Bukombe. Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) limesema
uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji utakaofanyika Desemba
14, mwaka huu, utatoa picha halisi ya uwezo wao wa kushika dola katika
Uchaguzi Mkuu 2015.
Pia, Chadema imewaomba wananchi wote waliofikisha
umri wa kupiga kura kujitokeza kujiandikisha katika daftari la makazi na
daftari la kudumu la wapigakura wakati uandikishaji utakapoanza.
Halima Mdee, ambaye ni mwenyekiti wa Bawacha na
mbunge wa Kawe, alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Kilimahewa wilayani Bukombe mkoani hapa.
Mdee alisema chama hicho kimejiandaa kuchukua dola
mwakani, lakini hilo litafanikiwa ikiwa uchaguzi wa serikali za mitaa
utatoa dira kamili ya ukombozi wa pili wa taifa.
“Watanzania, uchaguzi huu wa Desemba 14 ndiyo
utatoa dira kamili… utakuwa ni uchaguzi muhimu kuliko hata huo wa
mwakani wa madiwani, wabunge na urais kwani unapotaka kujenga nyumba
madhubuti lazima uanzie msingi imara na ndiyo maana tunasema uchaguzi
huu ni muhimu,” alisema.
“Wanawake wenzangu, acheni kuhongwa chumvi na
kanga na CCM. Kama wameshindwa kuwaletea maendeleo kwa miaka 52 ya
uhuru, ni maendeleo gani tena wanayotaka kuyaleta?” alihoji Mdee huku
wananchi wakimjibu, “hakuna, hakuna… wameshindwa”.
Naye katibu mkuu wa baraza hilo, Grace Tendega
alisema ifikapo Novemba 23, mwaka huu wananchi wajitokeze kujiandikisha
katika daftari la makazi ili kuwawezesha kushiriki ipasavyo katika
uchaguzi huo wa vijiji, vitongoji na mitaa.
“Tunawaomba wananchi ambao mmefikisha miaka 18
kujitokeza kwa wingi ili kuanza kuifuta CCM kuanzia ngazi ya chini kwa
kuanzia huko ili mwakani wakati wa uchaguzi ujao, tuwe tumewaonyesha
mlango wa kuondokea,” alisema Tendega.
Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Desemba 14, wakati Uchaguzi Mkuu utakuwa Oktoba mwakani.
kupigiwa kelele na CCM lakini hazina nguvu kutokana na kutodaiwa mahakamani kama hazitatolewa.
“Leo hii eti wanasema kuna haki za watoto, wazee,
afya, wasanii lakini wanashindwa kusema kwamba haki hizo Ibala ya 20
(1)(2) zimefungwa kudaiwa makahakani…ikataeni pindi itakapokuja kupigiwa
kura ya maoni kwani haina kitu na badala yake maoni yenu yametupwa
kando,” alisema Mwaifunga

No comments:
Post a Comment