LEO katika ukurasa huu wa habari za Afrika tunakuletea matukio muhimu ambayo yalitawala katika vyombo mbalimbali vya habari ndani ya mwaka huu kuanzia mwezi Januari.
Ikiwa wewe ni mfuatiliaji wa habari za Afrika hakika utakuwa umesikia mambo mengi yaliyotokea katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na mauaji katika nchi zilizoingia katika machafuko ya muda au muda mrefu.
Mengine yaliyotokea ni baadhi ya wanajeshi kuamua kuwaondoa kinguvu viongozi waliopo madarakani na kuzitawala nchi hizo kimabavu.
Afrika Kusini
Miongoni mwa matukio ambayo yalijiri katika nchi hizo tukianzia na Afrika ya Kusini, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alitangaza maombolezo nchini humo kutokana na mauaji ya wachimbaji madini 38 yaliyosababishwa na polisi wakati wakiandamana kudai kuongezewa mishahara, tukio ambalo lilihuzunisha watu wengi Afrika.

Pia Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa Kanisa la Anglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa Ellinah Wamukoya alisema kwamba uamuzi huo umeonesha heshima kubwa kwa kina mama.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa Ellinah Wamukoya alisema kwamba uamuzi huo umeonesha heshima kubwa kwa kina mama.
Tukio lingine kubwa kwa Afrika ni kuhusu mwana mama Ellinah Wamukoya (61) sasa atakuwa kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufalme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasa za kihafidhina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku Kanisa la Anglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa Jimbo la Captetown, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia suala hilo kwa haraka.

Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyombo vya habari, askofu huyo wa Jimbo la Capetown, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na mbingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumwapisha askofu na wale siyo mtu mweusi, mwafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.
Somalia
Mwaka huu Wabunge wa Somalia waliandika historia ya nchi hiyo, baada ya kufanya uchaguzi uliotawaliwa na amani na kumchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais wa nchi hiyo.
Waliopiga kura hizo ni wabunge pekee ambapo kulikuwa na wagombea 12 wa kinyanganyiro hicho cha kuongoza taifa hilo ambalo linakabiliwa na machafuko ya amani.

Licha ya Mataifa mbalimbali kuipongeza Serikali ya Somalia, kwa kufanya uchaguzi wa amani baada ya kipindi kirefu, Kundi la Al-Shabaab limesema kwamba haliwezi kuitambua serikali hiyo.
Pia Al-Shabaab wameanza kuuza nyama ya fisi katika mji wa Bandari Kusini mwa Somalia, kama njia ya kukusanya pesa kwa ajili ya kuendesha oparesheni zake za kijeshi.
No comments:
Post a Comment