Saturday, 13 April 2013

KONA YA SHERIA:Unachotakiwa kufahamu kuhusu ndoa kisheria



Kutokana na sheria ya ndoa ya Mwaka 1971, ndoa inatafsiriwa kuwa ni muungano wa hiari baina ya mwanaume na mwanamke, muungano unaokusudiwa kudumu kwa muda wote wa maisha yao.
Kutokana na tafsiri hiyo kuna mambo makuu matatu yanayotiliwa mkazo na tafsiri hiyo. Kwanza muungano huo lazima uwe wa hiari yaani usitokane na kushurutishwa ama na mzazi au mtu yeyote yule.
Ikiwa wawili hao watakuwa wamelazimishwa kufunga ndoa, basi ndoa hiyo haitakuwa ndoa kwa mujibu wa tafsiri ya ndoa katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Wapo ambao wakati mwingine unaweza kuona kwa mfano mzazi au mlezi anamlazimisha kuoana na fulani kwa sababu zake, ndoa kama hiyo kisheria sio haki na mwenye kulazimishwa anaweza kuamua akipenda kuachana na aina hiyo ya ndoa. Jambo la msingi ni kuhakikisha anayelalamika anakuwa ana ushahidi kwa kile ambacho analalamikia, kwa mfano anaweza kueleza namna alivyolazimishwa.
Ni kweli inawezekana fulani anafaa kuwa na mwanao, kisheria inashauriwa kutomlazimisha, badala yake lililo la msingi ni kushauri, kisha mtu mwenyewe aamue.
Pili ndoa lazima iwe muungano wa watu wawili na ni lazima watu hao wawe wa jinsia mbili tofauti yaani mwanaume na mwanamke. Kwa maana hiyo ndoa ya watu wa jinsia moja yaani mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke haitambuliki katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Siku hizi kuna watu wameanza kuja na mambo ya ndoa za jinsia moja, hizo ni aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa sheria za Tanzania hazikubaliki.
Tatu ni uhusiano huo uwe wenye kukusudiwa kudumu kwa muda wote. Lengo la kufunga ndoa ni ndoa hiyo idumu kwa kwa kipindi chote cha maisha ya wanandoa. Ndio kusema kwamba hakuna ndoa za mikataba, ya kusema labda mtaishi kwa muda fulani, kwa mfano mwaka mmoja.
Ndoa inayofungwa ikiwa na lengo ya kuvunjwa baada ya kipindi fulani si ndoa halali kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Ndoa itavunjwa ikiwa kutabainika/kutajitokeza mambo yanayoweza kupelekea ndoa kuvunjika kama inavyobainishwa kwenye sheria ya ndoa na si vinginevyo.
Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikaa tu bila kuangalia namna gani wanaweza kuzingatia sheria za ndoa.Kwa mfano wapo watu ambao wamekuwa wakiishi tu, huku wao wakifikiri kwamba kuishi kwao kunatosha kuifanya ifahamike kama ndoa.
Kisheria ni kwamba kuna taratibu zake za kuzingatiwa ili watu wafahamike kama wanandoa.Kukubali kuishi tu bila kuzingatia taratibu za kisheria kunaondoa maana halisi ya ndoa hasa kwa mfano watu wenyewe wanapokuwa hawako tayari kuzifuata taratibu hizo.
Aina Za Ndoa
Kutokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ndoa zimemegawanyika katika aina mbili ambazo ndoa ya mke mmoja ambapo huhusisha mume mmoja na mke mmoja.
Aina ya pili ni ndoa ya wake wengi ambayo mume mmoja anakuwa na wake zaidi ya mmoja, waweza kuwa wawili ama zaidi kulingana na vile ambayo wahusika wenyewe wataona inafaa au kulingana na imani zao za dini, hata hivyo ni lazima kuwepo na makubaliano.

Chadema yatishia kujitoa mchakato wa Katiba Mpya

Dodoma na Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitajitoa katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu.

Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.

Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Msimamo huo ulitolewa na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiitaka Serikali kuwasilisha muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ili maeneo kadhaa yafanyiwe marekebisho.

“Katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba tunataka marekebisho ya vifungu vyote vinavyohusu uwakilishi katika Bunge Maalumu la Katiba wa taasisi zilizoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Pia vifungu vyote vinavyohusu ushiriki wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar katika mijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya Muungano.”

Jukwaa la Katiba
Kwa upande wake, Jukwaa la Katiba limesema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kubadili mwenendo wake kuanzia katika utaratibu wa kuwapata wajumbe hao hadi uundwaji wa Bunge la Katiba na wananchi kupiga kura za maoni. Limesema isiporekebisha utaratibu huo, litakwenda mahakamani kusitisha mchakato mzima wa Katiba.

Kumalizika kwa uchaguzi huo kunaashiria kuanza kwa mabaraza ya Katiba Mei mwaka huu, ambayo yatakuwa yakijadili rasimu ya Katiba ambayo imetokana na maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananchi.

Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alisema uchaguzi huo ulikuwa na kasoro zaidi ya 15, ambazo ni itikadi za vyama na udini, rushwa, uchakachuaji, upendeleo, ubaguzi wa makundi ya watu wenye ulemavu na kukosekana kwa mwongozo timilifu wa uchaguzi huo.

Baadhi ya mikoa iliyokumbwa na kasoro hizo ni Dar es Salaam, Arusha, Mara, Singida na Dodoma. “Pia kulikuwa na vurugu katika uchaguzi huu, kukataliwa kwa barua za maombi za baadhi ya waombaji, kutokuwa na tarehe rasmi ya uchaguzi, uandikishaji bandia wa wapigakura, kukosekana kwa orodha ya majina ya wagombea katika mitaa na vijiji.”

Je hii ndiyo njia ya kujenga ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu?

Serikali imekataa ushauri wa wabunge na kusema kuwa itaendelea kuwaajiri wastaafu mbalimbali nchini hadi hapo soko la ajira litakapojitosheleza.
Mbali na hilo, jana Serikali ilitangaza bungeni kuwa kazi za wakuu wa mikoa siyo ajira rasmi, bali ni ajira za kisiasa ambazo hazipaswi kuhesabiwa.
Akijibu swali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Celina Kombani, alikiri kuwa bado Serikali inaendelea kutoa ajira kwa watu ambao wamestaafu na kuwa itaendelea kufanya hivyo kwa siku za usoni.
Alikuwa akijibu swali la Vicent Nyerere (Musoma-Chadema) ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kusitisha kutoa mikataba kwa wastaafu ili wahitimu wanaotoka vyuoni wapate ajira na kujenga nchi yao.
Mbunge huyo pia alihoji nafasi za wakuu wa mikoa nchini ambao wengi hufanya kazi wakiwa katika umri mkubwa, huku baadhi wakiwa wamestaafu utumishi wa umma. Waziri alisema ni kweli kuwa wako wataalamu wengi wanaohitimu vyuo vikuu hapa nchini ambao wanahitaji kuingia katika soko la ajira, lakini hupatiwa ajira kulingana na uwezo na bajeti ya Serikali.
Kuhusu wastaafu kuendelea kupewa ajira, alisema “Hilo linatokana na utaalamu walionao ambao ni vigumu kuziba nafasi zao kwa kipindi cha haraka.”
Kombani alizitaja kada ambazo Serikali inatoa mikataba kwa wastaafu kuwa ni walimu, waganga, wahandisi na wahadhiri wa vyuo ambao

