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Tec), katika chaguzi mbalimbali, ukiwamo wa juzi jijini Arusha pia umedhihirisha kwamba huko tuendako hapatakuwa salama iwapo tume hiyo haitafanyiwa mabadiliko makubwa.
Tunalazimika kusema hapa kwamba yafaa tutumie fursa tuliyonayo hivi sasa ya kuandika Katiba mpya kuhakikisha kwamba Katiba hiyo inatuzawadia Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyo huru na yenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Uchaguzi wa juzi jijini Arusha umedhihirisha ulegelege na udhaifu mkubwa uliopo katika Tume hiyo. Pamoja na kuwa na uzoefu wa kutosha katika kusimamia chaguzi mbalimbali, Tume hiyo haionyeshi kubadilika wala kuwa na dira na mwelekeo wa kuiwezesha kwenda na wakati kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa mujibu wa sheria.
Kama tulivyoshuhudia katika uchaguzi wa Arusha juzi, kasoro ambazo zingeweza kuzuilika zimeendelea kujitokeza na nyingi zimekuwa zikijirudia kutokana na watendaji wa taasisi hiyo nyeti kufanya kazi kwa mazoea tu.
Pamoja na wananchi kuwa na shahada halali za kupigia kura na majina yao kubandikwa katika mbao za matangazo, baadhi yao walizuiwa kupiga kura kutokana na Daftari la Wapigakura kutokuwa na majina, maelezo na picha zao.
Baadhi ya majina ya wapigakura yalitokea zaidi ya mara moja wakiwa na namba tofauti, huku wataalamu wa mifumo ya kompyuta wakisuasua kurekebisha matatizo yaliyojitokeza.
Matatizo hayo, ikiwa ni pamoja na Tume kushindwa kuhakiki Daftari la Wapigakura mara kwa mara ni viashiria vya vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kwani wananchi hawatakubali kuondoka vituoni pasipo kupiga kura kwa uzembe tu wa Tume hiyo.
Hii pengine inadhihirisha kwamba haitaweza hata kutumia teknolojia ya kisasa kuhesabu kura mwaka 2015. Matokeo yake ni vurugu zitakazotokana na kasoro hizo.

Bajeti finyu kikwazo cha kupata haki mahakamani-Jaji mkuu Tz



Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amesema ni vigumu mahakama kama taasisi ikaweza kutoa haki kwa wakati kama haitaweza kujitosheleza kimapato.
Aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akizindua kitabu kilichoandikwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta kiitwacho ‘Uhuru wa Mahakama’ na kuchapishwa na Kampuni ya Mkuki na Nyota.
“Uhuru wa kitaasisi ambao haujakamilika ni ule wa kifedha na kimiundombinu, bila huu kukamilika ni vigumu kila mwananchi kuweza kupata haki kwa wakati,” alisema Jaji Chande.
Alisema licha ya kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuongeza bajeti ya mahakama, bado lengo halijafikiwa na kuwa ni vyema muhimili huo ukatengewa fedha za kutosheleza kuendesha shughuli zake.
Jaji Chande alisema kuwa, katika bajeti ya mwaka 2013/14 muhimili huo umetengewa Sh160 bilioni ingawa mahitaji yake halisi ni Sh300 bilioni.
Alisema pia kuwa,kitabu hicho kitawasaidia viongozi wengi ambao wamekuwa wakidhani kuwa mahakama ni chombo cha Serikali. “Wakisoma kitabu hiki wataelewa na wataachana na dhana hii,” alisema Jaji Chande.
Akizungumzia maudhui yaliyopo kwenye kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Chande alisema kuwa kimelenga kumsaidia mwananchi wa kawaida kuijua mahakama na pia watawala, vyama vya siasa na wanasheria watapata mwongozo makini.
Kwa upande wake Jaji Samatta alisema kuwa, mwanzoni kabisa wazo lake lilikuwa ni kuandika juu ya kesi ambazo zimewahi kutikisa nchini kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar.
Alisema, alikuja kuachana na wazo hilo baada ya kuona hapati baadhi ya vielelezo ambavyo vingemwezesha kuandika kitabu hicho.

Saturday, 20 July 2013

TENDWA HAMA CHOHOTE KITAKACHO ANZISHA KAMBI YA MAFUNZO YA KIJESHI TUNAKIFUTA

OFISI ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini imevitaka vyama vya siasa kutii agizo la kutoanzisha kambi za mafunzo ya kulinda amani maarufu kwa jina la mgambo , huku ikisisitiza kwamba itachukua hatua za kisheria kwa chama chochote kitakachoiuka , ikiwemo kukifuta.

Aidha ofisi hiyo imesema kuwa Katiba ya nchi imempa jukumu kila mwananchi kulinda amani na usalama wa nchi, pia kujilinda yeye mwenyewe na mali zake kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola pale anaposikia au kuona mtu anataka kufanya au anafanya uhalifu au amemdhuru mtu.

Kauli hiyo imetolewa  jijini Dares Salaam na ofisi hiyo katika taarifa yake iliyoitoa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Rajab Juma kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa kufutia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutangaza hivi karibuni kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.

Alisema suala hilo lilitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na kuandikwa katika vyombo vya habari kabla ya chama hicho, kuwasiliana na taasisi husika ikiwemo ofisi hiyo ili kupata ushauri kuwa