Dodoma.Serikali
bado haijaamua utaratibu utakaotumika katika kupanga madaraja ya
watahiniwa wa mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka huu.
Naibu Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema juzi jioni katika
Viwanja vya Bunge kuwa, uamuzi juu ya utaratibu utakaotumika kupanga
matokeo hayo utaamuliwa katika vikao vya watendaji wa wizara hiyo.
“Baada ya
mkutano wa Bunge kumalizika, tutakwenda kukaa na kuamua utaratibu
tutakaotumia lakini sasa sina majibu,” alisema na kuongeza kuwa baada ya
wiki mbili atakuwa katika nafasi ya kusema utaratibu utakaotumika kupanga matokeo hayo.
Hivi karibuni Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, katika taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli zake katika kipindi cha Machi hadi Desemba 2013, iliitaka Serikali kusitisha utaratibu mpya wa upangaji wa matokeo ya mitihani.
Mabadiliko
hayo, daraja ziro ambalo kwa muundo wa zamani lilikuwa na alama 34-35
sasa litakuwa daraja la tano likiwa na alama 48-49.
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alikaririwa
na vyombo vya habari akisema muundo huo mpya utatumika kwa mzunguko
katika kipindi cha miaka minne.
Daraja la
kwanza halijaathiriwa na muundo mpya, kwani alama zake zimebaki pale
pale ambazo ni 7-17. Daraja la pili alama za muundo wa zamani zilikuwa
18-21 na sasa ni 18-24. Alama za daraja la tatu zilikuwa 22-25 na chini ya muundo mpya zitakuwa 25-31, wakati daraja la nne alama zimebadilika.

No comments:
Post a Comment