Wednesday, 17 April 2013
Monday, 15 April 2013
Raila, Kalonzo waenda Ikulu kwa Rais Uhuru
Lengo ni kufahamiana na kujadiliana kuhusu masuala ya nchi ya Kenya.
Nairobi. Vigogo wa Muungano wa
Demokrasia na Mageuzi (Cord) wa Kenya, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka
wamerudi kutoka nchini Afrika Kusini na kumtembelea Rais Uhuru Kenyatta.
Ujio huo wa Odinga kwa mujibu wa msemaji wake, Dennis Onyango lengo lilikuwa kufahamiana na kujadiliana masuala muhimu ya nchi.
Ujio huo wa Odinga kwa mujibu wa msemaji wake, Dennis Onyango lengo lilikuwa kufahamiana na kujadiliana masuala muhimu ya nchi.
Katika maongezi yao na Rais Kenyatta viongozi hao
wa Muungano wa Cord walisema kwamba watahudhuria sherehe za kufunguliwa
kwa Bunge la 11 nchini humo.
Akidhibitisha mbele ya waandishi wa habari taarifa
za kuhudhuria sherehe hizo za kufunguliwa kwa Bunge hilo kwa viongozi
hao Onyango alisema kwamba hayo ni makubaliano kati ya Uhuru na viongozi
hao.
Alisema viongozi hao pia walijadiliana kuhusu namna ya kukabili masuala yatakayowasilishwa bungeni kwa mtazamo wa kuridhiana.
Kwa sasa Muungano wa Jubilee unaounda serikali
unamiliki mabunge yote mawili, huku maspika Justin Muturi na Ekwe Ethuro
wa Bunge la Taifa na la seneti mtawalia wakiwa wa Jubilee. Kwa hivyo,
inatarajiwa kwamba ingawa Muungano wa Cord utakuwa upinzani kwa
Serikali, hautakuwa na uwezo wa kupinga masuala muhimu.
Kwa upande wake Rais Kenyatta na Naibu wake
William Ruto waliahidi kuhakikisha kwamba upinzani unakua wa maana
katika mabunge yote mawili na kwa Serikali kwa jumla.
“Walisema ni hamu yao kuona vyama vidogo vya upinzani vikitekeleza jukumu lao la kuiangalia Serikali ii isikiuke mipaka katika utendakazi wake,” alisema Onyango.
“Walisema ni hamu yao kuona vyama vidogo vya upinzani vikitekeleza jukumu lao la kuiangalia Serikali ii isikiuke mipaka katika utendakazi wake,” alisema Onyango.
Odinga alienda katika eneo Bunge la Khwisero
kaunti ya Kakamega, ambapo alimwambia Rais Kenyatta asinunue wabunge wa
Cord kuunga mkono upande wa Serikali.
Sh1 bilioni za kuzika viongozi zawakera wabunge
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia mjadala wa Hotuba ya makadirio ya fedha katika Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambapo alitamka kutounga mkono makadirio hayo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Ni zilizotangazwa kutengwa kupitia Hotuba ya Waziri Mkuu.
Dodoma. Serikali ya Rais Jakaya
Kikwete imelaumiwa kwa kutenga Sh1 bilioni kwa ajili ya maziko ya
viongozi huku Watanzania wengi wakilia na umaskini mkubwa.
Shutuma hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki bungeni
kwa nyakati tofauti wabunge akiwamo wa Viti Maalumu Lucy Owenya
(Chadema) na Kangi Lugola (Mwibara-CCM) wakati wakichangia hotuba ya
makadirio ya bajeti katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha
2013/14.
Katika mchango wake Owenya alisema inatia aibu
kuona kiasi kikubwa cha fedha kikitengwa kwa ajili ya maandalizi ya
kuzika viongozi huku mambo muhimu na ambayo ni kipaumbele yakiachwa.
