Thursday, 20 June 2013
Monday, 3 June 2013
Familia ya Pistorius yashtushwa na picha
Familia ya mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini,
Oscar Pistorius, wameshstushwa na picha zilizofichuliwa za bafu
alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.
Shirika la habari la Uingereza la Sky, mnamo
Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya zinazoshukiwa kuwa za bafu ambalo
mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.Polisi walisema kuwa wamechukizwa mno na kufichuliwa kwa picha hizo.
Bwana Pistorius mwenyewe anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa bafu alimokuwa , alisema alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake Jumanne.
Pistorius ni mwanariadha mlevamu asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu bandia au vyuma. Alishiriki michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.
''Familia ya Pistorius ilimuunga mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani , alisema mjomba wake,'' Arnold Pistorius.
''Tunaamini maneno yake , tunampenda na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi hii,''alisema Mjombake Pistorius.
"tumeshtushwa na picha hizi za ajali iliyotokea nyumbani kwa Oscar."
Msemaji wa polisi ameelezea kuwa polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo .
''Kitendo hiki hakikuhitajika na kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,'' alisema polisi huyo.
Pistorius atafikishwa mahakamani Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, kufuatia kukamatwa kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.
Kesi hiyo inatarajiwa kuakhirishwa kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.
Pistorius ameajiri baadhi ya mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea.
Anasema kuwa alimpiga risasi Bi Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya kudhani kimakosa alikuwa mwizi.
Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.
Gesi Mtwara yamtesa JK: Mawaziri watatu mashakani
MAANDAMANO makubwa ya kutaka Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio
cha wakazi wa Mtwara na Lindi wanaopinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka
Mtwara kwenda Dar es Salaam yanaandaliwa.
Baadhi ya wakazi wa Lindi na Mtwara kwa kushirikiana na Chama cha
Wananchi (CUF), Juni 29 mwaka huu wanatarajia kufanya maandamano hayo
kutoka makao makuu ya CUF Buguruni hadi Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Maandamano hayo pia yatakuwa na lengo la kumtaka Rais Kikwete awang’oe
madarakani mawaziri watatu ambao ni Profesa Sospeter Muhongo (Nishati
na Madini), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa),
Emanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani).
Wakizungumza katika mkutano wa kongamano la gesi lililowakutanisha
wakazi wa Lindi na Mtwara, lililofanyika jana jijini Dar es salaam
katika Ofisi za Makao Makuu ya CUF, baadhi ya wakazi hao walisema
wamechoshwa na ahadi za serikali.
Walisema wanaamua kufanya maandamano kwenda Ikulu ili kilio chao
kimfikie Rais Kikwete ambaye kama hatakisikiliza asitarajie wananchi
watarudi nyuma kutetea rasilimali zilizoko mikoani mwao.
Walibainisha kuwa vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ni
ishara ya kuchoshwa na mgawanyo wa rasilimali unaofanywa na serikali
ambayo hivi sasa badala ya kuufikiria mkoa wa Mtwara unahangaika kujenga
bomba la gesi kutoka mkoani humo.
Lipumba aanza
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba,
alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara zimesababishwa na
serikali ya CCM iliyopuuza kilio cha umaskini cha wakazi cha mkoa huo.
Alisema serikali imeanza kushtuka na kwenda kuweka msingi wa ujenzi wa
kiwanda cha saruji baada ya machafuko na upinzani kutoka kwa wananchi.
Alibainisha kuwa nguvu na kuwaziba midomo wanasiasa, wananchi na
wanaharakati kamwe hazitoisaidia serikali kutatua mzozo huo unaoonekana
kuutikisa utawala wa Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa watu wa Mtwara na Lindi wamekosa mahali na fursa za
kuonana na viongozi wao kuzungumzia suala la gesi na matokeo yake
imesababisha vurugu, manyanyaso kutoka kwa polisi waliokwenda kutuliza
ghasia.
Profesa Lipumba alisema serikali inaeneza propaganda za uongo kwamba
wananchi wa Mtwara hawataki Watanzania wengine wafaidi rasilimali
zinazotoka katika mkoa huo.
Alisema wananchi wanataka maendeleo yaanzie katika mkoa huo kutokana
na rasilimali zilizopo ndani yake ikiwemo kujengwa kiwanda cha mbolea na
kiwanda cha kufua umeme wa MW 300 kama ahadi ya serikali ya mwaka 2011
inavyoeleza.
Aliongeza kuwa serikali katika ahadi zake miaka miwili iliyopita
iliwaeleza wananchi wa Mtwara kwamba ingejenga kiwanda cha mbolea na
kujenga kiwanda cha kufua gesi ambayo ingezalisha umeme wa MW 300 kisha
uunganishwe kwenye gridi ya taifa lakini mipango hiyo haikufanyika.
Alisisitiza kwamba endapo mipango ya serikali iliyoainishwa kwenye
ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ingetekelezwa hakuna vurugu wala
matatizo ambayo yangejitokeza.
Alisema wananchi wanaoishi mikoa ya kusini wanadharaulika na kuonekana
hawastahili kupata haki kama watu wa mikoa mingine na kwamba hali hiyo
imewafanya wachoke na kufanya matendo ambayo yataaonyesha kuchoshwa na
kuhitaji mabadiliko.
Wakazi wafunguka
Baada ya Lipumba kuzungumza, wakazi waliokuwapo ukumbini hapo
walipata fursa ya kutoa dukuduku ambapo wengi wao walitaka mawaziri
watatu wang’olewe madarakani.