Tuesday, 9 April 2013

Hatua za dharura kutumika kudhibiti dawa za kulevya Zanzibar













Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali italazimika kuchukua hatua za dharura katika kukabiliana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.
Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiwatumia vijana kwa ajili ya kununua na kusambaza dawa za kulevya, bila ya kuzingatia athari zitokanazo na biashara hiyo haramu ambayo pia huzorotesha maendeleo ya kiuchumi kwa taifa.
Maalim Seif alieleza jhayo jana ana katika hafla ya ufunguzi wa kampeni ya kupunguza matumizi ya dawa za kulevya na athari zake shuleni, iliyofanyika Shule ya Sekondari ya Lumumba.
Alisema hatua za dharura ni lazima zitumike katika kuwashughulikia wafanyabiashara hao, vyenginevyo taifa litaendelea kuangamia kutokana na matumizi makubwa ya dawa za kulevya.
Alifahamisha kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakijali zaidi maslahi yao, na kuamua kuwatumia vijana kuendeleza biashara na matumizi ya dawa hizo, jambo ambalo halikubaliki kwa mustakbali wa Zanzibar.
Aliwahadharisha vijana kuwa makini na wafanyabiashara hao na kutokubali kutumiwa katika biashara hiyo. Ufunguzi wa kampeni hiyo iliyoandaliwa na “Sober Houses” chini ya ufadhili wa Hoteli ya “Double Tree Tanzania”, ulikwenda sambamba na uzinduzi wa chapisho maalum la kitabu ambacho kitatumika kufundishia shulen

Serikali yarudisha viboko shuleni





Kadhalika alisema Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa sababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakizitumia vibaya jambo ambalo linawarudisha nyuma kimasomo.



Mpoki Bukuku, MWananchi
Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ilisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.

“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.

Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”

Aliyalaumu mashirika yasiyo ya kiserikali na haki za binadamu ambayo yamekuwa yakipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo shuleni na kusababisha kushuka kwa nidhamu kwa kiasi kikubwa.

Kadhalika alisema Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa sababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakizitumia vibaya jambo ambalo linawarudisha nyuma kimasomo.
“Simu tunazipiga marufuku, mwalimu akimkuta mwanafunzi na simu amnyang’anye ndizo zinatuharibia taifa letu.”

Aliwapongeza wabunifu wa mtandao huo akisema ni wazalendo kwani wamekuwa msaada katika jitihada za Serikali kukuza elimu nchini.

“Watu wanapiga kelele Mulugo na Kawambwa wajiuzulu, hata tukijiuzulu haitasaidia, bali kila Mtanzania atoe mchango wake katika elimu ili kuweza kuiendeleza.”
Mwanzilishi wa tovuti hiyo, Faraja Nyalandu alisema itakuwa na manufaa kwa wanafunzi wa Tanzania kwani masomo yanayotolewa yanaandaliwa na walimu wazoefu wenye shahada hivyo wanafunzi watakapoitumia watapata manufaa makubwa.

Maoni ya wadau
Akizungumzia hatua hiyo ya Serikali, Waziri Kivuli wa Elimu Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lyimo aliitaka iache kuangalia mambo madogo ambayo yanachangia kwa kiasi kidogo tu kudorora kwa elimu na kuacha mambo makubwa.

“Kuna mambo makubwa zaidi yaliyotufikisha hapa tulipo, hii ni sawa na kushughulika na matawi na kuacha mizizi. Lazima tuangalie suala hili kwa upana zaidi, kuna ripoti nyingi na nzito hazijafanyiwa kazi mpaka sasa badala yake Serikali inaibuka na kuanza kutangaza vitu vidogo kama hivyo, wafanyie kazi kwanza ripoti ambazo zilitumia pesa nyingi za walipakodi kwani nyingi zina mapendekezo mazuri.”

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa, Rukonge Mwero alisema uzuri wa adhabu ya viboko ni kwamba haipotezi muda”

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo Bisimba alisema adhabu ya viboko haina maana katika kipindi hiki akisema wanafunzi wanapaswa kupewa adhabu ambazo zinawafundisha kama zile za kufanya usafi na kazi mbalimbali.