“Ni aibu na fedheha kubwa, hivi mmetenga kiasi
hicho kwani mnajua nani atakufa na lini atakufa ndio maana mnajiandaa
kumzika,” alihoji Owenya.
Mbunge huyo alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa
Serikali imeshindwa kufikiri na hasa namna ya kuwaondolea umasikini na
tabu wanazopata wananchi wake lakini inawaza habari za watu wanaojiandaa
kufa.
Vile vile katika mchango wake Lugola ambaye
alisema asingeunga mkono hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, alihoji sababu za kutengwa kwa fedha hizo bila
kujua nani atakufa lini.
Mbali na hilo, Owenya pia aliilaumu Ofisi ya
Waziri kwa kushindwa kutumia mbinu mbadala za kuzuia matumizi makubwa ya
fedha za walipa kodi zinazotumiwa na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kwenda
Dodoma kufuatilia hotuba ya Waziri Mkuu.
Alimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwatimua wakuu
wa mikoa ili warudi mikoani kwao ili kuokoa fedha za walipa kodi
zinazoteketea katika misafara yao mjini Dodoma.
Sunday, 14 April 2013
Spika asipuuze ushauri wa CAG
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda hivi karibuni alizifanyia mabadiliko kamati za kudumu za Bunge, huku Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ikiunganishwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).
Ikumbukwe kuwa kamati hizi za uangalizi wa mashirika ya umma ziliundwa wakati wa uongozi wa Spika Samuel Sitta na kuwapa wapinzani waziongoze.
Kwa kipindi chote cha uhai wa kamati hizo, kwa kweli zilijitahidi kufanya kazi ya kufuatilia kwa ukaribu fedha za serikali ambazo zimekuwa zikifujwa hovyo bila utaratibu wa wazi.
Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Spika Makinda alibadili utaratibu wa mtangulizi wake Sitta na hivyo akazivunja baadhi ya kamati na kuunda nyingine huku akiziunganisha POAC na PAC.
Lengo la Sitta lilikuwa ni kuongeza uwajibikaji wa serikali na ndiyo maana Bunge liliridhia kamati hizo tatu yaani Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC), Kamati ya Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ziongozwe na upinzani.
Uamuzi wa Spika Makinda kuziunganisha kamati za POAC na PAC umelalamikiwa na wengi akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovic Uttouh wakidai kila moja ilikuwa na majukumu makubwa ambayo hata hivyo hawakuyakamilisha, hivyo kuziunganisha ni kuwatishwa majukumu wajumbe wake.
Hata hivyo, wapo wanaoutazama uamuzi huo kama msukumo wa kisiasa wa Serikali ya CCM kujaribu kukibana chama kikuu cha upinzani bungeni na hivyo kutengeneza utaratibu huo kuwapunguzia madaraka.
Hivi karibuni CAG ameweka bayana kuwa kamati mpya ya PAC inahitaji muujiza wa Mungu kukamilisha kazi zake. Kwamba haiwezi kufikia nusu ya kazi zake za mwaka.
Alisema kabla ya kamati hizo kuunganishwa, POAC ilikuwa na mzigo mzito na sasa umeongezwa, ambapo katika hali ya kawaida itashindwa kufanya kazi ya kuisimamia serikali.
Hatupaswi kupuuza ushauri wa CAG. Huyu ni mtaalamu anayejua masuala ya fedha yalivyo na ugumu wake, hivyo kupendekeza kwake Kamati ya POAC irejeshwe kuna mantiki.
Ni wazi kuwa Spika wa Bunge alikurupuka pasipo kusikiliza mawazo ya wabunge katika uundwaji wa kamati mpya, vinginevyo kusingekuwa na manung’uniko haya tunayoyasikia leo.
Kosa hili la kuifuta kamati muhimu kama POAC kwa malengo ya kisiasa tu, ni tafsiri kwamba viongozi wetu hawajali maslahi ya watu na taifa kwa ujumla.
