Serikali imekataa ushauri wa wabunge na kusema kuwa itaendelea
kuwaajiri wastaafu mbalimbali nchini hadi hapo soko la ajira
litakapojitosheleza.
Mbali na hilo, jana Serikali ilitangaza bungeni
kuwa kazi za wakuu wa mikoa siyo ajira rasmi, bali ni ajira za kisiasa
ambazo hazipaswi kuhesabiwa.
Akijibu swali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Celina Kombani, alikiri kuwa
bado Serikali inaendelea kutoa ajira kwa watu ambao wamestaafu na kuwa
itaendelea kufanya hivyo kwa siku za usoni.
Alikuwa akijibu swali la Vicent Nyerere
(Musoma-Chadema) ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa
kusitisha kutoa mikataba kwa wastaafu ili wahitimu wanaotoka vyuoni
wapate ajira na kujenga nchi yao.
Mbunge huyo pia alihoji nafasi za wakuu wa mikoa
nchini ambao wengi hufanya kazi wakiwa katika umri mkubwa, huku baadhi
wakiwa wamestaafu utumishi wa umma. Waziri alisema ni kweli kuwa wako
wataalamu wengi wanaohitimu vyuo vikuu hapa nchini ambao wanahitaji
kuingia katika soko la ajira, lakini hupatiwa ajira kulingana na uwezo
na bajeti ya Serikali.
Kuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema “Hilo linatokana na utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha haraka.”
Kombani alizitaja kada ambazo Serikali inatoa
mikataba kwa wastaafu kuwa ni walimu, waganga, wahandisi na wahadhiri wa
vyuo ambaoKuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema “Hilo linatokana na utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha haraka.”
No comments:
Post a Comment