“Viboko havifundishi zaidi ya kumpatia mwanafunzi maumivu na kusababisha aichukie shule. Waelimishwe kwa kuelekezwa lakini wakiendelea kukiuka, wapewe adhabu za kufanya kazi mbalimbali.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema walimu hawapati faida yoyote kuwachapa au kutowachapa viboko wanafunzi.
  “Hawa viongozi kila kukicha wanazungumza mambo yasiyo na maana, badala ya kuzungumzia masilahi ya walimu wanazungumza kuhusu viboko, hatuelewi wakiamka kesho watasema nini,” alisema Mukoba.

Monday, 8 April 2013

Uhuru! Uhuru! Kesho ‘hakunaga’ Kenya


















Kesho kuapishwa akiwa ameshikiwa biblia na mke wake kama ilivyokuwa kwa Obama
Nderemo ,shamra shamra ,na vifijo za kuapishwa kwa Rais wa awamu vya nne nchini Kenya  zitasikika kesho katika Uwanja wa mpira wa Arap Moi.
Kesho Rais mteule wa Kenya,  Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Machi 4 mwaka huu.
Uhuru anachukua nchi hiyo akiwa ni rais wa nne ambapo awali alitanguliwa na baba yake mzazi   Jomo Kenyatta aliyeongoza kuanzia mwaka 1964 mpaka 1978, kisha akafuata mzee Arap Moi  na Mwai Kibaki.
Kuapishwa kwa Rais huyo kulichelewa kutokana na kufunguliwa kwa kesi na mpinzani wake  Raila Odinga ambaye alipinga matokeo hayo kwa kubaini kulikuwa na udanganyifu.
Lakini hata hivyo pingamizi hilo halikufua dafu kwani mahakama ilimuidhinisha Kenyatta kuwa ndiye mshindi halali nchini humo.
Baada ya mahakama ya juu kutoa uamuzi huo ,kwa upande wake Raila Odinga alikubali yaishe kwa kusema kwamba alishatoa ahadi ya kukubaliana na uamuzi wa mahakama.
Uhuru alishatamka wiki iliyopita  kwamba wakati wa kuapishwa hataapa kwa kuinua Biblia bali atasaidiwa na mkewe kama alivyoapishwa Rais Obama wa Marekani.
Akidhibitisha hilo Mkuu wa Majeshi ya Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi alisema  kuwa Kenyatta aliomba kwamba mkewe Margaret Kenyatta amshikie Biblia atakapokuwa akiapishwa.
“Hili ni ombi la rais mteule na itakuwa vyema tukubali ombi lake katika siku hii ya kihistoria,” alisema Jenerali Karangi.
Kenyatta ataweka  tu mkono wake wa kushoto juu ya Biblia ikishikiliwa na mkewe, katika kile anachotaja hatua ya kuachana na mtindo wa awali wa kuapisha marais wa Kenya wakiinua Biblia.
Kesho  Rais Mwai Kibaki atamkabidhi katiba Mpya Kenyatta, ambayo ilianza kutumika mnamo Agosti 2010. Mtindo huu utakuwa wa kwanza tangu nchi hiyo kupata Uhuru.
Sherehe hiyo itafanyika katika Uwanja wa Michezo wa Moi Kasarani, ambapo pia Naibu wa Rais William Ruto ataapishwa.
Shughuli hiyo inatarajiwa kumalizika saa 7.45. Kamati ya Mamlaka ya Ofisi ya Rais tayari ina ratiba ya mpangilio wa shughuli hiyo.
Utaratibu uliowekwa ni kwamba  wageni watasimama  pindi Rais Kibaki anayeondoka madarakani atakaowasili, pia itapigwa  saluti na mizinga 21.
Kenyatta atapambwa kwa vifaa vya mamlaka ambavyo ni pamoja na Mkuu wa Nakshi (CGH), pia atapokea mkuki, ngao na katiba.
Zana hizo zinaashiria mamlaka; kwa mfano Katiba inasimamia Kenya na watu wake, mkuki unasimamia Amiri Jeshi Mkuu ilhali CGH ni heshima kubwa zaidi Kenya.
Mkuki huo ni ule ule uliopitishwa kutoka kwa Hayati Mzee Jomo Kenyatta hadi kwa Rais Mstaafu Daniel Moi, kisha kwa Rais Kibaki na sasa atakabishiwa  Kenyatta.

