Historia imeendelea kuandikwa katika siasa za Tanzania
baada ya leo, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kujitoa CCM na kujiunga na
chama kimojawapo kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-(Ukawa).
Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es
Salaam leo katika mkutano na wanahabari Sumaye amesema chama alichojiunga
miongoni mwa vinne (Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD) vinavyounda Ukawa
kitajulikana baadaye.
Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Dar. Historia
imeendelea kuandikwa katika siasa za Tanzania baada ya leo, Waziri Mkuu
mstaafu, Frederick Sumaye kujitoa CCM na kujiunga na chama kimojawapo
kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-(Ukawa).
Sumaye anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kujiondoa
chama tawala katika historia ya Tanzania, ambapo waziri mkuu wa kwanza kuhama
CCM ni Edward Lowassa aliyejiunga Chadema miezi michache iliyopita.
Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam leo katika
mkutano na wanahabari Sumaye amesema chama alichojiunga miongoni mwa vinne
(Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD) vinavyounda Ukawa kitajulikana baadaye.
Waziri Mkuu huyo aliyehudumu Uwaziri Mkuu miaka yote
10 ya utawala wa awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amesema
amejiunga Ukawa kwa kushirikiana na viongozi wa umoja huo awatumikie Watanzania
kwa kasi kubwa baada ya uchaguzi kwa kuwa anaamini Ukawa utashinda.
Amesema kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM na kuvurugwa
kwa mchakato wa uchaguzi kumechangia wananchi kukata tamaa hali iliyochochea
uungwaji mkono wa upinzani tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
“Na sasa kuzuia wimbi la mabadiliko ni kazi kubwa
sana. Naamini Ukawa watashinda uchaguzi huu, CCM wamezubaa wakidhani watashinda
wakati wananchi wamechoka, wanahitaji mabadiliko” alisema na kuongeza.
“Sijajiunga Ukawa kwa kuwa mgombea wake wa urais
anatoka Kanda ya Kaskazini, wala kwa kuwa viongozi wengi waandamizi wanatokea
huko la hasha bali kutaka kutoa uzoefu wangu nikishirishiana na Lowassa katika
uongozi wa nchi, alisema na kudai dhana kwamba hakuna maisha ya kisiasa nje ya
CCM imepitwa na wakati.

No comments:
Post a Comment