Tunaamini kuwa Spika wa Bunge kwa mamlaka aliyonayo ataufanyia kazi ushauri wa CAG kwa manufaa ya taifa letu ili kuokoa fedha za umma zisipotee holela.
Saturday, 13 April 2013
Muuza dawa za kulevya aliyeishia kukatwa mkono, mguu
Hata baada ya kuhamia Uswis bado maisha yanaendelea kuwa magumu.Alijikuta akiandamwa na majanga zaidi.
Mbembele anaendelea na simulizi yake, anasema
mwishoni mwa mwaka 1999 alifanikiwa kuhamia nchini Uswizi,
alijiandikisha kama mkimbizi kutoka Msumbiji.
Hali ilivyokuwa nchini Uswizi
“Nilivyofika Uswizi, nilipelekwa moja kwa moja kwenye kambi ya wakimbizi iliyokuwapo jimbo la Debendorf katika Jiji la Zurich, nilijitambulisha kama John ‘Chuma’ Fernando kutoka Msumbiji.
Alipokelewa vizuri na maofisa wa uhamiaji na kupewa chumba kilichokuwa na mahitaji muhimu ya maisha ya mtu wa kawaida.
“Nilivyofika Uswizi, nilipelekwa moja kwa moja kwenye kambi ya wakimbizi iliyokuwapo jimbo la Debendorf katika Jiji la Zurich, nilijitambulisha kama John ‘Chuma’ Fernando kutoka Msumbiji.
Alipokelewa vizuri na maofisa wa uhamiaji na kupewa chumba kilichokuwa na mahitaji muhimu ya maisha ya mtu wa kawaida.
“Nilianza maisha mapya katika kambi hiyo,
nilikutana na wazamiaji wengi kutoka nchi za Afrika mashariki na kati
kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Demokrasia ya Kongo,”
anasema na kuongeza.
“Maisha yalikuwa mazuri kwa sababu tulikuwa
tunapewa kiasi cha dola 600 kila mwezi pamoja na mahitaji na huduma
nyingine kama za michezo na cha kufurahisha zaidi tulikuwa huru kufanya
mambo yetu”.
“Baada ya maisha ya miaka mitatu kambini pale
ilitokea kampeni ya kuwarudisha watu waliokuwa na mazingira mazuri
nchini mwao kutokana na kuporomoka kwa uchumi katika nchi za Ulaya”
“Kiongozi wa kambi yetu ‘Shefa’ alisikia taarifa
halisi za uraia wangu kuwa ni Mtanzania na akaamua kufikisha taarifa
hizo kwa maofisa wa uhamiaji ambao walinipeleka kwa Balozi wa Msumbiji
kwa mahojiano,” anabainisha na kuongeza;“Nilifikishwa kwa Balozi wa
Msumbiji, nilifanya naye mahojiano kuhusu uraia wangu, baadaye
alinishtukia kutokana na kutokuongea vizuri kireno”
Anasema baada kushtukiwa na balozi alimueleza kuwa
yeye ni Mmakonde wa Msumbiji ambaye hakubahatika kwenda shule ndiyo
maana hakuweza kuongea Kireno kwa Ufasaha.
“Nilimwambia natokea Mweda mji wa Msumbiji unaopakana na Tanzania ambapo watu wake walikuwa wanaongea Kimakonde mchanganyiko na Kireno kama mimi”
“Nilimwambia natokea Mweda mji wa Msumbiji unaopakana na Tanzania ambapo watu wake walikuwa wanaongea Kimakonde mchanganyiko na Kireno kama mimi”
Mbembele anaongea kwa kuonyesha ushujaa wa
kumshinda balozi katika maongezi kwa kumdanganya “Balozi alinibembeleza
nirudi msumbiji lakini nilikataa kwa kudai kuwa sababu nilizoondokea
kule bado hazikutatuliwa”.