Kalonzo aaga kwa sherehe
Wakati kesho Uhuru akijiandaa kuapishwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo, Makamu wa Rais anayeondoka madarakani Kalonzo Musyoka aliandaa sherehe kubwa nyumbani kwake kwa lengo la kuwaaga wafanyakazi wenzake.
Wafanyakazi hao wakiongozwa na wakuu wa idara mbali mbali waliandaliwa chakula maridadi kabisa kikisindikizwa kwa hotuba  zenye kuvutia za kumsifia kiongozi huyo.
Kiongozi huyo alisifiwa  kutokana na uongozi wake bora katika wizara hiyo na akiwa msaidizi mkuu wa rais.
Kwenye hotuba yake makamu wa Rais  huyo aliyeandamana na mkewe Pauline Kalonzo, aliwapongeza wafanyakazi wote wa wizara hiyo kutokana na ushirikiano wao akisema kwamba kujitolea kwao kutoa huduma kuliiletea sifa wizara hiyo.

Tuesday, 2 April 2013

Maghorofa 100 Dar feki, Serikali ina kigugumizi

 Kwanini Serikali haichukui hatua kwa majengo hayo 100 yaliyobainika kuwa hayajajengwa kwa kuzingatia viwango? Wenye akili timamu wanaweza kuendelea kujiuliza maswali mengi zaidi na kujibu wanavyoweza.


Dar es Salaam.
Kuporomoka jengo lililopo Mtaa wa Indira Gandhi Jijini Dar es Salaam, huenda ikawa mwanzo tu wa kuporomoka majengo mengine zaidi hasa kufuatia matokeo ya tume iliyoundwa mwaka 2006 iliyobaini zaidi ya majengo 100 Jijini Dar es Salaam yamejengwa bila kuzingatia viwango.
Kwanini Serikali haichukui hatua kwa majengo hayo 100 yaliyobainika kuwa hayajajengwa kwa kuzingatia viwango? Wenye akili timamu wanaweza kuendelea kujiuliza maswali mengi zaidi na kujibu wanavyoweza.
Wapo wanaoweza kusema rushwa ndio inasababisha mambo mengi kutofanyiwa kazi kwa ufasaha, lakini mbele ya sheria utaombwa utoe ushahidi, hapo bila shaka patafanya wengi kubadili maneno kwamba aaah labda Serikali inaendelea kufanya mchakato, mpango mkakati, mkakati yakinifu nk dhidi ya majengo hayo.
Kubomoa jengo lenye ghorofa 16 au hata chini au zaidi ya hapo baada ya kulibaini halijazingatia viwango, ni lazima uwe na uso mgumu. Baadhi ya wananchi wanasema wenye majengo bila shaka hawawezi kutulia wakisubiri sheria ifanye inachotakiwa kufanya, hapo ndipo ugumu unapoanzia.
Pinda analo na kujibu
Baadhi ya watu wanafikiri kuondolewa madarakani kwa viongozi walio katika wizara husika na sakata hili akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye ofisi yake ilichunguza na kubaini maghorofa zaidi 100 kuwa ni feki, kunaweza kuwa ni mojawapo ya mambo muhimu kwa sasa.
Mke na watoto wafukiwa
Licha kwamba jengo hilo liliporomoka saa 2.30 asubuhi, baadhi ya watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa njia ya simu na wengine wakipiga kelele za kuomba msaada.
Idd Baka ambaye alikuwa akiwasiliana na mkewe ambaye aliegesha gari huku ndani kukiwa na watoto wake wawili alikwenda dukani kununua bidhaa, mara jengo hilo likaporomoka, alikuwa akiwasiliana nae hadi majira ya mchana simu ya mke wake haikuwa inapatikana.
Vifaa duni
Ni dhahiri kwamba endapo kungekuwapo na vifaa vya kutosha katika zoezi la uokoaji lingewezaa kufanikiwa kwa  muda mfupi na kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapata majeruhi wakiwa hai.  
Katapila latumika
Cha  ajabu na aibu kwa taifa kutokuwa tayari kwa kuwa na vifaa vya kuokolea kwani tangu saa 2:30 hadi ilipofika saa 4.30 ndipo lilipatikana katapila moja ambalo nalo halikuwa na tija kutokana na kuwapo kwa uwezekano wa kuwakandamiza au kuwajeruhi zaidi  watu waliofukiwa na kifusi hicho.
Kutokana na kutokuwepo na vifaa vya kukatia nongo waokoaji iliwachukua takribani dakika 15 kukata nondo zilizokuwa zimemkandamiza.
Umati wa watu ulivamia kifusi na kuanza kukisomba kwa mikono  ili hali jambo hili lilikuwa kama mchezo wa kuigiza ambao umegharimu uhai wa watu zaidi ya 35 pamoja na kuharibu magari yaliyobondwa na kuwa kama chapati takribani matano.
Mashuhuda
Ali Mparang’ombe mmoja wa mafundi wa jengo hilo anasema kudondoka kwa jengo hilo ni mtiririko wa majengo mengine kutokuwa katika viwango vinavyotakiwa.


