Ombaomba wa India wanafanya jambo kukushawishi kumsaidia.Kwa mfano
nikiwa katika mitaa ya New Delhi, nilikutana na ombaomba, walianza
kunichezea muziki na michezo mingine, kabla ya kunisogelea na kuomba
Kwa mfano mwisho wa viongozi kujaza fomu za kueleza mali zao na
kuzirudisha kwenye sekretarieti hiyo ilikuwa Disemba 31 mwaka jana. Hata
hivyo wale ambao hawajatangaza mali, hakuna hatua za kisheria
wanazochukuliwa.
New Delhi, India. Hivi
karibuni nilikuwa nchini India, ni baada ya kuwa nimechaguliwa kati ya
waandishi pekee wawili kutoka Tanzania, kuungana na waandishi wengine 16
kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa ajili ya mafunzo na pia kuripoti
mkutano baina ya India na nchi za Afrika, uliofanyika Jijini New Delhi.
Zaidi ya New Delhi, nilitembelea pia miji mingine
kama vile Noida, Agra, Mumbai na kadhalika. Ninachoweza kusema ni kuwa
kuna mambo mengi ambayo Tanzania inapaswa kujifunza kutoka India. India
ni taifa linalokua haraka, wapo ombaomba lakini hata ukizungumza nao
unakuta ‘wanafikiri tofauti’ na sisi;wana tofauti kubwa na wa hapa
nchini.
Tofauti ya ombaomba wa Tanzania na India
Ombaomba wa India wanafanya jambo kukushawishi kumsaidia.Kwa mfano nikiwa katika mitaa ya New Delhi, nilikutana na ombaomba, walianza kunichezea muziki na michezo mingine, kabla ya kunisogelea na kuomba.
Ombaomba wa India wanafanya jambo kukushawishi kumsaidia.Kwa mfano nikiwa katika mitaa ya New Delhi, nilikutana na ombaomba, walianza kunichezea muziki na michezo mingine, kabla ya kunisogelea na kuomba.
Mtoto mwenye mmoja mwenye umri wa miaka nane hivi,
alijichora uso kama paka usoni, hakika utatamani kumwangia maana
anachekesha. Japo si wote wanaofanya kitu kabla ya kuomba, wengi ni
wabunifu.
Hata nilipotembelea katika miji mingine, ikiwemo
Mumbai bado niliendelea kubaini ubunifu wa watu hawa, kule nilikutana
kwa mfano na dada mmoja aliniita akanifunga ua mkono wa kulia, nikawa
nafikiri ni kama ‘karibu mgeni’…kule alikuwa ni ombaomba, baadae alianza
kuniomba fedha.Haina maana kwamba ombaomba ni kazi nzuri, ninachotaka
kukieleza hapa ni kwamba ni kuonyesha namna gani wenzetu wana ubunifu.
Hata wafanyakazi nchini, unakuta wengi sawa
wanakuwa ofisini lakini wapo ambao ni wazembe, wengine wako bize na
mitandao ya kijamii, badala ya kufanya mambo ya maana, mwisho wa mwezi
ndio wa kwanza kuuliza kama mshahara umeshatoka au bado.
Baadhi ya wanandoa, ni mafisadi, anatumia fedha
kuhonga, kulewa badala ya kuimarisha nyumba yake. Ulioa au kuolewa
kwanini kama unashindwa kutulia na familia yako? Wengi wazuri wa
kulalamika wanapata fedha ndogo, je unakitumiaje kidogo unachokipata?
Wengine wanahonga zaidi kuliko kufanya maendeleo,
japo wachumi wanashauri kwamba ukitaka kuwa na maendeleo hakikisha
angalau unaweka akiba asilimia 15 ya kipato chako, ili mwisho wa mwaka
ufanyie kitu fulani kikubwa.
Wapo wanaoweza kuuliza aaah kipato chenyewe kidogo
nitaweza kuwekeza hiyo asilimia 15? Jiulize je, kipato chako
kingepungua au mwajiri wako angepunguza mshahara kwa asilimia 15
ungefanyaje?
Kama ungeishi, maana yake ni kwamba unapaswa
kuishi na kufumbia macho hiyo asilimia 15 kwa kuiweka akiba ili hatimaye
mwisho wa siku ufungue mradi au kuendeleza shughuli zako, hii ndio siri
muhimu ya kufanikiwa katika maisha.Fanya kama hiyo asilimia 15 haiko,
tafuta njia zingine za kuishi.
Mojawapo ya sababu ya kutokua haraka kwa maendeleo
hapa nchini, ni tatizo la ubunifu na uwezo wa kuthubutu.Wengi wa
Watanzania ni maarufu wa kulalamika, badala ya kuchukua hatua.Muda
mwingi unapotea.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma India na Tanzania
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma Tanzania ina maswali mengi hasa namna inavyofanya kazi zake. Ni kama iko tu kufurahisha wakubwa, sio kusaidia kweli taifa, ndivyo watu wengi wanavyoona.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma Tanzania ina maswali mengi hasa namna inavyofanya kazi zake. Ni kama iko tu kufurahisha wakubwa, sio kusaidia kweli taifa, ndivyo watu wengi wanavyoona.