Waziri Nchimbi anatakiwa kung’olewa kwa sababu ya kutowachukulia hatua
polisi waliokwenda kutuliza ghasia mkoani humo kuendesha vitendo vya
kihalifu, kubaka na kuwanyanyasa wananchi.
Mmoja wa wakazi hao alisema Nchimbi alisema damu ya polisi
iliyomwagika haitapotea bure wakati askari hao walikufa kwenye ajali
wakiwa njiani kwenda Mtwara.
“Polisi hawakufa kwenye mapambano, walikufa kwa ajali ya gari lao sasa
wananchi watalipa vipi vifo hivyo? Waziri Nchimbi alichemka na
hatufai,” alisema mkazi huyo.
Pia wananchi hao walimtaka Waziri Shamsi Vuai Nahodha aondolewe
madarakani kwa kushindwa kuulinda mkoa huo pamoja na kutowawajibisha
wanajeshi waliokiuka maadili ya kazi zao wakati wakilinda usalama mara
baada ya kutokea kwa vurugu.
Mwananchi mwingine alitaka Waziri Muhongo aondolewe kwa kuwa
ameshindwa kusimamia suala hilo la gesi lililo chini ya wizara yake na
hivyo kusababisa vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
Friday, 31 May 2013
Mizengwe yaanza Wizara ya Nishati
BAADHI
ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakishirikiana na wenzao
ndani ya mashirika na taasisi tanzu za wizara hiyo, wamekuwa wakihujumu
jitihada za sasa za kuirejesha wizara katika mstari, Raia Mwema limeambiwa.
Jitihada hizo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari serikalini, zimekuwa pia zikiwahusisha kwa karibu baadhi ya wenyeviti wa bodi za mashirika na taasisi hizo na watendaji wakuu wake ambao wanahisi ya kuwa, kwa mazingira mapya wizarani, ajira zao zinakaribia ukingoni kutokana na ama utendaji binafsi usiokidhi au kwa kushindwa kudhibiti uozo katika taasisi na mashirika yao.
Habari zaidi zinasema sasa upo mtandao wa makundi hayo ulioungana kuendesha kampeni ya kuukataa uongozi wa wizara kwa madai kwamba umekuwa ukiendesha mambo kibabe japo wengi nje ya wizara hiyo wanauona uongozi huo kuwa uliodhamiria utendaji kazi kwa viwango vya juu, urejeshaji imani ya umma kwa vyombo vya utoaji huduma na udhibiti mali na mapato ambao ulikwishakukosekana, na ambao ndio uliokuwa ugonjwa mkubwa ndani ya wizara na katika mashirika na taasisi zake.
Raia Mwema limedokezwa pia kwamba nje ya wizara, taasisi na mashirika yake, mtandao huo unaungwa mkono na baadhi ya wabunge, wengine wakiwa katika kamati zinazohusiana na wizara hiyo, na kwamba mipango inayosukwa ili kupeleka ujumbe kwa mamlaka husika kuwa uongozi wa wizara haufai, uondolewe, ni pamoja na kukwamisha bajeti ya wizara itakayowasilishwa bungeni kiasi cha wiki mbili kuanzia sasa.
Hoja nyingine zanazodaiwa kushadidiwa na mtandao huo kama sababu za ziada kutaka mabadiliko ya uongozi wizarani ni kuwa Waziri mpya, Profesa Sospeter Muhongo, si mwanasiasa, ubunge wake uliompa uwaziri umetokana na yeye kuteuliwa na hilo linawakera baadhi ya wabunge wa majimbo ambao wanaona si vyema wao kuachwa, mtu wa “kuja” akapewa nafasi hiyo kubwa tena katika wizara inayotajwa kuwa tajiri na yenye ulaji kama ya Nishati na Madini.
Ukiacha hilo, Raia Mwema limeambiwa pia ya kuwa madai mengine ni suala ambalo chimbuko lake ni ukabila. Waziri Profesa Muhongo anatoka Mkoa wa Mara ambako ndiko anakotoka pia Katibu Mkuu, Eliachim Maswi, ingawa inafahamika kwamba wanatoka katika maeneo mawili tofauti ya mkoa huo. Kwa mujibu wa madai ya wana mtandao huo, Profesa Muhongo na Maswi kuwa wanatoka katika Mkoa mmoja na sasa wanafanya kazi ofisi moja ni tatizo.
Maswi mwenyewe alipoulizwa na Raia Mwema juu ya madai hayo, mwanzoni mwa wiki hii, alisema hana namna ya kuzuia watu wasizungumze wanayoyataka. Alisema yawepo au yasiwepo, yeye na timu wanayoijenga wizarani wameamua kufanya kazi ili kuleta tija katika maeneo waliyokabidhiwa kuyasimamia.
“ Rais Jakaya Kikwete aliyetuteua hakufanya hivyo ili tuje hapa tuchezecheze. Tumepewa majukumu ya kutekeleza. Hebu niambie, nyumbani kwako siku hizi umeme unakatika mara ngapi?
“Ukiona kuna mawazo kama hayo, ujue tunafanya kazi. Sisi hatutajali yanayosemwa, kipimo chetu ni kama umma unaridhika. Kama unaona baadhi ya kero zilizokuwapo, zilizokuwa ndani ya uwezo wetu, sasa zimepungua kwenye vitu kama umeme, na kama tumeanza kupata stahili yetu kwenye maeneo kama ya migodi ujue wizarani sasa kuna wachapakazi,” alisema Maswi.
