Igunga. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe amesema sababu ya kutaja
mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ni kuzuia mianya ya watu wachache
kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
Zitto
alitoa kauli hiyo jana mjini Igunga, wakati akitangaza mshahara wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Zitto, kwa mwaka
kiongozi huyo wa nchi analipwa Sh384 milioni ambazo ni wastani wa Sh32
milioni kwa mwezi bila kukatwa kodi.
Hatua
ya Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya
Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), kutaja mshahara wa rais inakuja wiki
moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri mkuu kuwa ni Sh26 milioni kwa
mwezi pasipo kukatwa kodi
Zitto
alisema hoja ya msingi si kiasi wanancholipwa viongozi hao walioajiriwa
na wananchi bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho. Alisemaha ni
jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa Sh200,000 kwa
mwezi ukikatwa kodi huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea
mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi.
Alisema
katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara na
malipo mengine huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na
marupu rupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya
ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
“Kwa
hiyo hata kesho kama Dk Slaa akiwa Rais na akataka kupunguza mshahara
wake kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa
ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka Serikalini,” alisema Zitto.
Zitto
alisema kuwa kitendo cha Serikali kuyafungia magazeti ya Mwananchi na
Mtanzania, hakikuzingatiwa kulingana na uwazi uliowekwa kwa kuandika
uwazi wa viwango vya mishahara.
Alisema
kuwa waziri aliyehusika kufunguia magazeti hayo hakufikiria kwa makini
kutokana na kuwa na uelewa mdogo na kuongeza kuwa hakuna kosa lolote
linalopelekea kufungiwa magazeti hayo kutokana na ukweli ulioandikwa
No comments:
Post a Comment