“Baada ya maongezi, balozi alishindwa kutafuta
sababu ya kuniruidisha Msumbiji hivyo nikaendelea na maisha ya ukimbizi
pale Dubendorf,”anasimulia kuwa wakati akishangilia ushindi wa
kumdanganya balozi kumbe alikuwa ameshawekwa katika kitabu cha watu
watukutu na wenye makosa.
Matukio ya ushirikina na jaribio la kutolewa sadaka
Baada ya kushinda jaribio la kurudishwa nyumbani Mbembele anasema chuki ilizidi baina yake na baadhi ya raia wa Kenya waliokuwapo kambini hapo na kumtengenezea mazingira magumu ya kuishi.
Baada ya kushinda jaribio la kurudishwa nyumbani Mbembele anasema chuki ilizidi baina yake na baadhi ya raia wa Kenya waliokuwapo kambini hapo na kumtengenezea mazingira magumu ya kuishi.
“Nilikosa rafiki, nilihisi kila mtu ni adui yangu.
Sikuwa na chakufanya zaidi ya kumuomba Mungu na kuendelea na maisha kwa
kuwa raia wengi walikuwa wanarudishwa makwao kwa wingi”.
Anasema siku moja akiwa matembezini alikutana na wazungu watatu
ambao walikuwa wanaelekea katika sherehe kubwa ya utamaduni wa Waswizi
ambayo hujumuisha toleo la sadaka ya damu ya binadamu.
“Kule Uswizi tarehe 1 Agosti kila mwaka
huazimishwa sherehe ya nchi nzima, baadhi ya wenyeji husherekea na kutoa
sadaka ya damu kwa miungu na mizimu yao,” anabainisha Mbembele na
kuongeza;
“Wale watu watatu walinibembeleza tukashirikiane
nao katika sherehe hizo mpaka nikakubali kuandamana nao huku tukitembea
taratibu kuelekea katika msitu mkali uliopo ndani ya milima iliyopo
pembezoni mwa mji”
Huku akionyesha dalili za kusisitiza uwepo wa
uchawi uliopitiliza huko Uswizi, Mbembele anasema “Wanasema Tanzania
kuna uchawi, aaah uchawi Ulaya bwana”
“Tulipoingia katikati ya poli tukielekea katika
viwanja maalumu vya sherehe hizo, mtu mmoja kati ya wale watatu
alibadilika ghafla akawa kama sokwe mkubwa mwenye meno ya kutisha kiasi
cha kunitisha na kufanya niishiwe nguvu” anasema na kuongeza kuwa jambo
hilo lilimtisha mno na kumkosesha raha.
KONA YA SHERIA:Unachotakiwa kufahamu kuhusu ndoa kisheria
Kutokana na sheria ya ndoa ya Mwaka 1971, ndoa inatafsiriwa kuwa ni muungano wa hiari baina ya mwanaume na mwanamke, muungano unaokusudiwa kudumu kwa muda wote wa maisha yao.
Kutokana na tafsiri hiyo kuna mambo makuu matatu
yanayotiliwa mkazo na tafsiri hiyo. Kwanza muungano huo lazima uwe wa
hiari yaani usitokane na kushurutishwa ama na mzazi au mtu yeyote yule.
Ikiwa wawili hao watakuwa wamelazimishwa kufunga
ndoa, basi ndoa hiyo haitakuwa ndoa kwa mujibu wa tafsiri ya ndoa katika
sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Wapo ambao wakati mwingine unaweza kuona kwa mfano
mzazi au mlezi anamlazimisha kuoana na fulani kwa sababu zake, ndoa
kama hiyo kisheria sio haki na mwenye kulazimishwa anaweza kuamua
akipenda kuachana na aina hiyo ya ndoa. Jambo la msingi ni kuhakikisha
anayelalamika anakuwa ana ushahidi kwa kile ambacho analalamikia, kwa
mfano anaweza kueleza namna alivyolazimishwa.