Katibu Mkuu Maswi aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Kaimu Katibu Mkuu katikati ya Julai mwaka jana, kiasi cha mwaka mmoja uliopita, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa na David Jairo aliyekuwa ametuhumiwa na Bunge, pamoja na mambo mengine, kwa ubadhirifu.
Aidha, Profesa Muhongo, mmoja wa Watanzania wachache wataalamu wa jiolojia, amejiunga serikalini mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kwanza kama mbunge kupitia nafasi 10 za Rais kuteua wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ni Shirika la Umeme (TANESCO) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Jenerali mstaafu na mkuu wa zamani wa Majeshi, Robert Mbona, Mtendaji wake Mkuu ni Mhandisi Godfrey Mhando.
Mengine ni EWURA ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Simon Sayore; huku Mtendaji Mkuu akiwa Haruna Masebu; Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Balozi Ami Mpungwe na Mtendaji Mkuu ni Dk. Dk Lutengano Mwakahesya; Wakala wa Madini (TMAA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Dk. Yamungu Kayandabila, Mtendaji Mkuu akiwa Mhandisi Paul Masanja.
Mengine ni STAMICO ambalo Mwenyekiti wa Bodi ni Ramadhani Omari Hatibu, Mtendaji Mkuu akiwa Grey Mwakalukwa; GST lililo chini ya Uenyekiti wa Bodi wa Profesa Idrissa Kikula na Mendaji Mkuu akiwa Prof Abdul Mruma na TPDC ambalo Mwenyekiti wake ni Michael Mwanda na Mtendaji Mkuu ni Yona Kilagane.
Kwa karibu mwaka mmoja sasa huduma kama ya umeme imekuwa ikitengemaa baada ya nchi kuwa imeingia katika mgao miaka iliyopita hali iliyoilazimisha Serikali kuanza kutegemea umeme wa kuuziwa na mashirika binafsi ambayo yalichipuka kufuatia mgao huo, mengi yakivuna mapesa mengi katika biashara hiyo na moja kati hayo likizua kashfa ambayo ilimlazimisha aliyekuwa waziri mkuu wa miaka ya mwanzo ya awamu ya Rais Kikwete, Edward Lowassa, kujiuzulu katika kile kilichojulikana kama kashfa ya Richmond.
Ulaji mwingine ambao Katibu Mkuu kwa kushirikiana na viongozi wenzake wameudhibiti ni ule uliokuwa ukifanyika katika sekta ya madini nchini.
Ulaji huo ulikuwa ukizihusisha kampuni tatu za uchimbaji madini nchini ambazo sasa zimetakiwa kulipa malimbikizo ya kodi ambazo awali hazikuwa zikilipwa.
Kampuni hizo ni Tanzanite One inayoendesha uchimbaji wa madini ya vito aina ya tanzanite, Mererani mkoani Arusha, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) na Kampuni ya Resolute (Resolute Mining Tanzania Ltd).
Kampuni hizo zimetakiwa na uongozi wa sasa wa Wizara ya Nishati na Madini kulipa zaidi ya dola za Marekani milioni 5.2 (zaidi ya Sh bilioni nane). Bado haijulikani “uvumilivu” wa awali miongoni mwa waliokuwa viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini uliofanya kampuni hizo kutolipa kodi hiyo ulikuwa unatokana na nini hasa.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema inazo, kampuni hizo zinakabiliwa na shinikizo la kutakiwa kulipa kodi hizo, shinikizo linaloambatana na dalili za kuwekewa vikwazo.
Kati ya vikwazo vinavyoambana na shinikizo la kuzitaka kampuni hizo kulipa fedha hizo ni pamoja na Kampuni ya Tanzanite One kuwa katika hatari ya kupewa leseni baada ya leseni yake ya sasa kwisha muda wake.
Lakini wakati Tanzanite One wakikabiliwa na shinikizo la namna hiyo, kampuni za uchimbaji dhahabu za GGML na Resolute zinaweza kunyimwa leseni za kusafirisha madini nje ya nchi.

Piga vita tumbaku: zuia matangazo,uhamasishaji na udhamini wake
Mei 31, kila mwaka, yaani leo… ni siku ya kupinga matumizi ya
tumbaku duniani. Shirika la Afya Duniani(WHO) na washirika wake
wameitenga siku hii kuwa ni maalum kwa ajili ya kupiga vita matumizi ya
sigara inayotengenezwa kwa tumbaku.
Katika siku hii elimu hutolewa kuhusu athari za
kiafya zitokanazo na tumbaku na pia kuwakilisha sera bora za namna ya
kupunguza utumiaji wa tumbaku.
WHO linasema tumbaku inaua takribani watu milioni 6
kila mwaka na kati ya hao 600,000 sio wavutaji wa tumbaku. Mwaka huu
ikiwa na kauli mbiu “fungia matangazo yanayotangaza, uhamasishaji na
udhamini wa tumbaku.
Tumbaku ni hatari kwa afya na huleta madhara makubwa katika maeneo mbalimbali ya mwili kama vile moyo,ini na mapafu.
Uvutaji wa tumbaku unakuweka katika hatari ya
kupata shambulizi la moyo, kiharusi,kikohozi sugu,mikwamo katika mirija
ya kupitishia hewa,kuharibika tishu za mapafu, saratani hasa ya
mapafu,koo na mdomo,pia madhara ya mishipa ya damu kuifanya kunyauka na
kuwa myembamba hivyo kusababisha shinikizo la damu.
