Mei 31, kila mwaka, yaani leo… ni siku ya kupinga matumizi ya
tumbaku duniani. Shirika la Afya Duniani(WHO) na washirika wake
wameitenga siku hii kuwa ni maalum kwa ajili ya kupiga vita matumizi ya
sigara inayotengenezwa kwa tumbaku.
Katika siku hii elimu hutolewa kuhusu athari za
kiafya zitokanazo na tumbaku na pia kuwakilisha sera bora za namna ya
kupunguza utumiaji wa tumbaku.
WHO linasema tumbaku inaua takribani watu milioni 6
kila mwaka na kati ya hao 600,000 sio wavutaji wa tumbaku. Mwaka huu
ikiwa na kauli mbiu “fungia matangazo yanayotangaza, uhamasishaji na
udhamini wa tumbaku.
Tumbaku ni hatari kwa afya na huleta madhara makubwa katika maeneo mbalimbali ya mwili kama vile moyo,ini na mapafu.
Uvutaji wa tumbaku unakuweka katika hatari ya
kupata shambulizi la moyo, kiharusi,kikohozi sugu,mikwamo katika mirija
ya kupitishia hewa,kuharibika tishu za mapafu, saratani hasa ya
mapafu,koo na mdomo,pia madhara ya mishipa ya damu kuifanya kunyauka na
kuwa myembamba hivyo kusababisha shinikizo la damu.
Matumizi ya kilevi hiki ni hatari kwa mvutaji na
yule aliye karibu na mvutaji. Madhara ya kiafya ni yaleyale, tofauti ni
ndogo kuwa muathirika sana ni yule anaevuta. Kwa sababu hii, nchi
mbalimbali duniani zimepiga marafuku matumizi ya tumbaku katika maeneo
yenye mkusanyiko wa watu; kama vile ndani ya vyombo vya usafiri,maeneo
ya starehe na mikutano.
Je unayafamu Madhara ya tumbaku?
Utumiaji tumbaku huleta madhara kwa mwanamke kama
vile ugumba, kijifungua kabla ya wakati, mimba kutoka na kuharibika,
mtoto kufia tumboni, kuzaliwa na uzito mdogo.
Moyo na ubongo
Utumiaji wa tumbaku husababisha mishipa ya damu
kusinyaa/kuwa myembamba na kukamaa kwa mishipa ya damu inayopeleka damu
katika misuli ya moyo, kuchochea mapigo ya moyo kwenda mbio na
kuongezeka kwa lehemu (cholesteral). Matokeo ya haya ni kuharibika tishu
za moyo,shambulizi la moyo, shinikizo la damu, ugonjwa wa
kiharusi,ugonjwa wa kusahau kwa wavutaji wa umri mkubwa, upungufu wa
uwezo wa kiakili, kushindwa kutambua na kupoteza kumbukumbu.
Mapafu
Kuharibika kwa tishu za mapafu na mirija ya
hewa,madhahara yake ni Kikohozi sugu, mikwamo katika njia ya
hewa,kushindwa kupumua vizuri, kupata maambukizi ya mara kwa mara ya
vimelea vinavyoshambulia mfumo wa upumuaji na Saratani ya mapafu.
Taarifa za kitafiti kuhusu utumiaji tumbaku
Wataalamu wa saratani wanaeleza katika tafiti
mbalimbali kuwa asilimia 30% za saratani zote hutokana na utumiaji
tumbaki peke yake.Huku saratani ya mapafu ikiongezeka idadi kwa kina
mama na kua….hii ni kutokana na taarifa ya utafiti uliofanyika nchini
Uingereza,hii inatokana na wanawake wanaotumia tumbaku.Inakadiriwa kuwa
17.2% ya wanaume watumia tumbaku wako katika hatari yakupata saratani ya
mapafu huku wanawake wakiwa ni 11.6%.
Tumbaki inasababisha vifo vya mapema ambavyo
vinazuilika kama watu wasingeitumia,tafiti zinaonyesha kuharibika na
kutoka kwa mimba kwa watumiaji tumbaku,pia watoto huzaliwa na uzito
mdogo na pia kuzaliwa kabla ya mda kufika(njiti),Napia kuna hatari kwa
zaidi ya 1.4 mpaka 3 yakupata vifo vya ghafla kwa mtoto aliye tumboni.
Tatafiti iliyofanyika kwa watoto wa panya wataalam
wamegundua tumbaku hupunguza uwezo wa ubongo wa mtoto kutambua hali ya
hewa kua ndogo hivyo mtoto hupata jeraha la ubongo wakati wakuzaliwa.
Uhanithi umeonekana kwa asilimia 85% kwa watumiaj wa tumbaku
ukilinganisha na wasiotumia, tumbaku ni moja ya kisababishi cha upungufu
wa nguvu za kiume.
Tafiti nyingine ambayo ilichapishwa katika bbc
health news ilisema kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa saratani ya
mapafu kwa upande wakina mama imeongezeka nakukaribia ya wanaume
ukilinganisha na miaka ya nyuma hii imetokana na tabia mpya yakina mama
kujiingiza katika utumiaji na uvutaji tumbaku
Tafiti nyingine ambayo ilifanyika nchini uingereza
ilihusisha madaktari wakiume 34,486 nusu yao walikufa mapema kutoka na
uvutaji sigara,wavutaji wako katika hatari ya kufa mapema kabla ya
kufika umri wa miaka 60-70 mara 3 zaidi ukilinaganisha na wasiovuta.
Kwa nini tumbaki ni hatari kwa afya ya mwili?
Tumbaku ina takribani kemikali 19 ambazo ni
visababishi vya saratani,,na matokeo yake hujitokeza hata baadae
maishani zaid ya maika 20
Tumbaku imebeba kemikali ambayo ni moja ya
kisababishi cha saratani mwili, inaitwa pyrolitic,husababisha vitu
vilivyomo ndani ya chembe hai kuvurugika, kitaalam genetic mutation.
Mvurugiko huu ndio baadaye huleta saratani,pia tumbaku ina kemikali
iitwayo nikotini ambayo husababisha uteja (addiction), husababisha mtu
kuwa na utegemezi(dependency) wa kimwili na kiakili(saikologia) kwa
tumbaku, hivyo mtu hushindwa kustahimili kutoikosa tumbaki na mtu
huridhika pale anapoipata
Namna yakuacha na kijikinga na utumiaji tumbaku.
Zipo zaidi ya mbinu ishirini za namna yakuacha
utumiaji tumbaku,kwanza unatakiwa kujichelewesha zaidi ya dakika kumi
pale unapopata hamu yakuvuta tumbaku halafu fanya jambo lingine lolote
ili kupoteza wazo la hamu ya uvutaji. Fanya hivi kwa mara nyingi zaidi.
Jaribu kukwepa na kuvitambua vitu vinavyokushawishi kuvuta sigara kama
vile kunywa pombe, kusikiliza mziki au kampani ya marifiki wanaovuta
tumbaku.Mazoezi ya viungo vya mwili yanasaidia sana kupoteza wazo la
kutamani tumbaku, kufanya mazoezi kwa dakika 30 kila siku inasaidia, pia
unapokuwepo mahali km ofisini jaribu kunyoosha miguu, mikono, shingo
mgongo, au hata kupiga ‘pushup’,pia kusali kufanya kazi ndogondogo km
kufuma.

No comments:
Post a Comment