Ni kweli inawezekana fulani anafaa kuwa na mwanao,
kisheria inashauriwa kutomlazimisha, badala yake lililo la msingi ni
kushauri, kisha mtu mwenyewe aamue.
Pili ndoa lazima iwe muungano wa watu wawili na ni
lazima watu hao wawe wa jinsia mbili tofauti yaani mwanaume na
mwanamke. Kwa maana hiyo ndoa ya watu wa jinsia moja yaani mwanaume na
mwanaume au mwanamke na mwanamke haitambuliki katika sheria ya ndoa ya
mwaka 1971.
Siku hizi kuna watu wameanza kuja na mambo ya ndoa
za jinsia moja, hizo ni aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa sheria za
Tanzania hazikubaliki.
Tatu ni uhusiano huo uwe wenye kukusudiwa kudumu
kwa muda wote. Lengo la kufunga ndoa ni ndoa hiyo idumu kwa kwa kipindi
chote cha maisha ya wanandoa. Ndio kusema kwamba hakuna ndoa za
mikataba, ya kusema labda mtaishi kwa muda fulani, kwa mfano mwaka
mmoja.
Ndoa inayofungwa ikiwa na lengo ya kuvunjwa baada ya kipindi fulani si ndoa halali kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Ndoa itavunjwa ikiwa kutabainika/kutajitokeza mambo yanayoweza kupelekea ndoa kuvunjika kama inavyobainishwa kwenye sheria ya ndoa na si vinginevyo.
Ndoa itavunjwa ikiwa kutabainika/kutajitokeza mambo yanayoweza kupelekea ndoa kuvunjika kama inavyobainishwa kwenye sheria ya ndoa na si vinginevyo.
Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikaa tu bila
kuangalia namna gani wanaweza kuzingatia sheria za ndoa.Kwa mfano wapo
watu ambao wamekuwa wakiishi tu, huku wao wakifikiri kwamba kuishi kwao
kunatosha kuifanya ifahamike kama ndoa.
Kisheria ni kwamba kuna taratibu zake za
kuzingatiwa ili watu wafahamike kama wanandoa.Kukubali kuishi tu bila
kuzingatia taratibu za kisheria kunaondoa maana halisi ya ndoa hasa kwa
mfano watu wenyewe wanapokuwa hawako tayari kuzifuata taratibu hizo.
Aina Za Ndoa
Kutokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ndoa zimemegawanyika katika aina mbili ambazo ndoa ya mke mmoja ambapo huhusisha mume mmoja na mke mmoja.
Aina ya pili ni ndoa ya wake wengi ambayo mume mmoja anakuwa na wake
zaidi ya mmoja, waweza kuwa wawili ama zaidi kulingana na vile ambayo
wahusika wenyewe wataona inafaa au kulingana na imani zao za dini, hata
hivyo ni lazima kuwepo na makubaliano.Kutokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ndoa zimemegawanyika katika aina mbili ambazo ndoa ya mke mmoja ambapo huhusisha mume mmoja na mke mmoja.
Chadema yatishia kujitoa mchakato wa Katiba Mpya
Dodoma na Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), kimesema kitajitoa katika mchakato wa Katiba
Mpya endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia
Aprili 30, mwaka huu.
Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.
Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Msimamo huo ulitolewa na Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba yake ya
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiitaka
Serikali kuwasilisha muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ili
maeneo kadhaa yafanyiwe marekebisho.
“Katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba tunataka marekebisho ya vifungu vyote vinavyohusu uwakilishi katika Bunge Maalumu la Katiba wa taasisi zilizoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Pia vifungu vyote vinavyohusu ushiriki wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar katika mijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya Muungano.”
Jukwaa la Katiba
Kwa upande wake, Jukwaa la Katiba limesema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kubadili mwenendo wake kuanzia katika utaratibu wa kuwapata wajumbe hao hadi uundwaji wa Bunge la Katiba na wananchi kupiga kura za maoni. Limesema isiporekebisha utaratibu huo, litakwenda mahakamani kusitisha mchakato mzima wa Katiba.