Matumizi ya kilevi hiki ni hatari kwa mvutaji na
yule aliye karibu na mvutaji. Madhara ya kiafya ni yaleyale, tofauti ni
ndogo kuwa muathirika sana ni yule anaevuta. Kwa sababu hii, nchi
mbalimbali duniani zimepiga marafuku matumizi ya tumbaku katika maeneo
yenye mkusanyiko wa watu; kama vile ndani ya vyombo vya usafiri,maeneo
ya starehe na mikutano.
Je unayafamu Madhara ya tumbaku?
Utumiaji tumbaku huleta madhara kwa mwanamke kama
vile ugumba, kijifungua kabla ya wakati, mimba kutoka na kuharibika,
mtoto kufia tumboni, kuzaliwa na uzito mdogo.
Moyo na ubongo
Utumiaji wa tumbaku husababisha mishipa ya damu
kusinyaa/kuwa myembamba na kukamaa kwa mishipa ya damu inayopeleka damu
katika misuli ya moyo, kuchochea mapigo ya moyo kwenda mbio na
kuongezeka kwa lehemu (cholesteral). Matokeo ya haya ni kuharibika tishu
za moyo,shambulizi la moyo, shinikizo la damu, ugonjwa wa
kiharusi,ugonjwa wa kusahau kwa wavutaji wa umri mkubwa, upungufu wa
uwezo wa kiakili, kushindwa kutambua na kupoteza kumbukumbu.
Mapafu
Kuharibika kwa tishu za mapafu na mirija ya
hewa,madhahara yake ni Kikohozi sugu, mikwamo katika njia ya
hewa,kushindwa kupumua vizuri, kupata maambukizi ya mara kwa mara ya
vimelea vinavyoshambulia mfumo wa upumuaji na Saratani ya mapafu.
Taarifa za kitafiti kuhusu utumiaji tumbaku
Wataalamu wa saratani wanaeleza katika tafiti
mbalimbali kuwa asilimia 30% za saratani zote hutokana na utumiaji
tumbaki peke yake.Huku saratani ya mapafu ikiongezeka idadi kwa kina
mama na kua….hii ni kutokana na taarifa ya utafiti uliofanyika nchini
Uingereza,hii inatokana na wanawake wanaotumia tumbaku.Inakadiriwa kuwa
17.2% ya wanaume watumia tumbaku wako katika hatari yakupata saratani ya
mapafu huku wanawake wakiwa ni 11.6%.
Tumbaki inasababisha vifo vya mapema ambavyo
vinazuilika kama watu wasingeitumia,tafiti zinaonyesha kuharibika na
kutoka kwa mimba kwa watumiaji tumbaku,pia watoto huzaliwa na uzito
mdogo na pia kuzaliwa kabla ya mda kufika(njiti),Napia kuna hatari kwa
zaidi ya 1.4 mpaka 3 yakupata vifo vya ghafla kwa mtoto aliye tumboni.
Tatafiti iliyofanyika kwa watoto wa panya wataalam
wamegundua tumbaku hupunguza uwezo wa ubongo wa mtoto kutambua hali ya
hewa kua ndogo hivyo mtoto hupata jeraha la ubongo wakati wakuzaliwa.
Uhanithi umeonekana kwa asilimia 85% kwa watumiaj wa tumbaku
ukilinganisha na wasiotumia, tumbaku ni moja ya kisababishi cha upungufu
wa nguvu za kiume.
Tafiti nyingine ambayo ilichapishwa katika bbc
health news ilisema kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa saratani ya
mapafu kwa upande wakina mama imeongezeka nakukaribia ya wanaume
ukilinganisha na miaka ya nyuma hii imetokana na tabia mpya yakina mama
kujiingiza katika utumiaji na uvutaji tumbaku
Tafiti nyingine ambayo ilifanyika nchini uingereza
ilihusisha madaktari wakiume 34,486 nusu yao walikufa mapema kutoka na
uvutaji sigara,wavutaji wako katika hatari ya kufa mapema kabla ya
kufika umri wa miaka 60-70 mara 3 zaidi ukilinaganisha na wasiovuta.
Kwa nini tumbaki ni hatari kwa afya ya mwili?
Tumbaku ina takribani kemikali 19 ambazo ni
visababishi vya saratani,,na matokeo yake hujitokeza hata baadae
maishani zaid ya maika 20
Tumbaku imebeba kemikali ambayo ni moja ya
kisababishi cha saratani mwili, inaitwa pyrolitic,husababisha vitu
vilivyomo ndani ya chembe hai kuvurugika, kitaalam genetic mutation.
Mvurugiko huu ndio baadaye huleta saratani,pia tumbaku ina kemikali
iitwayo nikotini ambayo husababisha uteja (addiction), husababisha mtu
kuwa na utegemezi(dependency) wa kimwili na kiakili(saikologia) kwa
tumbaku, hivyo mtu hushindwa kustahimili kutoikosa tumbaki na mtu
huridhika pale anapoipata
Namna yakuacha na kijikinga na utumiaji tumbaku.
Zipo zaidi ya mbinu ishirini za namna yakuacha
utumiaji tumbaku,kwanza unatakiwa kujichelewesha zaidi ya dakika kumi
pale unapopata hamu yakuvuta tumbaku halafu fanya jambo lingine lolote
ili kupoteza wazo la hamu ya uvutaji. Fanya hivi kwa mara nyingi zaidi.