“Ndugu yangu mimi ni fundi nilikuwa nimeingia ndani, lakini nilitoka kwenda upande wa pili kutafuta chai kwani leo (Ijumaa iliyopita) ni sikukuu mama lishe hawakuwepo wengi hapa”anasimulia Mparang’ombe na kuongeza:
“Ndipo kwa kule nilisikia kishindo kikubwa, kuja kuangalia ni jengo nililotoka takribani dakika 15 tu limeanguka, nimepoteza watu muhimu sana ambao tulikuwa tukifanya sote kazi, sasa sijui itakuwaje”.
Mparang’ombe anasema jengo hilo lilikuwa likijengwa chini ya viwango kwani katika ndoo 12 za mchanga walikuwa wakichanganya saruji mfuko mmoja.
Majengo mengi feki
“Hapa kama kama ndoo 12 mfuko mmoja wa saruji unategemea nini, na ni majengo mengi hapa mjini ambayo yamejengwa kwa aina hii, hivyo ni kudra za Mwenyezi  Mungu zinahitajika”anasema Mparang’ombe.
“Jengo hili lilipofika ghorofa ya 12 lilisimamishwa kujengwa na ghorofa ya 15 lilisimamishwa tena lakini hatujui alikuwa anatumia njia gani hadi akawa anaruhusiwa kuendelea na ujenzi,” anasema.
Kibali cha jengo lililoanguka
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala, Kheri Kessy alisema mwaka 2007 walitoa kibali kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kushirikiana na ‘Aliraza Investment Limited’ kujenga jengo la ghorofa 10.
Alipotakiwa kueleza kwa nini hawakuchukua hatua baada ya kuendelea kujengwa hadi kufikia ghorofa zaidi ya 10,  alisema hawahusiki, ila kuna taasisi zingine za Serikali zinazosimamia majengo zinatakiwa kuulizwa.
Matokeo ya tume yanapuuzwa
Mwaka 2006 Tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ilibaini kuwa zaidi ya maghorofa 100 yaliyopo jijini Dar es Salaam yalikuwa chini ya viwango.
Idadi hiyo ni tone tu la maghorofa yaliyo chini ya viwango nchi nzima ambayo bila shaka kuyabomoa ugumu unakuja pale wamiliki wake kuwa vigogo na wafanyabiashara mashuhuri.
Hali kadhalika akiwa bungeni wakati wa majumuisho ya Ofisi yake Bungeni mwaka 2008/09, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ofisi yake ingechukua hatua za makusudi dhidi ya majengo ili kuzuia vifo kama hivi visivyo vya lazima. Kufumbia macho mambo ndiko leo kumesababisha watu zaidi ya 35 kuuawa, achilia mbali mali zingine yakiwemo magari.

