
abunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mmoja wa Baraza la wawakilishi Zanzibar wameteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Wabunge hao ni Faith Mtambo na Mary Chatanda (wote viti maalumu (CCM), Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangala na Ali Mzee Ali ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika orodha hiyo ya wajumbe wapya, pia yumo Wilson Masilingi ambaye alikuwa Mbunge wa Muleba Kusini mpaka mwaka 2010, ambapo alishindwa katika kura za maoni ndani ya chama chake na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaeleza kuwa , Rais Jakaya Kikwete amemteua kwa kipindi cha pili, Balozi Christopher Liundi kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu na kwamba uteuzi huo umeanza rasmi Machi 6,mwaka huu.
Liundi aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2010, huku wajumbe wake wakati huo wakiwa ni Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu, Rose Lugembe, Shabani Mnubi, Nuru Milao, Joseph Chilambo, Wilfred Nyachia, Makumba Kimweri, Dk Aggrey Mlimuka na Issa Suleiman.
Wajumbe wengine wa bodi hiyo mpya ni Aggrey Mlimuka, Dash-Hood Mndeme, Dk Ali Mndali na Balozi mstaafu Abdi Mshangama. Kwa nini wana siasa wapewe nafasi za uongozi? Kwa nini sisi watanzania tusifike sehemu tuone kwamba kuwa mwanasiasa siyo kwamba unaweza kufanya kila kitu?
Je ni kujenga ajira kweli huku kama wale watu wenye madaraka tayari wataendelea kulimbikiziwa madaraka?Wale vijana amabao wanamemaliza vyuo vyetu je wao wataenda kufanya kazi wapi au hadi wajiunge na CCM?
No comments:
Post a Comment