Jaribu kukwepa na kuvitambua vitu vinavyokushawishi kuvuta sigara kama
vile kunywa pombe, kusikiliza mziki au kampani ya marifiki wanaovuta
tumbaku.Mazoezi ya viungo vya mwili yanasaidia sana kupoteza wazo la
kutamani tumbaku, kufanya mazoezi kwa dakika 30 kila siku inasaidia, pia
unapokuwepo mahali km ofisini jaribu kunyoosha miguu, mikono, shingo
mgongo, au hata kupiga ‘pushup’,pia kusali kufanya kazi ndogondogo km
kufuma.
Utafiti; Big G inaongeza usikivu, kumbukumbu
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa utafunaji wa Big G
zisizo na sukari unasaidia kuongeza usikivu na kumbukumbu,
kunakosababishwa na urahisishaji wa mtiririko wa damu kuelekea kwenye
ubongo.
Pengine mzazi wako, mwalimu amewahi kukukataza kutumia, kununua
kitu hiki, lakini imebainika Big G inaongeza kumbukumbu usikivu makini
na uchangamfu, kuimarisha afya ya kinywa.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa
utafunaji wa Big G zisizo na sukari unasaidia kuongeza usikivu na
kumbukumbu, kunakosababishwa na urahisishaji wa mtiririko wa damu
kuelekea kwenye ubongo.
Utafiti huo uliofanywa katika Chuo Kikuu cha
Cardiff nchini Uingereza na kuchapishwa mwezi uliopita, ulihusisha
kikundi cha watu ambao walitafuna Big G na wengine wasiotafuna kwa
kuwapa zoezi la kuweka kumbukumbu katika sauti kwa muda wa nusu saa.
Zoezi hilo lilikuwa ni la kusikiliza sauti ya orodha ya namba na kuzitaja kwa mfululizo.
Big G inatoa majibu sahihi
Waliotafuna Big G walitoa majibu sahihi tena kwa haraka zaidi tofauti na wenzao ambao hawakutafuna Big G.
Tafiti zilizotangulia zilionyesha kwamba utafunaji
wa Big-G una faida nyingi mwilini na Dk Chris Miles aliongoza utafiti
huo uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Cardiff.
“ Kutafuna Big-G kunawafanya watu wawe katika tahadhari zaidi.
“Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kitendo hicho
kinasaidia kwa kiasi kikubwa usafirishaji wa damu safi kwenda kwenye
ubongo,” anasema daktari huyo.
Lakini kama utawaambia watu watafune bila kuwapo
kwa Big G, hutapata matokeo yanayofanana. Hivyo inaonekana kuwa,
unahitaji kuwa na Big G ili kurahisisha utafunaji wako.
Madereva wa magari makubwa ya mizigo watakuwa
wamepata habari njema, kwani ikiwa kutafuna Big-G kunaongeza tahadhari
ni wazi kuwa inaweza kuwasaidia kuwa makini zaidi wawapo barabarani
hususani wakati wa usiku.
Hili halijajulikana bado, licha ya ukweli kuwa athari za utafunaji huo hutegemea na aina ya Big-G yenyewe.
Dk Miles anasema watu wengi hutafuna Big-G kwa lengo la kupata
harufu nzuri kinywani na sio kwa madhumuni ya kuongeza usikivu ama
tahadhari.
Utafiti uliofanywa na mchambuzi wa masuala ya
masoko anayefahamika kama Mintel, unaonyesha kwamba asilimia 92 ya
watumiaji wa Big-G wanafanya hivyo wakiwa na lengo la kutengeneza harufu
nzuri vinywani.
Wengu wanaofanya hivyo wanajiongezea hali ya
tahadhari bila ya wao kufahamu. Zipo faida nyingi za kiafya
zinazotokana na utafunaji wa Big-G.
Mapitio mengine yaliyofanywa na watalaam kutoka
katika Chuo Kikuu hicho cha Cardiff mwaka 2011, yalitoa ushahidi kuwa
utafunaji wa Big-G unasaidia sana katika kupunguza msongo wa mawazo.
Utafiti wa Cardiff haukuangalia athari
zinazosababishwa na utafunaji wa Big-G kiafya, lakini utafiti wa Mintel
uliofanyika Disemba mwaka jana ulionyesha kuwa ni watu sita kati ya kumi
wanaotafuna Big-G huamini kuwa zinaweza kuwasaidia kuboresha meno yao.
Ukweli ni kwamba watu hao wako sahihi, hiyo ni kwa
mujibu wa Dk Nigel Carter, Mkuu Taasisi ya Dental Health Foundation ya
nchini Uingereza.
Pamoja na mapitio yaliyobainishwa na Jarida la
British Jounal la Uingereza mwaka 2011, kuna athari iliyojificha katika
bidhaa zenye sukari inayokinzana na zile zisizo na sukari.
Kwa kawaida Big –G zenye sukari zinaongeza ‘asidi’ mdomoni inayoweza kuharibu meno kwa kuathiri mizizi yake.
“Hii ni hatari, nafikiri ulaji wa aina hizo za Big-G ni hatari sana kwa afya ya meno yao,” anasema Carter.
Kuna kiwango kidogo sana cha Big-G zisizo na
sukari zenye ladha inayoweza kuzalisha ‘asidi’ mdomoni. Kama athari zipo
ni kwa kiwango kidogo sana.
Kama ‘asidi’ hiyo itazalishwa kwa kiasi kidogo
sana nadhani itakuwa ni rahisi kupotea tofauti na zile za kawaida
zilizoongezewa sukari.
Athari kubwa ya kutafuna Big-G, ni kusaidia kuongeza mate mdomoni anasema Dk Carter.
