Miezi kadhaa baada treni ya kubeba abiria jijini Dar
es Salaam kusitisha safari zake kutokana na ubovu, imeelezwa kuwa hali hiyo ni
kutokana na uchakavu wa injini.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Reli
Tanzania, Charles Ndenge alisema treni hiyo imekuwa ikiharibika mara kwa mara,
kutokana na injini zake kutumika kwa muda mrefu, huku treni hiyo ikifanya kazi
tofauti na ilivyoundwa.
Elizabeth Edward
Dar es Salaam. Miezi kadhaa baada treni ya kubeba abiria jijini Dar es Salaam kusitisha
safari zake kutokana na ubovu, imeelezwa kuwa hali hiyo ni kutokana na uchakavu
wa injini.
Mkuu wa Masoko
wa Kampuni ya Reli Tanzania, Charles Ndenge alisema treni hiyo imekuwa ikiharibika
mara kwa mara, kutokana na injini zake kutumika kwa muda mrefu, huku treni hiyo
ikifanya kazi tofauti na ilivyoundwa.
“Treni hii
ilitengenezwa kwa safari za mbali, hata hivyo imeshafanya kazi kwa muda mrefu
na injini zake zimechoka ndiyo maana zinafanyiwa marekebisho niwahakikishie
watumiaji huduma ya usafiri itarejea kama kawaida” alisema Ndenge.
Alifafanua
mpaka sasa matengenezo yamefika katika hatua nzuri na wiki mbili zijazo huduma
hiyo itaanza kufanya kazi tena.
Ili kuepukana
na adha ya kusitishwa kwa huduma hiyo mara kwa mara, Ndenga alisema kwamba
kunahitajika treni iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya safari za mjini.
“Usafiri wa
treni kwa safari fupi unaweza kuwa imara endapo kutakuwa na treni
zilizotengenezwa maalumu kwa ajili ya kazi hiyo mikakati ambayo inaendelea,
lakini hatuwezi kuizungumzia kwa sasa”alisema.
Aliweka wazi
kwamba matengenezo ya injini hizo yanaendelea na wiki mbili zijazo huduma hiyo
ya usafiri inaweza kurejea.
Kusitishwa kwa
huduma hiyo ya usafiri kumeleta kero kubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam, ambao
wamekuwa wakitegemea njia kukabiliana na changamoto ya foleni hasa nyakati za
asubuhi na jioni.
Wakizungumza na
Mwananchi kwa nyakati tofauti, baadhi wa watumiaji wa usafiri huo walidai kuwa
kukosekana kwa treni kumesababisha kuathirika kwa shughuli zao za kiuchumi
kutokana na kutumia muda mwingi kwenye foleni.
“Treni ilikuwa
inasaidia sana, lakini sasa hivi tunalazimika kupoteza muda mwingi kwenye
foleni za daladala, hivyo tunaomba wahusika waliangalie suala hili kwa umakini
zaidi usafiri wetu walala hoi urejee”alisema Erick Kivambala mkazi wa Ubungo
Jasmine Ally mkazi wa Tabata alisema kukosekana kwa usafiri huo, kumeleta
changamoto kubwa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu kwenye
daladaa kutokana na kusumbuliwa makondakta.
“Ingawa hata
watu wazima tumeathirika lakini wanafunzi ndiyo wameathirika zaidi, maana treni
ndiyo ilikuwa inawabeba bila matatizo yoyote, siku hizi unawakuta kwenye vituo
vya daladala wakikunjana mashati na makondakta”alisema.
Kwa upande wake
Ofisa Habari Mkuu Wizara ya Uchukuzi, William Budoya Ndenge alikiri kuwepo kwa
kadhia hiyo na kueleza kuwa treni maalum kwa ajili ya safari za mjini
zinahitajika kukabiliana na changamoto za usafiri katika maeneo hayo.
“Ili usafiri
huu uwe wa uhakika ni lazima ziwepo treni ambazo zimetengenezwa maalum kwa
ajili ya kutoa huduma za usafiri maeneo ya mijini,”alisema.
Kuhusiana na
madai ya kuwepo kwa mvutano kati ya TRL na Wizara ya Uchukuzi katika suala la
uendeshaji wa treni hiyo, Budoya alisema jambo hilo halina ukweli na wamekuwa
wakishirikiana bega kwa bega kuhakikisha huduma hiyo inarejea.
“Sisi tunatunga
sera na TRL ni waendeshaji tunatambua fika kwamba treni hili ni mkombozi kwa
wakazi wengi wa Dar es Salaam, ndiyo maana tunaweka nguvu zote kuhakikisha linarejea”alisema
Budoya

No comments:
Post a Comment