Kumalizika kwa uchaguzi huo kunaashiria kuanza kwa mabaraza ya Katiba Mei mwaka huu, ambayo yatakuwa yakijadili rasimu ya Katiba ambayo imetokana na maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananchi.
Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alisema uchaguzi huo ulikuwa na kasoro zaidi ya 15, ambazo ni itikadi za vyama na udini, rushwa, uchakachuaji, upendeleo, ubaguzi wa makundi ya watu wenye ulemavu na kukosekana kwa mwongozo timilifu wa uchaguzi huo.
Baadhi ya mikoa iliyokumbwa na kasoro hizo ni Dar es Salaam, Arusha, Mara, Singida na Dodoma. “Pia kulikuwa na vurugu katika uchaguzi huu, kukataliwa kwa barua za maombi za baadhi ya waombaji, kutokuwa na tarehe rasmi ya uchaguzi, uandikishaji bandia wa wapigakura, kukosekana kwa orodha ya majina ya wagombea katika mitaa na vijiji.”
Je hii ndiyo njia ya kujenga ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu?
Serikali imekataa ushauri wa wabunge na kusema kuwa itaendelea
kuwaajiri wastaafu mbalimbali nchini hadi hapo soko la ajira
litakapojitosheleza.
Mbali na hilo, jana Serikali ilitangaza bungeni
kuwa kazi za wakuu wa mikoa siyo ajira rasmi, bali ni ajira za kisiasa
ambazo hazipaswi kuhesabiwa.
Akijibu swali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Celina Kombani, alikiri kuwa
bado Serikali inaendelea kutoa ajira kwa watu ambao wamestaafu na kuwa
itaendelea kufanya hivyo kwa siku za usoni.
Alikuwa akijibu swali la Vicent Nyerere
(Musoma-Chadema) ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa
kusitisha kutoa mikataba kwa wastaafu ili wahitimu wanaotoka vyuoni
wapate ajira na kujenga nchi yao.
Mbunge huyo pia alihoji nafasi za wakuu wa mikoa
nchini ambao wengi hufanya kazi wakiwa katika umri mkubwa, huku baadhi
wakiwa wamestaafu utumishi wa umma. Waziri alisema ni kweli kuwa wako
wataalamu wengi wanaohitimu vyuo vikuu hapa nchini ambao wanahitaji
kuingia katika soko la ajira, lakini hupatiwa ajira kulingana na uwezo
na bajeti ya Serikali.
Kuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema “Hilo linatokana na utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha haraka.”
Kombani alizitaja kada ambazo Serikali inatoa
mikataba kwa wastaafu kuwa ni walimu, waganga, wahandisi na wahadhiri wa
vyuo ambaoKuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema “Hilo linatokana na utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha haraka.”
Tuesday, 9 April 2013
Hatua za dharura kutumika kudhibiti dawa za kulevya Zanzibar
Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali italazimika kuchukua hatua za dharura katika kukabiliana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.
Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiwatumia
vijana kwa ajili ya kununua na kusambaza dawa za kulevya, bila ya
kuzingatia athari zitokanazo na biashara hiyo haramu ambayo pia
huzorotesha maendeleo ya kiuchumi kwa taifa.
Maalim Seif alieleza jhayo jana ana katika hafla
ya ufunguzi wa kampeni ya kupunguza matumizi ya dawa za kulevya na
athari zake shuleni, iliyofanyika Shule ya Sekondari ya Lumumba.
Alisema hatua za dharura ni lazima zitumike katika
kuwashughulikia wafanyabiashara hao, vyenginevyo taifa litaendelea
kuangamia kutokana na matumizi makubwa ya dawa za kulevya.