Mate yanasaidia utaratibu wa kinga asilia unaojumuisha chumvi
iliyomo ndani yake kwa kuongeza ama kupunguza madini kwenye meno ambayo
yanasababishwa na vyakula vyenye asidi inayotokana na sukari.
Kadri jinsi chumvi inavyokuwa nyingi kwenye mate, ndivyo utaratibu huo unavyokuwa rahisi zaidi.
Big G inalinda meno
Dk Carter anabainisha kwamba kwenye Big-G zenye
sukari, sukari inachanganywa haraka na mate hayo na kuondoa na uharibifu
wa meno.
Pamoja na yote hayo BDHF inasisitiza matumizi ya Big-G zisizo na sukari kwamba zina faida zaidi.
Utumiaji wa vyakula visivyo na sukari ni muhimu
sana katika kulinda fizi. Je, matumizi hayo yanahesabiwa kama kitendo
chanya kwa afya ya fizi na kinywa kwa ujumla?
“Ni kweli kabisa”. Hivyo ni vizuri kutosafisha
meno baada ya kula na badala watu wanapaswa kutafuna Big G kwa muda wa
dakika 10 hadi 20. Hii itasaidia kuongeza mate mdomoni na pia kuboresha
meno yako kwa kuyaondoa katika hatari ya kuoza, anahitimisha Daktari
huyo.
Wenye divisheni ziro 30,000 wapeta
Dar es Salaam. Wanafunzi 30,063 waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyopita, wameula baada ya kupandishwa hadi daraja la nne kutokana na ukokotoaji upya wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyofanywa na Baraza la Mitihani la Taifa (Nacte) na kutangazwa jana.
Marekebisho hayo yalifanyika baada ya kufutwa kwa matokeo ya awali yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu.
Kufutwa kwa matokeo hayo, ilikuwa ni utekelezaji
wa sehemu ya mapendekezo ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, baada ya wanafunzi 240,909 kupata daraja sifuri kwenye matokeo
yaliyotangazwa mara ya kwanza.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema sasa watakaokuwa na
sifuri ni 210,846 sawa na asilimia 56.92 wakati wavulana wakiwa ni
104,259 na wasichana 106,587.
Hiyo ina maana kuwa sasa ufaulu umepanda na kuwa asilimia 43.08 badala ya ule wa kwanza ambao ulikuwa asilimia 34.5.
Dk Kawambwa alisema kutokana na ukokotoaji mpya wa
matokeo ya sasa, idadi ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo kwa daraja
la kwanza mpaka la nne imeongezeka na kufikia wanafunzi 159,747 kutoka
126,847.
Wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 3,242
wavulana wakiwa ni 2,179 na wasichana 1,063 ikiwa ni asilimia 0.88 ya
matokeo yote, daraja la pili ni 10,355 sawa na asilimia 2.8 wavulana
wakiwa 7,267 na wasichana 3,088.
Waliopata daraja la tatu ni 21,752 sawa na
asilimia 5.87 wavulana wakiwa 14,979 na wasichana 6,773, daraja la nne
ni 124,260 sawa na asilimia 33.54 .
Tofauti na matokeo yaliyofutwa, ambayo watahiniwa
waliopata daraja la kwanza walikuwa ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na
wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na
wasichana 1997.
Waliopata daraja la tatu walikuwa 15,426, wavulana
10,813 na wasichana 4,613, waliopata daraja la nne 103,327, wavulana
64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903,
wavulana 120,664 na wasichana 120,239.
Dk Kawambwa alieleza watahiniwa waliosajiliwa
kufanya mtihani huo walikuwa ni 480,029 na waliofanya ni 458,139 sawa na
asilimia 95.44.
Alisema kuwa watahiniwa wa shule waliosajiliwa
kufanya mtihani huo walikuwa ni 411,225 na waliofanya ni 397,138 sawa na
asilimia 96.57 huku wa kujitegemea wakiwa ni 68,804 na waliofanya ni
61,001.
Agizo la serikali
Dk Kawambwa alisema kuwa matokeo hayo yamefanyiwa
kazi kwa kutumia mfumo wa `Fixed Grade Ranges’(ukokotoaji matokeo
usiobadilika) badala ya ule wa zamani wa `Flexible Grade Ranges’
(ukokotoaji matokeo unaoweza kubadilika).
Mei 3, mwaka huu, Serikali kupitia kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi,
alitangaza uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo na kusema kuwa
yatatayarishwa kwa mfumo wa zamani wa `Flexible Grade Ranges’.
Lukuvi alisema kuwa, mapendekezo hayo yalitolewa
na Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza na matokeo hayo na
mapendekezo hayo yaliridhiwa na Baraza la Mawaziri.
Dk Kawambwa jana alisema kuwa, mfumo wa Fixed
Grade Ranges ndiyo uliotumika na kuwa kuanzia sasa mitihani yote itakuwa
ikitumia mfumo huo.
Alisema kuwa pendekezo la Serikali lilishindikana kutumika kwani isingewezekana kuchanganya mifumo miwili kwa wakati mmoja.
“Ni kweli kuwa Serikali iliagiza matokeo haya
yachakatwe kwa mfumo wa 2011 ambao ulikuwa ni `Flexible Grade Ranges’,
kitaalamu siyo sahihi kutumia mifumo miwili kwa wakati mmoja, kwa kuwa
haya matokeo ya 2012 yalitumia mfumo wa `Fixed Grade Ranges’,
isingewezekana kuubadili.