Jamii:Kwanini Tanzania haiendelei haraka

Ombaomba wa India wanafanya jambo kukushawishi kumsaidia.Kwa mfano nikiwa katika mitaa ya New Delhi, nilikutana na ombaomba, walianza kunichezea muziki na michezo mingine, kabla ya kunisogelea na kuomba

 
New Delhi, India. Hivi karibuni nilikuwa nchini India, ni baada ya kuwa nimechaguliwa kati ya waandishi pekee wawili kutoka Tanzania, kuungana na waandishi wengine 16 kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa ajili ya mafunzo na pia kuripoti mkutano baina ya India na nchi za Afrika, uliofanyika Jijini New Delhi.
Zaidi ya New Delhi, nilitembelea pia miji mingine kama vile Noida, Agra, Mumbai na kadhalika. Ninachoweza kusema ni kuwa kuna mambo mengi ambayo Tanzania inapaswa kujifunza kutoka India. India ni taifa linalokua haraka, wapo ombaomba lakini hata ukizungumza nao unakuta ‘wanafikiri  tofauti’ na sisi;wana tofauti kubwa na wa hapa nchini.
Tofauti ya ombaomba wa Tanzania na India
Ombaomba wa India wanafanya jambo kukushawishi kumsaidia.Kwa mfano nikiwa katika mitaa ya New Delhi, nilikutana na ombaomba, walianza kunichezea muziki na michezo mingine, kabla ya kunisogelea na kuomba.
Mtoto mwenye mmoja mwenye umri wa miaka nane hivi, alijichora uso kama paka usoni, hakika utatamani kumwangia maana anachekesha. Japo si wote wanaofanya kitu kabla ya kuomba, wengi ni wabunifu.
Hata nilipotembelea katika miji mingine, ikiwemo Mumbai bado niliendelea kubaini ubunifu wa watu hawa, kule nilikutana kwa mfano na dada mmoja aliniita akanifunga ua mkono wa kulia, nikawa nafikiri ni kama ‘karibu mgeni’…kule alikuwa ni ombaomba, baadae alianza kuniomba fedha.Haina maana kwamba ombaomba ni kazi nzuri, ninachotaka kukieleza hapa ni kwamba ni kuonyesha namna gani wenzetu wana ubunifu.
Hata wafanyakazi nchini, unakuta wengi sawa wanakuwa ofisini lakini wapo ambao ni wazembe, wengine wako bize na mitandao ya kijamii, badala ya kufanya mambo ya maana, mwisho wa mwezi ndio wa kwanza kuuliza kama mshahara umeshatoka au bado.
Baadhi ya wanandoa, ni mafisadi, anatumia fedha kuhonga, kulewa badala ya kuimarisha nyumba yake. Ulioa au kuolewa kwanini kama unashindwa kutulia na familia yako? Wengi wazuri wa kulalamika wanapata fedha ndogo, je unakitumiaje kidogo unachokipata?
Wengine wanahonga zaidi kuliko kufanya maendeleo, japo wachumi wanashauri kwamba ukitaka kuwa na maendeleo hakikisha angalau unaweka akiba asilimia 15 ya kipato chako, ili mwisho wa mwaka ufanyie kitu fulani kikubwa.
Wapo wanaoweza kuuliza aaah kipato chenyewe kidogo nitaweza kuwekeza hiyo asilimia 15? Jiulize je, kipato chako kingepungua au mwajiri wako angepunguza mshahara kwa asilimia 15 ungefanyaje?
Kama ungeishi, maana yake ni kwamba unapaswa kuishi na kufumbia macho hiyo asilimia 15 kwa kuiweka akiba ili hatimaye mwisho wa siku ufungue mradi au kuendeleza shughuli zako, hii ndio siri muhimu ya kufanikiwa katika maisha.Fanya kama hiyo asilimia 15 haiko, tafuta njia zingine za kuishi.
Mojawapo ya sababu ya kutokua haraka kwa maendeleo hapa nchini, ni tatizo la ubunifu na uwezo wa kuthubutu.Wengi wa Watanzania ni maarufu wa kulalamika, badala ya kuchukua hatua.Muda mwingi unapotea.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma India na Tanzania
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma Tanzania ina maswali mengi hasa namna inavyofanya kazi zake. Ni kama iko tu kufurahisha wakubwa, sio kusaidia kweli taifa, ndivyo watu wengi wanavyoona.
Kwa mfano mwisho wa viongozi kujaza fomu za kueleza mali zao na kuzirudisha kwenye sekretarieti hiyo ilikuwa Disemba 31 mwaka jana. Hata hivyo wale ambao hawajatangaza mali, hakuna hatua za kisheria wanazochukuliwa.