Alifahamisha kuwa wafanyabiashara wa dawa za
kulevya wamekuwa wakijali zaidi maslahi yao, na kuamua kuwatumia vijana
kuendeleza biashara na matumizi ya dawa hizo, jambo ambalo halikubaliki
kwa mustakbali wa Zanzibar.
Aliwahadharisha vijana kuwa makini na
wafanyabiashara hao na kutokubali kutumiwa katika biashara hiyo.
Ufunguzi wa kampeni hiyo iliyoandaliwa na “Sober Houses” chini ya
ufadhili wa Hoteli ya “Double Tree Tanzania”, ulikwenda sambamba na
uzinduzi wa chapisho maalum la kitabu ambacho kitatumika kufundishia
shulenSerikali yarudisha viboko shuleni
Kadhalika alisema Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa sababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakizitumia vibaya jambo ambalo linawarudisha nyuma kimasomo.
Mpoki Bukuku, MWananchi
Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.
Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.
“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.
Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”
Aliyalaumu mashirika yasiyo ya kiserikali na haki za binadamu ambayo yamekuwa yakipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo shuleni na kusababisha kushuka kwa nidhamu kwa kiasi kikubwa.
Kadhalika alisema Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa sababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakizitumia vibaya jambo ambalo linawarudisha nyuma kimasomo.
“Simu tunazipiga marufuku, mwalimu akimkuta mwanafunzi na simu amnyang’anye ndizo zinatuharibia taifa letu.”
Aliwapongeza wabunifu wa mtandao huo akisema ni wazalendo kwani wamekuwa msaada katika jitihada za Serikali kukuza elimu nchini.
“Watu wanapiga kelele Mulugo na Kawambwa wajiuzulu, hata tukijiuzulu haitasaidia, bali kila Mtanzania atoe mchango wake katika elimu ili kuweza kuiendeleza.”
Mwanzilishi wa tovuti hiyo, Faraja Nyalandu alisema itakuwa na manufaa kwa wanafunzi wa Tanzania kwani masomo yanayotolewa yanaandaliwa na walimu wazoefu wenye shahada hivyo wanafunzi watakapoitumia watapata manufaa makubwa.
Maoni ya wadau
Akizungumzia hatua hiyo ya Serikali, Waziri Kivuli wa Elimu Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lyimo aliitaka iache kuangalia mambo madogo ambayo yanachangia kwa kiasi kidogo tu kudorora kwa elimu na kuacha mambo makubwa.
“Kuna mambo makubwa zaidi yaliyotufikisha hapa tulipo, hii ni sawa na kushughulika na matawi na kuacha mizizi. Lazima tuangalie suala hili kwa upana zaidi, kuna ripoti nyingi na nzito hazijafanyiwa kazi mpaka sasa badala yake Serikali inaibuka na kuanza kutangaza vitu vidogo kama hivyo, wafanyie kazi kwanza ripoti ambazo zilitumia pesa nyingi za walipakodi kwani nyingi zina mapendekezo mazuri.”
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa, Rukonge Mwero alisema uzuri wa adhabu ya viboko ni kwamba haipotezi muda”
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba alisema adhabu ya viboko haina maana katika kipindi hiki akisema wanafunzi wanapaswa kupewa adhabu ambazo zinawafundisha kama zile za kufanya usafi na kazi mbalimbali.
“Viboko havifundishi zaidi ya kumpatia mwanafunzi maumivu na kusababisha aichukie shule. Waelimishwe kwa kuelekezwa lakini wakiendelea kukiuka, wapewe adhabu za kufanya kazi mbalimbali.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema walimu hawapati faida yoyote kuwachapa au kutowachapa viboko wanafunzi.
“Hawa viongozi kila kukicha wanazungumza mambo yasiyo na maana, badala ya kuzungumzia masilahi ya walimu wanazungumza kuhusu viboko, hatuelewi wakiamka kesho watasema nini,” alisema Mukoba.
Subscribe to:
Comments (Atom)