“Kwa hiyo tulishauriana serikalini tukakubali
kufanya `standardisation’ (ukokotoaji) kwa mfumo wa `Fixed Grade Ranges’
kwani kama tungetumia mfumo wa zamani wa `Flexible Grade Ranges’ lazima
yangetokea matatizo,” alisema.
Shule bora na za mwisho
Katika shule kumi bora, Shule ya Wasichana ya
Sekondari ya Kifungilo iliyoko Tanga imetolewa katika kundi hilo kwenye
matokeo mapya na nafasi yake kuchukuliwa na Shule ya Wasichana ya Feza
ya Dar es Salaam.
Baada ya ukokotoaji mpya bado St.Francis Girls ya
Mbeya imebeki kwenye nafasi ya kwanza ikifuatiwa Marian Boys ya Pwani,
Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Canossa ya Dar es
Salaam, Rosmini ya Tanga, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, St. Mary’s
Mazinde Juu ya Tanga na Jude Moshono ya Arusha.
Shule 10 za Mwisho
Shule za Ungulu Morogoro, Mkumba na Tongoni za Tanga na Ndame ya Unguja zimetoka katika kundi hilo la shule za mwisho
Shule za mwisho katika matokeo haya zimeongozwa na
Mibuyuni ya Lindi, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Kikale
ya Pwani, Zirai ya Tanga, Matanda ya Lindi, Kwamndolwa Tanga, Chuno ya
Mtwara, Maendeleo ya Pwani na Maendeleo ya Dar es Salaam.
Monday, 20 May 2013
JK: mnaotaka Urais anzeni kupitapita
*Awataka wafanye mchakato wao bila kuvuruga chama
*Awashushua wanaokacha majimbo na kuwanunia wenzao
*Wabunge wamtaka awang’oe mawaziri watatu ‘mizigo’
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania urais mwaka 2015 kuendelea na mchakato huo.
Rais Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni hatari kwa kuwa yanaweza kukipasua chama. Rais Kikwete aliyasema hayo katika mkutano ndani wa wabunge wa chama hicho uliofanyika jana katika ukumbi wa CCM (white house) mkoani hapa.
Mkutano huo ambao ulianza saa 3.00 asubuhi ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya taifa ikiwamo utekelezaki wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika majimbo na ahadi mbalimbali za viongozi wa taifa.
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya ukumbi huo kilieleza kuwa Rais Kikwete aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais kuwa na tahadhari na watu aliowaita vishoka wa siasa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete alisema watu wa aina hiyo wana tabia ya kula huku na huku kwa kujiingiza katika kambi zaidi ya moja.
“Tuangalie makundi ya urais 2015 yasishambuliane kwa kuvunja chama, wenye nia hiyo ya kugombea waendelee na mikakati yao kujenga chuki kwa makundi mengine.
“Katika hatua hiyo, pia mkumbuke kuwa katika kambi hizo za urais zinatakiwa kujitizama wao na wafuasi wao maana wafuasi wengine hawaaminiki, ” alisema Rais Kikwete.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa ajenda alizokuwa nazo Rais Kikwete ni pamoja na suala la urais na utendaji wa wabunge majimboni.
Rais Kikwete aliwataka wabunge wa chama hicho kubadili mwenendo wa kuyatelekeza majimbo yao na badala yake akawahimiza kujenga tabia ya kutembelea majimbo yao mara kwa mara.
“Hili JK amelisemea kwa ukali kwamba tabia ya baadhi ya wabunge kuhamia mijini na kutelekeza majimbo yao ni hatari kwani mwisho wa siku wananchi watawanyima kura na kuzipeleka upinzani.
“Pia alikemea tabia ya baadhi ya wabunge kununa na kuwachukia watu wengine wenye nia ya kugombea katika majimbo yao. Akasema mbunge asiyetimiza wajibu wake kwa wananchi wake na bungeni ni vigumu kubaki.
“Wanatakiwa kurudi majimboni kwao kusimamia ilani ya chama pamoja na ahadi zao walizoahidi na zile za viongozi wa chama na Serikali ikiwamo ahadi zake kama rais,” alisema.
Kuhusu suala la ukosoaji, Rais Kikwete alisema wabunge wa chama hicho wana wajibu wa kuikosoa Serikali yao lakini akaonya aina ya ukosoaji wenye lengo la kuibomoa Serikali.
“Mnatakiwa kuisimamia Serikali na kuikosoa bila kuibomoa, lakini kuna baadhi yenu mmekuwa mkiibomoa Serikali kwa jinsi mnavyochangia huko bungeni… hilo si jambo jema hata kidogo, waachieni wale wenzetu,”alisema Kikwete.
Chanzo hicho kilieleza kuwa wabunge wamekuwa hawaridhishwi na utendaji wa baadhi ya mawaziri ambao walisema ni mizigo na kutaka waondolewe katika nafasi zao.
Chanzo hicho kilitaja majina ya mawaziri hao wanaodaiwa kuwa ni mizigo kuwa ni Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. David David Mathayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenera Mkangara.
Baadhi ya wabunge walimtaka Rais Kikwete kudhibiti ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri mbalimbali nchini, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.
“Rais anatakiwa kukunjua makucha yake kuondokana na uozo huu katika halmashauri zetu. Haiwezekani waendelee kunyamaziwa, tunatakiwa kuimarisha chama kwa kuangalia namna Serikali inavyoweza kutimiza ahadi kwa wananchi,” kilisema.
Kiliendelea kusema. “Serikali iweze kusaidia katika kutimiza ahadi kwa kutelekeza ilani ya chama, viongozi wa vijiji, kata na vitongoji kuanza kulipwa mshahara maana wamejitolea kwa muda mrefu hivyo huwalazimu kupata ushawishi kutokana na njaa,” kilisema.