Saturday, 30 March 2013

Odinga akwaa kisiki tena



Nairobi.Mahakama ya Juu ya Kenya imemthibitisha Uhuru Kenyetta kuwa Rais halali mteule wa nchi hiyo pamoja na mgombea mwenza wake, William Ruto.


Mahakama hiyo iliwathibitisha Kenyatta na Ruto jana katika uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo uliowapa ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Machi 4, 2013, iliyofunguliwa na mpinzani wao mkuu katika kinyang’anyiro hicho, Waziri Mkuu, Raila Odinga.


Odinga katika kesi hiyo aliituhumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo kuwa ilihujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi, Kenyatta.Hata hivyo, katika uamuzi wake jana Mahakama hiyo ilisema kwamba Kenyatta na Ruto walichaguliwa kihalali katika uchaguzi huo mkuu.

Maaskofu waijia juu Serikali



Dodoma. Wakristo wamesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuwasaidia ili waishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, wakati akisoma tamko la Maaskofu wa madhehebu ya Kikristo Tanzania katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa lililopo eneo la Jamatini.

Katika tamko hilo alilolisoma kwa niaba ya Maaskofu wote, Kinyunyu alisema kuwa umefika wakati ambao Wakristo wamechoka na vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya waumini wa dini zingine.


“Tatizo ni kuwa Serikali inashindwa kuchukua hatua mapema, makanisa yanachomwa, migogoro inazidi, lakini hakuna hatua zozote ambazo Serikali inachukua katika kunusuru hali hiyo, tumechoka,” alisema.


“ Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa muda mwafaka kwa kila jambo ambalo linatokea kwa Wakristo na hata inapoonyesha kuwa imechukua hatua haionyeshi sana kujali juu ya yale wanayofanyiwa Wakristo. Askofu huyo alisema kuwa matokeo yanayotokea Zanzibar mathalan, Wakristo wanaoishi huko yamewasababishia hofu hivyo wengi kuanza kuvikimbia visiwa hivyo na kukimbilia Tanzania Bara.


Kwa mujibu wa Askofu Kinyunyu, suala la uchomaji wa makanisa hadi sasa limeshindwa kupatiwa ufumbuzi na kila kukicha bado makanisa yanaendelea kuchomwa moto akahoji Serikali kukaa kimya maana yake nini.

Aidha, tamko hilo limeitaka Serikali kuweka utaratibu mzuri na ufafanuzi wa kina kuhusu uchinjaji wa nyama ambao umekuwa ni tatizo kubwa hapa nchini. “Hapa litolewe tamko kila mtu kwa imani yake achinje mwenyewe siyo kuanza kulaumiana au kumpa haki mmoja akachinja na mwingine akaachwa. Tunaomba sana ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo ili kuondoa mgogoro baina yetu na wenzetu.”
wamekuwa wakifanyiwa, lakini akasisitiza kuwa wanatakiwa kupigana kwa maombi na ndiyo silaha kubwa ya ushindi.


Katika hatua nyingine, wakati Wakristo wakiwa na hofu ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka watu wasiofahamika wamevamia makanisa matatu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini na kuvunja ofisi za wachungaji na wainjilisti.