Imeelezwa kuwa katika kikao hicho kinachoendelea kitakuwa na ajenda nyingi ambazo zitaibuliwa na wabunge.
Hizo ni pamoja na maslahi ya wabunge, utendaji kwa baadi ya mawaziri na aina ya ukosoaji inayofanywa na baadhi ya wabunge wa chama hicho.
Baada ya mapumziko ya mchana, kikao hicho kiliendelea kwa wabunge kupata nafasi ya kujadili hoja mbalimbali kutokana na hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa asubuhi.
Rais Kikwete anakutana na wabunge hao wakati wenyewe wanaonekana kugawanyika kutokana na kuwapo kundi la wabunge wanaoitetea Serikali na wengine wanaoikosoa.
Miongoni mwa wabunge wanaoikosoa Serikali ya chama hicho waziwazi ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy.
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa wabunge hao machachari walichanwa hadharani na baadhi ya wabunge wanaoiunga mkono Serikali hali inayoonyesha kuwa wabunge hao si wamoja.
Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba alisimama na kueleza kuwa anashangazwa na aina ya ukosoaji unaofanywa na wabunge hao na kusema. “Kama hawataki kufuata maelekezo ya chama wahame,” alisema.

Matajiri watumia nyaraka feki ujenzi wa maghorofa
WATU wanaodaiwa ni matajiri wakubwa, wameendelea kulisumbua Jiji la Dar
es Salaam kwa kupuuza na kukiuka sheria zilizopo, huku wakiendesha
shughuli za ujenzi wa maghorofa kwa kutumia uwezo wa fedha zao. Pia
matajiri hao wamedaiwa kuwasilisha taarifa za uongo Halmashauri ya Jiji
wakiomba kupewa kibali cha ujenzi wa nyumba ya kaiwada, lakini baada ya
kupatiwa hujenga jengo la ghorofa kuanzia tano hadi kumi.
Hata hivyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imegundua taarifa za uongo juu ya ujenzi wa majengo pacha makubwa ya biashara yanayojengwa eneo la Manispaa ya Kinondoni kitalu namba 288 barabara ya Toure Drive Msasani.
Kitendo hicho kiliwafanya wananchi wa eneo hilo kupatwa na hofu juu ya usalama wao na kuiomba Serikali kupitia idara zinazohusika kuchukua hatua.
Kutokana na hali hiyo Manispaa ya Kinondoni, imelazimika kuzuia ujenzi wa majengo hayo pacha tangu Aprili 19, mwaka huu wakati yakiwa hatua ya mwanzo kwa sababu ya kuwa na wasiwasi na mkataba.
Kwa mujibu wa barua ya zuio ya halmashauri ya Kinondoni yenye kumbukumbu KMC/MEK/V22/24 kwenda kwa mmiliki wa majengo hayo, aliyetajwa kwa jina la Silverstone Properties, ilimtaka kusimama ujenzi huo.
Barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Godfrey Mgomi ilifafanua kwamba mkataba huo hauonyeshi idadi halisi ya ghorofa zinazojengwa kwa majengo hayo.
Ilifafanua kuwa, mkataba wake huo hauna taarifa muhimu zinazoendana na ujenzi wa maghorofa jijini Dar es Salaam, jambo ambalo linatia wasiwasi wa ubora wa majengo na usalama wa watu.
Halmashauri hiyo ilitoa onyo kwa mmiliki wa majengo hayo kwa kumtaka atii amri hiyo, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
MTANZANIA ilifika ofisini kwa Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Gerald Urio kujua sababu ya ujenzi huo kuendelea licha ya kuwapo na zuio.
Mhandisi Urio alikiri halmashauri hiyo kuzuia jengo hilo, kutokana na sababu mbalimbali huku akishangaa ujenzi wa jengo hilo kuendelea na kufikia ghorofa mbili.
“Ni kweli tulisimamisha ujenzi wa majengo hayo na hadi sasa ninapozungumza na wewe sijapata taarifa zozote kama yameruhusiwa kuendelea kujengwa,” alisema.

Gari la polisi lakamatwa na bangi
GARI la polisi wa usalama barabarani Mkoa wa Arusha pamoja na askari
polisi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, kwa
kukutwa wakisafirisha magunia 18 ya bangi. Polisi hao wakiwa na gari
hilo, walikamatwa juzi katika maeneo ya Kilema Pofu, Wilaya ya Moshi
Vijijini mkoani hapa. Askari hao walikamatwa Mei 18 mwaka huu na katika
kusafirisha bangi hiyo, walikuwa wakishirikiana na mfanyabiashara mmoja
aliyejulikana kwa jina la Livingstone Urassa (35).
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema askari hao walikamatwa kutokana na mtego uliokuwa umewekwa na askari polisi mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata taarifa kuwa kuna mfanyabiashara anasafirisha bangi kwa kutumia gari ambayo haisimamishwi njiani.
Kamanda Boaz alisema kwamba, baada ya kuwakamata askari hao, walikwenda hadi nyumbani kwa mfanyabiashara huyo na kukuta magunia mengine 16 yakiwa yamefichwa kwenye migomba.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz gari hilo la polisi lilikuwa likiendeshwa na mmoja wa askari hao, ambaye ni koplo Edward na Pc George na kwamba namba za gari hazijafahamika.
Hata hivyo, taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema gari hilo la polisi linashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro.

Subscribe to:
Comments (Atom)